MGENI KUTOKA MJINI SEHEMU YA 3
SIMULIZI........MGENI KUTOKA
MTUNZI........SHAX GOLD
NO..........003
Devota aliwaonesha wakina amina uyo kijana mwenyewe ambae ni jeydan aliekuwa juu ya paa ya nyumba akiweka ile solar panel yake mda uwo bibi yake aliingia ndani ili kuandaa upishi wa usiku pale njee alibakia mzee mrisho na jeydan tu peke yao.
“Mhh! Jamani kweli yule kijana ni mzuri alafu ni mtana shati vibaya mno sijawai kuona kwenye kijiji ichii..!!!” aliongea grace uku macho yake yote yakiwa kwa jeydan anae funga solar.
“Shikamoooo!! Mume wetuuuu!!!!” devota aliongea kwasauti ya juu uku akimtazama mzee mrisho kule alipo maana wao walikuwa wanapita kwenye kinjia tu kidogo dogo, cha ajabu mcharuko wa kijiji amina alikuwa kimya ana mtazama tu jeydan lakini irene yeye alimtazama mara moja tu na kuendelea kuchapa lapa ila grace na amina wao walikuwa wana mtazama tu jeydan wana kenua tu.
“Marahabaaa!! wanawake wangu karibuni...!!!”
Mzee mrisho aliongea uku akiwa tazama na jeydan nae aliwa tazama tu na kutabasamu kisha akaendelea na ufundi wake.
“Asante tuna muogopa uyo mzee...!!!”
basi mara nyingi wakina devota wakipita kwa mzee mrisho lazima wataniane na ndo ilivyo kuwa sikuiyo aliongea ni devota peke yake wenzake walikuwa wana mtazama jeydan kasoro irene basi waliondoka pale, wakati wapo mbele sasa amina alikuwa bado ana mtazama jeydan japo wapo kwenye majani majani awezi akamuona jeydan sasa alivyo ona hamu yake imeisha ilibidi ageuke mbele ili aendelee na safari na wenzake akajikuta amevamia fukutu la majani basi alipiga mzinga aka dondoka chini na ndoo yake ya maji ikadondoka maji yote yaka mwagika.
Sangapi wenzake wasiangue kicheko adi irene alie fahamika kwa upole nae alicheka vibaya mno amina aliinuka pale chini chapu akatazama kwenye paa ya nyumba aliyopo jeydan akumuona apo sasa ndipo alipo pata nafasi ya kuongea kwa ukali.
“yani nyinyi mbwaa kweli nyie!! Baada mnisaide apa nilivyo dondoka nyie ndo kwanza mna nicheka...!!” amina aliongea kwa ukali uku akiwatazama wenzie wanao mcheka.
“Nawewe nae shoga yangu umezidi kushangaa kama vile misukule ya mama tatu..” devota aliongea uku akishusha ndoo yake chini na kuendelea kucheka.
“We ropoka tu subili ya kukute ndo utajua vizuri..”
grace aliongea na kutua ndoo yake chini akachukua ndoo ya amina aka muekea maji kisha akaiweka tena kichwani na wenzake pia walifanya ivyo ivyo. Kisha wakaondoka zao mishale ya jioni kabisa baada ya jeydan kupata chajio (chakula cha jioni) alichukua simu yake ya touch kisha akaondoka na babu yake ampeleke sehemu pa kulala walivyo kuwa njiani mzee mrisho alimwambia mjukuu wake.
“Jey mjukuu wangu..”
“Naam babu..”
“Ichi kijiji mimi nimezaliwa hapa nimekulia hapa na nimeoa hapa na nita kufa hapa na nita zikwa hapa, mimi ichi kijiji nakijua vizuri sana babu yangu ivyo chukua hii dawa hapa itakusaida sana usiku waleo...”
Aliongea mzee mrisho na kumpa dawa ya kienyeji mjukuu wake basi jeydan akukataa alipokea babu yake akampa maelekezo jinsi ya kutumia ile dawa walivyo karibia na kwakina juma mbavu mzee mrisho aligeuza na kuondoka zake basi jeydan alienda mpaka kwenye iyo nyumba akamkuta juma mbavu akiwa ana kura zake ugali na samaki uku akiwa amekaa kwenye kigoda basi jeydan alimpa salamu lakini juma mbavu akuitikia jeydan akuelewa alimsalimia tena ikawa ivyo ivyo akaona isiwe kesi ilibidi aulize pakwenda kulala.
“Ety ndugu yangu ndo tunalala wapi vile..?”
Juma mbavu alimkata jicho baya jeydan uku mashavu yake yakivimba kutokana na tonge alililo liweka mdomoni alinyoosha tu kidole kuonesha chumba anacho paswa kwenda kulala basi jeydan alienda kwenye icho chumba kilichopo njee yani chumba cha njee ndani kulikuwa na kibatari tu ndo kinacho toa mwanga mule ndani basi jeydan akupapenda kabisa mule ndani jinsi palivyo ila sasa ata fanyaje ilibidi ajibwage akachukua shuka lake alilo kuja nalo akajifunika uku akichati kidogo juma nae aliingia ndani akafunga mlango na kutoa shati kisha akamlingishia jeydan kifua kwa kutikisa kama vile makalio mpaka jeydan akaoga akahisi ata bakwa ila juma ni mbovu sana wa kulala alipo kusa tu kitanda alikuwa tayari wa juzi jeydan alichukua dawa yake akaitumia na kulala nayeye mishale ya saa nane usiku mida mibovu.
ITAENDELEA......
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO
Maoni
Chapisha Maoni