ZOMBI WA DAR EPISODE 08
ZOMBI WA DAR
ABELUKA
EPISODE YA 08
«RIP MAMA TONY.»
TULIISHIA....
"naona umeongea tena hahahaha. utamfanya Nini Sasa yule mama maana hata Mimi kanike..." Aliongea same hata hakumaliza sentensi akatulia na kusimama chap akabaki anashangaa kuona gari la Mr Hance likiwa nimepack nje ya nyumba yake.
"Gari la nani lile mkuu?.."aliuliza zombi
"La bosi wangu..." Same alijibu mala mlango wa lile gari unafunguliwa akatoka Mr hance akiwa ndani ya suti yake nyeusi akageuka na kumtazama same.
ENDELEA....
"zombi twende usiogope nitakutambulisha kama mdogo wangu..."same alianza kutembea kuelekea mbele alipo Mr hance.
"Karibu bosi ni baraka kubwa kutembelewa na mtu mashughuli Kama wewe twende ndani mweshimiwa.." same aliongea kwa utu na utulivu akionyesha unyenyekevu mkubwa kwa mr hance.
Lakini Mr hance alikuwa akitazamana na zombi mda huo.
"Huyu ni rajah kweli kabisa Sasa inakuwaje ananiangalia Kama hanijui? Mbona hajashituka kuniona au amepoteza kumbukumbu?.." Mr hance aliongea moyoni kidogo amani ikarudi akaamini zombi hakumbuki chochote kilichotokea zamani.
"Bosi huyo ni mdogo wangu chizichizi, karibu ndani tafadhal.." same alisukuma geti kwa kutabasam na kuingia ndani, zombi akafuatia Mr hance akabaki pale nje
"Bosi wangu ingine ndani bwana.."
"Kijana siwezi kukaa nyumbani kwako ni kubaya.." Mr hance hakupepesa maneno aliongea kwa dharau kubwa na kuondoka..
"Daah Sasa sijui alifuata nini hapa?au alikuja kunitukana tu mjinga huyu aliona kama nafasi binti yake. Ngoja nikajipikie chakula mie .." same aliingia ndani kinyonge pamoja na zombi.
Walipoingia ndani same akaenda kuandaa chakula Zombo akaingia bafuni kuoga maana alijichafua sana. Baada ya mda mfupi alitoka bafuni akaingia chumba cha same akabadili nguo, nguo alizovaa zilikuwa za same. Alitoka akiwa smart kidogo na kwenda kukaa sebuleni.
"Same.." aliita zombi akiwa amekaa kwenye sofa.
"Nini zombi?." same aliitika akiwa jikoni anaendelea kupika.
"Bosi wako ni Kama nimewahi kumuona mahali.."
" Umeanza wenge wewe, Ulimuona wapi?.."
"Nimesahau, sikumbuki!.."
"Embu washa tv Hapo ucheki sinema zetu naona akili zishaanza kukuruka.." same alipuuza Yale maneno ya zombi akaendelea kupika.
USIKU KWA MR HANCE
Mr hance alikuwa mezani anapata chakula na binti yake enjoy
"Enjoy tayari umeachana na yule kijana?.."
"Ndiyo hatuna mahusiano nahisi utakuwa umefurahi sasa. usije ukamfanya chochote kijana wa watu sina mahusiano nae tena?.."aliongea enjoy akaendelea kula
"Vizuri binti, ila nimekuchagulia mwanaume kutoka familia ya sikamanga huyo ndo atakuowa sawa?.."
"Nani huyo baba?.." aliuliza enjoy kwa jazba akaacha mpaka kula.
"Jordan atakuowa.."
"Lakini simpendi jordan.."enjoy alipandisha sauti
"Utajifunza kumpenda mkiwa ndani ya ndoa usiniulize maswali zaidi tumeshaweka makubaliano na kampuni ya sikamanga kijana wao atamuowa binti yangu nimemaliza.."aliongea Mr hance akainuka mezani na kuelekea chumbani kwake.
"Ulaaniwe baba yangu.."enjoy alimlaani baba yake kwa sauti ya juu
"Asante binti yangu mzuri.." alijibu Mr akiwa anapanda ngazi.
"Dada enjoy usiwe mbishi kwa baba yako msikilize tu?.." aliongea dada wa kazi akiwa anatoa vyombo mezani
"Kaa kimya we mbwa fanya kazi zako usinishauli Mimi sawa.." enjoy aliinuka kwa hasira na kuanza kutembea haraka haraka anaelekea chumbani kwake
"Jordani,,, jordan ety aniowe mimi!!!!..." Enjoy aliongea peke yake akiendelea kupanda ngazi kuelekea chumbani, kabla hajafika juu mlango wa chini unafunguliwa sauti ya yule dada wa kazi ikasikika ikimkaribisha mgeni aliyeingia.
"Karibu dada ..." Aliongea yule dada wa kazi
"Asante Mr hance nimemkuta?.."
"We unamuulizia baba yangu wa nini saizi usiku?.."aliingilia enjoy mazungumzo akiwa anarudi chini
"Samahani we ni binti wa mr Hance unaitwa enjoy?.."
"Ndiyo Mimi niambiye shida yako?.."
"Baba yako aliniambia kuhusu wewe woow kumbe ni mrembo!!."
Mr hance alisikia sauti ya yule mgeni akatoka chumbani
"Oooh Suzi umefika... Njoo huku juu.." Mr alikuwa amesimama ngazini nje ya mlango wa chumba chake.
"Nakuja baby mwanao alikuwa ananisumbua hapa..." Suzi alianza kupanda ngazi kuelekea chumba cha Mr hance akitabasam.
"Enjoy usije ukamsumbua Tena huyu binti, nadhani umeshaewa ni nani kwangu na ni nani kwako.."
"Baba jamani huyo dada mbona tupo sawa kabisa kiumri !!.." aliongea enjoy Mr hance hakujibu alipiliza na Suzi chumbani.
"Ee mama yangu pumzika kwa amani haya mambo anayoyafanya baba hapana!!!.."
USIKU KWA SAME
"Zombi nenda ukalale bwana hizo movie zake za kizombi zinanitisha nashindwa kufanya kazi vizuri. utaangalia hata kesho nikiwa sipo.."aliongea same akiwa amekaa meza ya pembeni ya computer akimalizia kazi zake za ofisini.
"Sawa.." zombi alizima tv na kwenda kulala chumba kile kilichokuwa pembeni na sebure.
Baada ya mda mfupi same alisimama pale mezani na kuelekea chumbani kwake kulala akiwa anapiga miayo ya usingizi.
Mida hiyo ya saa nane usiku nyumba ilikuwa kimya wote wakioneka kulala zombi pamoja na same. Lakini chumba cha zombi tunaona mlango unafunguka taratibu alafu tunamuona Zombi anatoka akiwa ameshika kijibegi.
Sijui kile kijibegi kinanini, pia sijui kama nikichaa cha njaa kimempanda au la.
Ila anaelekea mlangoni kwa kunyata sana kusudi same asisikie kelele za kwato. Mwendo huo sasa wa kunyata yani mwendo wa Zombi ulivyo kuwa wa taratibu alafu aongeze na kunyata huo mwendo unaoupata hapo hakika huwezi kusikia kama kuna mtu anatoka.hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa same hakusikia chochote.
MAJIRA HAYO KWA MAMA TONY
mama tony na mmewe wanalala chumba kimoja tony kijana wao analala kivyake.
Chumbani kwa mama tony mda huo amelala usingizi mzito hajielewi kabisa akijua fika yupo na mme pembeni.
Kuna njozi mama tony alikuwa akiiota alishuta haraka njozini na kuanza kuhema kwa nguvu.
Ni dhahiri ilikuwa ni njozi ya kutisha kwake. akachukua grass ya maji aliyoweka pembeni akanywa na kulala Tena.
Alipo pitiwa na usingizi kwa mara nyingine Cha ajabubu ile njozi mbaya aliyokuwa anaota awali ikaendelea palepale.
Alishituka akiwa anahemama juu juu. alishangaa kuona neti imefungwa vizuri juu ikiwa kabla hajalala alishuka neti imekuwa imefungwa tena juu? Alimtazama mmewe labda ndiye amehusika kufunga neti lakini aliona mme anakoroma ndani ya shuka, basi akajua sio mme aliyehusika kwenye neti.
Mama tony hofu ikazidi alipo tazama mlangoni akaona kufuri kubwa lenye alama ya fuvu..
" Hili kufuri limetoka wapi?.." alijiuliza kwa wasiwasi akainuka kitandani kidogo kidogo akawa anaenda ilipokuwa switch awashe taa.
Kabla hajafika taa ilijiwasha bila ya yeye kugusana switch.
Hofu ikazidi kwa mama tony akawa anarudi nyuma taratibu kijasho chembamba kikimtoka paa mala feni ikajiwasha, kumpatia kaubaridi mama tony. Baridi ya feni ni Kama ilizidi kuchochoea joto kwake, yani feni ijiwashe alafu upunge upepo kwa amani alidondokea kitandani kwa kukosa nguvu akiwa anatetema kama
Alianza kutazama kila Kona ya chumba mapigo yake moyo yakigonga kwa kwa kasi kubwa. Akiendelea kushangaa redio yake ikajiwasha na kuanza kudunda nyimbo zisizo eleweka yani zilikuwa ni Kama kelele tu kwenye masikio yake, mwisho kabisa ikapiga nyimbo ya Michael Jackson ya kizombi zombi. baada ya sekunde tano mziki ulizima.
Mama tony uvumilivu kamshinda
"Mme wangu amka naogopa Mimi..." Mama tony machozi yakiwa yamemuanza usoni alimuamsha mme kwa kamtikisa tikisa mwisho akalivuta shuka alilo jifunika mme wake kwa nguvu.
"Ndo Nini Sasa we mama kuamshana kwa kusukumana sukumana hivi?.." aliongea baba tony akiwa anageuza sura kumtazama mkewe. ee bwana hiyo sura ni ya zombi sio baba tony.
"Msaadaaaaaaaa...."
TUTAENDELEA.........
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni