MZIMU UMERUDI TENA EPISODE:8
MZIMU UMERUDI TENA
EPISODE:8
MTUNZI:HAMIDU MCHAKO
..............ILIPOISHIA.........................
Niliwastua wenzangu kua turudi kambini kunatatizo limetokea.
Tulianza kurudi ila sikua na hakika kama tutawahi kufika maana yalikua ni masafa marefu hadi kufika
................ENDELEA.................
Safari ya kurudi iliendelea tulizidi kukaza mwendo ila kwa kua sikuile ilikua ni ya mkosi basi hata safariyetu ilikua hivyo hivyo.
Tulipoondoka pale mawindoni tuli muua mtoto wa simba hivyo kulikua na simba mmoja dume alichukia kitendo kile.
Baada ya kuona tunaondoka nae aliunga msafara bila sisi kujua.
Tukiwa bado tuko njiani tukiwa na kasi ya ajabu simba yule dume alianza kutushamburia taratibu.
Mwanzo mimi nilihisi kama vile kunakitu kisichokua cha kawaida kimetokea nyuma ya msafara wetu.
Lakini nilipuuzia na hapo ndipo nilipofanya kosa.
Tukiwa tunaendelea na safari maskio yangu yalicheza yakiashiria kunatatizo limetokea kwenye msafara wetu.Lakini pia nilipuuzia
Akili yangu fikra yangu ilihama na ilikua iko kambini.
Sikuhitaji wazungu wauwawe kwa sababu wao ndio wanadawa ya kuniponyesha na kurudi katika haliyangu ya ubinaadam.
Safari ya kurudi kambini hakika ilikua ni ndefu sana lakini nilisikia mlio kwa mbali wa mwenzetu ambae alikua miongoni mwa kundi letu kamavile kakamatwa na anaomba msaada.
Nilisimama kwa kasi hadi sehem niliyokita mikono ya mbele majani yaling'oka.
Wenzangu nilio ongozana nao waliponiona nimesimama nao wakasimama.
Nilipoangalia tuko wangapi niligundua tumebaki watano badala ya saba.
Nilitoa ishara kua turudini nyuma kunatatizo.
Tulirudi tena kama kilomita nne kutoka pale tuliposimama.
Tulipokaribia eneo la tukio nilihisi hapa hakuna usalama.
Nilitoa ishara tujigawanye na tukavamie kwa pamoja ili tuwaokoe wenzetu.
Tulijigawa na tukawazunguuka wale simba.
Mimi nilokua ndio wa kwanza kujitokeza pale.
Hakika sikuamini kuona kilichotokea na nikajilaumu kwa uzembe wangu wa kupuuzia jambo ambalo lilikua ni lakweli limetokea.
Nilitoa mlio kwa nguvu huku nikijiftua na nikiwasogelea walikua ni simba madume matatu tuna yenyenguvu.
Baada ya mimi kubweka na kukoroma kwa nguvu waliacha kuwashambuli wale wenzetu wawili na wakaanza kunifata mimi.
Niliwatazama kwa makini sana ila hawakufaham kama wamezunguukwa.
Nimi nilirudi nyuma taratibu nikiwalengesha waje sehen nzuri ili tuwashambulie kiulaini.
Wakiwa wananitazama mimi wenzangu walitoka mbio na kila mmoja alimdaka simba wake shingoni.
Wakiwa wanajitahidi kujinasua mimi niling'ata sehem ya koo na nikatoka na nyamaile ya koo.
Nilifanya hivyo
kwa simba wote watatu.
Baada ya kumaliza kaziile ya kuwaua tuliwafata wenzetu hakika walikua na hali mbaya sana.
Tuliwapa moyo na tukawanyanyua pale na tukaanza kuwakokota turudinao kambini.
*************************************
*************************************
Mwendo wa kutoka pale hadi kambini bado ulikua sio mdogo.
Tulizidi kuwakokota lakini ilishindikana na Haliyao ilizidi kuwa mbaya zaidi.
Haliile ilienda hadi wakashindwa kutembea kabisa wakakaa shini.
Hali ya mbwa mwitu ilibadilika wakarudi katika asiriyao ya ubinaadam na wakafariki.
Kitendokile kiliniuma sana kuona nimewapoteza wenzangu wawili tena kizembe na nilijilaumu sana kwa tukio lile.
Niliwaambia wenzangu tufanye mpango tuwahifadhi nduguzetu.
Kwa kua tulikua Mbwa mwitu watu basi pia tuliweza kusimama na hata kutembea kwa kutumia miguu.
Yulisimama kwa miguu miwili wote watano tuliobaki na tukaushika mti nkubwa mmoja tukauvuta hadi tukaung'oa kisha pale tulipoung'oa mti tukawatumbukiza kisha tukawafukia.
**************************************
**************************************
Tulipomaliza kuwafukia Safari ya kurudi kambini iliendelea.
Tuliongeza speed tukawa kama mishale.
Tulipoikaribia kambi hatukusiki milio wala vurugu yeyote yaani kulikua kumetulia kilichokua kinaonekana juu ya kambi ni moshi mnee na mweusi.
Tulipoingia kambini hatukuamini kilichotokea.
Tulikuta lile jengo la kambi linawaka moto. Hapo mimi nilitahamaki sana huku nikibweka.
Nilipoendelea kukagua kulia na kushoto nilikuta maiti nyingi za wale wazungu na wale mbwa mwitu watu waliokua wamebaki pale.
Daah nilichoka sana na hapo ndipo nilipokata tamaa ya kujakua binaadam wa kawaidi kwani waliokua na dawa ya kuja kunibadilisha niwe binaadam wa kawaida wote wamefariki.
Basi niliomba angalau kungekua na mwanajeshi hata mmoja aje anipige risasi na mimi nife maana sikuona umuhimu au thamani ya kuishi katika hali hii na mawazo mengi yalinijia nikisema kama nimeshaipoteza familia yangu kunaumuhimu gani wa kubaki hai katika maisha haya ya upweke.
Nikiwa naendelea kutafakari nilihisi duayangu umejibiwa nilimuona mwanajeshi mmoja akinifata mimi huku kashika bunduki mkononi.
Niliinua kichwa huku nikimtazama vuzuri na nikasema sifanyi chochote bora na mimi nife.
Ila nilikumbuka mafunzo niliyokua nimefundishwa katika uwindaji.
Na ninakumbuka niliambiwa ukiwa kama shujaa ni hakiyako kupambana hadi kufa ila sio kufa kizembe.
Nilikumbuka wenzangu tuliowazika kule hapo ndipo nikawa kichaa nikasema siwezi kufa kizembe nikajiandaa kumsubiri anisogelee Nikiwa namtazama kimakini na yeye alikua anakuja kwa umakini pia.
Aliikoki bunduki yake vizuri na Akaitoa risasi.
Wee niliiona na niliikwepa alihisi mimi ni mzembe ila mimi nilikua shujaa wa ukweli.
Alipoona nimeikataa Akajipanga upya.
Kila nikitazama kulia na kushoto labda nitawaona wale wenzangu wanne waliobakia nikashangaa siwaoni.
Kumbe nao baada ya kufika kambini walipoona kambi imesambaratishwa walianza msako labda kama watawapata watu waliofanya vile.
Wakiwa kwenyemsako wao walisikia ule mlio wa bunduki Ambao risasi yake niliikataa.
**************************************
Tukiwa tunawindana mimi na yule mjeshi ghafla nilisikia kichaka kinatikiswa na wale wenzangu wanne waliobaki wakatokeza.
Ila sikuamini nilichokiona baada ya wale wenzangu kujitokeza.
Kwani walipotoka tu Yule mjeshi Alimtageti mmoja miongoni mwao na Akampa risasi ya kichwa.
Moyo uliniuma na nikabweka kwa sauti kubwa na nikajikuta nimechomoka nilipokua na nikamvaa yule mjeshi nikaanza kumgalagaza nikamchangua kwa hasira nikamtia mkono,mguu,kichwa vyote nilivitenganisha.
**************************************
**************************************
Baada ya kummaliza yule mjeshi nilikua na hasira sana kiasi ambacho machoyangu yalikua yanaona brue brue.
Nikajisogeza pembeni nikakaa kwa muda kama nususaa nikaanza kubadilika na nikaanza kurudi kuwa binaadam.
Na yotehaya yasinge nitokea ila ni baada ya kuambiwa mimi ni mchawi nikafukuzwa kijijini na mwenyekiti.
Wamesababisha niipoteze familia yangu kwani baada ya yaleyote kutokea na kuisha niliamua nitembelee kwenyelile pango sikumkuta mkewangu wala mwanangu nilichokuta pale ni mifupa mifupa na hapo ndipo nilipoamini kua mke na mwanangu wamefariki.
Sikuuona umuhimu wa kutafuta dawa ya kujibadirisha niwe mwanaadam wa kawaida japokua niliambiwa iko ulaya.
Nilifikiri Nikatafute dawa ya kua binaadam Lakini kutakua na raha gani mimi kua binaadam nikiwa nimeshaipoteza familia yangu.Na nikishakua binaadam sitoweza kulipa kisasi.
Nimiaka ishirini hadi sasa imepita na lau angekuwepo mwanangu hadi sasa angekua na miaka 21.
Niliwamisi sana na kutokana na hili ni lazima nitaenda kule kijijini kwenda kulipa kisasi kwa yule Alie nisababishia haya na mwenyekiti pamoja na wanakijiji kwa ujumla.Na nilazima nilazima nilazima nikalipe kisasi.
**************************************
**************************************
Mzee alipofika hapo Alisema kwa msisitizo kua ni lazima akalipe kisasi kisha akasema....
Kijana hayo ndio yalio nikuta hivyo ukiwa kama mwanaadam yatakukuta mengi tu
Nilijikuta chozi linanitoka kwa ajili ya kumuonea huruma yule mzee.
Moyo ukaanza kwenda mbio macho yakaanza kuona tofauti nilikua naona bruu bruu
Kucha zikaanza kunitoka nikawa sijielewi.
Nikanyanyuka pale nikakimbia kuelekea ndani kabisa mstuni.
Nilijihisi maumivu mwili mzima.Ngozi yangu ya mgongoni hadi tumboni nilihisi kama kunavitu vinataka vichomoke.
Pua yangu ikaongezeka urefu hapo ndipo nilipogundua kua ninabadilia na kuanza kua mbwa mwitu.
**************************************
**************************************
Maumivu yalianza kukonga kila sehem ya mwili manyoya madigo madogo yalianza kutoka.
Nikawa nalia huku naita Mama! Mama! Mama! Mama!!!!!!!!!!
Kwani neno mama nililizoea sana tangu napata akili nilimjua mama na sikuwahi kuita baba kwa sababu mama alibiambia baba Amefariki.
Nikiwa naendelea kuita Mama.
Niliona kichaka kinatikiswa kabla sikukaa sawa walitokea wale mbwa mwitu watu watatu.
Hawa kunifaham na wala hawakufahamishwa juu ya ujio wangu.
Waliponiona wakaanza kubweka kwa sauti kubwa huku wakinisogelea mimi,Hapo ndipo nilipojiona mimi kilasiku ni wamatatizo.
Kwakua na mimi nilishaanza kubadilika kuwa mbwa mwitu sikua muoga niliendelea kuugulia maumivu ninayoyasikia.
Dakika chache mbele nilijikuta nimepigwa kikumbo cha ajabu kilichonipeleka hadi chini.
Nibora ukumbwe na semi kuliko kikumbokile.
Nikiwa nagalagala pembeni kwa maumivu ya aina mbili.moja kwa kubadilika kua mbwa mwitu na mbili kile kikumbo nilichokumbwa.
Walinisogelea wale mbwa mwitu watu wakanitazama kwa umakini kisha wakaniuliza.
Waliongea sauti ya kawaida lakini ilikua na mkwaruzo na besi kama mazimwi.
Wewe ni nani mbona kama unafanana na sisi?
Sikuwajibu chochote bali nilibaki kusema tu mama! Mama! Mama! kwani fikrazangu na mawazoyangu yote yalikua kwa mamayangu mlezi na sijui ni lini nitaonana nae maana kilasiku mambo yanazidi kuwa magumu.
**************************************
Wakiwa bado wanaendelea kunidadisi mimi ni nani?
Niliona upande wa pili wa kichaka unatikiswa wote wakakaa makini kuangalia ni kitugani.
Lakini alitokea yule mzee alienisaidia na kunishika mkono huku akiniuliza uko salama?
Nilishindwa kumjibu nilibaki kimya.
Hali iliendelea kua ngumu kila baada ya muda ulivyokua unasonga.
Masikio yakawa yanasikia kama mingurumo ya upepo ila niliwasikia kwa mbali wakiulizana.
Wale mbwa mwitu watu watatu walimuuliza yule mzee huyu ni nani mbona umekuja na kumshika mkono kama mnajuana?
Yule mzee alianza kueleza kile kisa chote kilichotokea hadi kunisaidia na mwisho akasema keshakua miongoni mwa asiri yetu.
Hali ya maumivu ilianza kupungua nikahisi uchovu wa hali ya juu viungo vililegea kanavile nimepigwa na virungu kwenye jointi na ufaham wa kibinaadam ulianza kunijia ile hali ikapotea macho kucha na manyoya yalitoeka.
Nikakurupuka haraka na neno nililoanza kusema ni mamaaaa mama mama.
Wakaniuliza ni kwanini unaita tu mama mama
Nikawajibu ninamiaka miwili sijaonana na mamaangu.
Na hii safari nilikua naenda kwa mamaangu sasa napata shida kiasihiki na sijui lini nitafika kwa mamaangu.
Wakaniuliza ulikua unaenda kijiji gani?
Niliwajibu KWEDIZINGA Ndiko aliko mamaangu
Yule mzee hakujua kua kijiji alichosema ni lazima alipe kisasi ni hicho kwani mwanzo kilikua kinaitwa KWARE na sasa kinaitwa kwedizinga na laiti kisingebadilishwa jina basi tungefahamiana.
Yule mzee alinisogelea na Akaanza kunipa moyo nyamaza kijana utafika tu kwenu usiwe na wasiwasi.
Hakika sijapata kuona mzee aliekua akinibembeleza na kunipa moyo kama yeye na sikujua ni kwa nini ananifanyia vile. Ila Amakweli Dam ni nzito kuliko maji
Baada ya kunibembeleza nilitulia na akili zikarudi zikawa sawa.
Tukaondoka pale tukaelekea kwenyepangolake alilokua akiishi na ndiopale aliponipa msaada.
Niliendelea kuishi na yule mzee Huku akiniambia.
Kijijini kwa wazaziwako utaenda ila hadi ufike mwezi kumi na tano.
Pale mwezi utakapokua mkubwa itabidi mida ya saa sita usiku utoke nnje ya pango uuangalie ule mwezi haliyako itabadilika utakua nusu ni mtu na nusu ni mbwa mwitu na hapo utafungua mdomo.
Kitatoka kitu cheupe na brue mwezini na kitakuja mdomoni kitaingia na wewe utakimeza.
Hiyo inaitwa YUIJA Ukiila hiyo utaweza kujikontrol na utakua na nguvu za ajabu hutopigwa pushi ukadondoka bali wewe utakua ni mwenye nguvu na mwenye hisia ya kitu kitakachokuja au kutokea.
Nilimjibu yule mzee sawa hakuna tatizo.
Nilikaa pale kwa siku kama 10 na ulipofika mwezi kumi na tano saa sita usiku nilitoka nikafanye kama nilivyo Ambiwa.
Nilitoka nnje nikakaza macho kuutaza ule mwezi.
macho yalianza kutoa machozi na yakaanza kuona brue brue.
Meno yalianza kua marefu na zikafuatia kucha.
Ngozi ilianza kuwasha kisha yakajitokeza manyoya.
Kdri nilivyoendelea kuutazama maumivu nayo yalizidi kushamili mwilini.
kichwa kilianza kugonga kengele za ajabu nisizo zifaham.
Nilianza kuona juu ya mwezi kamavile kunakitu kinashuka.
Niliutanua mdomowangu kwa ajili ya kukipokea.
Hakika kilikua na mwanga mkali eneilote lilikua jeupeee hata ukidondosha sindano unaouwezo wa kuiokota.
Kilikuja mdomoni kikaingia nikakimeza na baada ya kukimeza maumivu yote yalipotea na nikawa ninanguvu ya ajabu.
Nikiwa bado ninashangaa shangaa ghafla alitokea mnyama wa ajabu ambae sikuweza kumfaham kwa mapema.
Na kwa jinsi nilivyokua na nguvu nilianza kumkimbiza yule mnyama bila kujua niendako sio sehem salama.........
.................ITAENDELEA..................
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni