DEAR EX SEHEMU YA 4



STORY DEAR EX

MTUNZI : MADAM YUSTAR

SEHEMU YA NNE

Tuendeleee....

Doreen alishtuka saana baada ya kuona Peter ndo Mc, alimuomba Mwenyezi Mungu apuepushie na chochote kile alichokipanga Peter.

Heka heka za sherehe zilianza, kila mmoja alikuwa na furaha lakini Doreen uso wake ulijawa na tabasamu lenye uchungu ndani yake. Hakujua kwanini Peter anafanya hayo yote.

Utambulisho ulikamilika , watu walikula na kukata keki. Hatimae maharusi walipewa zawadi za kutosha.

John mda wote alitabasamu kwa furaha huku akimwangalia mke wake.

Wakati shamra shamra zinaendelea, MC alitangaza kupokea zawadi ambayo iliitajika kusomwa pale mbele, bila kipingamizo John aliruhusu ujumbe usomwe.

Ujumbe uliandikwa hivi;

"Naelewa nipo mbali na wewe, umbali wangu mimi na wewe umekufanya ukaolewa bila kujali hisia zangu. Doreen nimekuwa nikikukumbuka sana hasa nyakati za huzume. Nakumbuka ulikuwa mwanamke unayebeba matatizo yangu kama yako. Huenda nisiwe na zawadi yoyote kwako lakini nakiri kutoka moyoni, hongera saama, ndoa yako ikawe yenye baraka zaidi kila la kheri mamii..."

Ulikuwa ujumbe mfupi ila uliorarua na kuchana chana moyo wa Doreen machozi yalianza kumtiririka kafla. Haelewi alichofanya kakosea au yupo sahihi.

John taratibu alichukua leso na kuweza kumfura nayo mke wake huku akimwambia.

"Naelewa kiasi gani huyo ex wako anavyoteseka, ni wakati wangu wa kuweza kuringa na mwanamke wangu , hayo maneno yake yasikurudishe nyuma au kukuumiza nakupenda leo, kesho na hata milele. Asante kwa kuwa mwanamke wa ndoto zangu."

"Aaah... John acha kuongea sana nimekuelewa vizuri sana, lakini sipo tayari kukuumiza kwa namna yoyote ile hivyo tambua hata mimi nakupenda sana"

Wawili haw walikumbatiana kwa furaha huku watu wakipiga makofi kuwapongeza.

Baada ya mambo yote kuisha John na mke wake Doreen walipewa hoteli ya kwenda kupumzika kwa siku chache. Hivyo walipanda gari na kwenda kumpumzika kwenye hoteli ambayo iliandaliwa.

Mume wa Doreen alimshika mkono mke wake hadi chumbani alikuwa mtu mwenye furaha sana, alianza kumvua nguo mke wake taratibu.

Baada ya hapo walienda bafuni kupunguza uchovu,  mda wote Doreen badoo alionekana hayupo sawa kabsa. Hata mume wake aliweza kulitambua hilo hivyo baada ya kumaliza kuoga alimuomba mke wake wapumzike hakutaka kabsa kumchosha mke wake.

Doreen alishukuru sana,  alimkumbatia mume wake huku akimuaga kwa maneno matamu ya kumsindikiza usingizini.

         ******

Alfajiri na mapema Doreen aliamshwa na mlio wa simu,  alinyanyuka na kuweza kwenda kuangalia,  aliona ujumbe umeingia kwenye simu yake 

"Naamini,  umeamka salama mama... Naamini unafurahia maisha yako mapya ya ndoa,  hongera kwa kupata mume bora,  hongera kwa kuingia kwenye ndoa... Neno pekee ninaloweza kusema. Asante kwa kuweza kuwa mmoja ya wana familia wangu. Nikutakie kila la kheri,  tambua moyoni mwangu una nafasi kubwa sana"

Doreen alichukizwa sana na kitendo cha Peter kuendelea kumfatilia kwa hasira alitoa laini ,  aliitafua huku akirusha simu yake ukutani... Kitendo kile kilimfanya mume wake ashtuke usingizini......

Je! Nini kitafata ? Kaa hapa hapa


ITAENDELEA.........


TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21