MKUFU WA MALKIA WA GOSHEN SEHEMU YA 1

MKUFU WA MALKIA WA GOSHEN -- 001 *Simulizi za series* Jua lilinyanyuka na kuangaza ardhi ya Goshen: mojawapo ya tawala kubwa iliyopata kutokea mashariki ya mbali katika karne ya kumi baada ya kuzaliwa kwa kristo. Ndege wake wakubwa wenye rangi za kuvutia waliamka wakaruka huku na kule wakitandaza sauti zao nyembamba. Sauti hizo marigoli zikawasili masikioni mwa malkia Sandarus na kumwamsha. Alikuwa amevalia nguo nyepesi za kulalia zilizokuwa zinaangaza kuonyesha mwili wake mchanga wa miaka ishirini na tano. Kichwa chake chenye hekima kilikuwa kimefunikwa na nywele nyingi rangi ya kahawia. Miguu yake mirefu ila yenye nyama ilisimika ardhini na kusimamisha mwili wake mrefu mwembamba. Alah! Alikuwa mzuri haswa. Macho yake yalikuwa makubwa yaliyolegea. Mdomo wake ulikuwa mdogo ila hakika ukichanua kwa tabasamu ungekufanya uache shughuli yako na kumtazama. Nyonga zake zilijiachanua na kukikimbia kiuno. Vidole vyake vilikuwa vyembamba virefu vyenye kucha bawabu. Tumbo lake flati na mapaja me...