BINTI MFALME SEHEMU YA 3
HADITHI- BINTI MFALME
SEHEMU - 3
MTUNZI- LISSA WA MARIAM
"Nitafanya chochote ikiwezekana tutapambana, huyo mtu wanayemtaka wana Bweleo lazima afe, itabidi vijana wangu wasikae bure wawe wanafanya mazoezi kwaajili ya pambano, maana muda wowote naweza kufanya jambo kubwa"
"Vizuri sana mfalme wangu, mimi nakuunga mkono, alafu kwanini usiongeze wanaume mashujaa waweze kufanya? kuna kijana mmoja niliwahi kumshuhudia akipambana, hakika ungemuweka hapa lingekuwa jambo bora, huenda akakusaidia katika mipango yako"
"Asante sana malkia wangu, kama itawezekana niitiwe huyo kijana nimuone niweze kuongea nae" mfalme alisema
*********
Siku ya pili Chansa aliitwa kwa mfalme na kuweza kuongea nae
"Nimepata sifa zako kuwa wewe ni kijana shupavu, nataka nikupatie kazi, ila bado sijaona ushupavu wako, unaweza kunithibitishia?" Mfalme alimuuliza
"Ewe mfalme wangu mtukufu, niambie chochote nitakifanya" Chansa alijibu kwa kujiamini
"Nataka upigane na wapiganaji wangu watatu ukiweza kuwapiga basi nitakupatia kazi katika jumba langu hili"
"Sawa mtukufu mfalme nitafanya hivyo"
Chansa alikubali mfalme alimwambia aondoke na arudi baada ya siku mbili kwaajili ya pambano,
Taarifa zile Legita aliweza kuzipata alimfuata Chansa mpaka anapoishi ili kuweza kuzungumza nae
"Kwanini unaamua kupigana? Huoni kama utahatarisha maisha yako?"
"Hapana hutakiwi kuwa na hofu mimi nitakuwa salama"
"Haiwezekani, mimi sitaki upigane, watu watatu upigane nao alafu unasema utakuwa salama kweli? Najua kwanini baba anaongeza wapiganaji, lengo lake anataka kutawala himaya mbili naona ni hatari, embu kataa kwa niaba yangu Chansa"
"Haitowezekana Legita, tayari ushachelewa nilishamkubalia mfalme nikikataa sasa hivi huenda itakuwa hatari kwangu, pia mimi ni mwanaume siogopi kupigana"
"Kwanini hutaki kunielewa? Hivi ukifa mimi nitaishije? Unataka niishi na maumivu siku zote kwenye moyo wangu? Nakupenda Chansa sipo tayari kuona unaumia, kama utaenda kupigana hakika mimi na wewe itakuwa basi, maana hakuna faida ya kuishi na mtu ambae hakusikilizi" Legita alisema na kuanza kuondoka kwa hasira
"Legita! Legita! Legita" Chansa aliita bila mafanikio
********
Siku ya pambano ilifika, mfalme aliwaalika wanakijiji wa himaya yake wote na kufanya kama sherehe, watu walicheza na kunywa pombe za kienyeji huku wakisubiri wapambanaji waingie ulingoni na kuanza kupambana, siku hiyo Legita alikaa ndani na kijakazi wake mwingine aitwae Nyami, hakutaka kushuhudia kabisa,
Pambano lilianza aliweza kusikia sauti za kelele za watu wakishangilia tu nje, moyo wake ulijawa na wasiwasi mkubwa sana,
"Embu Nyami nenda, naomba ukaangalie pambano" Legita alimwambia kijakazi.
ITAENDELEA..........
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni