Machapisho

BEYOND LOVE ( ZAIDI YA MAPENZI) SEHEMU YA 8

Picha
SIMULIZI: BEYOND LOVE ( ZAIDI YA MAPENZI) SEHEMU YA 8  ndani ya gari kwenda hospitali ya Ocean Road, Tom akiwa ameacha maagizo kwa wauguzi kwamba ikitokea Mariam akaonekana na kuulizia basi aelekezwe mahali walikokuwa, wauguzi wakaahidi kumsaidia kufanya hivyo. Safari ya hospitali ya Ocean Road ikaanza, siku zote Tom alipita nje ya hospitali hiyo akielekea feri lakini hakuwahi kuwaza kwamba siku moja angeingia humo akiuguliwa na baba yake, hakuamini kama Saratani ingeweza kuingia ndani ya familia yake, aliuona ugonjwa wa watu wengine. Matibabu yalianza siku hiyo hiyo kwa njia ya vidonge, mionzi na dawa za sindano ambazo badala ya kuonekana kumsaidia mzee Chacha zilimdhoofisha zaidi, afya yake ikaharibika kabisa na kupoteza uzito mwingi ndani ya muda mfupi! Nywele zote zikanyonyoka kichwani sababu ya ukali wa dawa alizokuwa akipewa. Kila mara Tom alipomwangalia baba yake alishindwa kuvumilia na kutoka nje ambako alibubujikwa na machozi akitamani angalau Mariam angeonekana na kumpa manen...

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 14

Picha
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI. MTUNZI : ALEX KILEO.. SEHEMU YA KUMI NA NNE. ________________ ILIPOISHIA.. ________________ Hiyo siku ya Safari ilipofika ikabidi waondoke pamoja na Omari kama walivyokubaliana. Mzee Mkwiji akawafanyia tambiko dogo kwa ajili ya usalama wao, kisha wakaagana nae kwa ahadi ya kurudi tena baada ya kutoka uko waendako. Wakaenda mpaka mjini, wakaingia kwenye mashine ya kutolea pesa (ATM), wakachukua pesa ya kuwatosha wao, wakatafuta mabasi ya Shinyanga wakapanda, safari ya kuelekea shinyanga ikaanza.. ____________ ENDELEA.. _____________ ...Muda wote safarini Omari aliutumia kujificha na gazeti ambalo alikuwa analisoma, na hata aliposinzia, alilitumia gazeti hilo kujifunika nalo usoni. Shinyanga mjini waliingia saa tano usiku, walipokelewa na mama yake Kayoza, ila aliwashangaa kwa jinsi walivyokuwa na majeraha, "vipi jamani, mbona mna mavidonda hivyo usoni" mama yake Kayoza akauliza. "tulipata ajali mama" Kayoza akajibu kwa kudeka. "na hi...

AKWELINA SEHEMU YA 20-21

Picha
AKWELINA SEHEMU YA 20 Mvua hiyo ilinyesha kwa muda mrefu sana, Yalipofika majira ya asubuhi kakinga alikuwa anatetemeka kutokana baridi kakinga alipomkagua akwelina alimuona anapumua kwa tabu hali iliyompatia Kakinga wasiwasi mkubwa sana kakinga alihisi huenda akwelina anasikia baridi akaenda katika mgahawa akanunua chai ya moto akaweka ndani ya mfuko akamuwekea katika nguo za akwelina ili apate joto, Hali ilizidi kuwa mbaya kwa akwelina ikampelekea akwelina akawa anatetemeka sana , kakinga alipoona hali imezidi kuwa mbaya aliondoka hadi hospital alipofika daktari ampima akagundua mtoto amepata ugonjwa unaotokana na baridi kali : “”” kijana mtoto wako amepatwa na baridi Kali ambayo linaweza kumsababishia kifo kwahiyo inatakiwa ukalipie shilingi laki moja ( Tsh 100000 ) kwa ajili ya matibabu ya mtoto wako sawa kwa sasa nampatia huduma ya kwanza na dawa hizo zitadumu ndani ya siku tatu baada ya hapo anaweza kupoteza maisha hakikisha umelipia. Daktari alipomaliza kumueleza Kakinga alimchu...

MISS TANZANIA SEHEMU YA 23

Picha
MISS TANZANIA SEHEMU YA 23 MTUNZI: PATRICK.CK ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA .Mambo mengi yatajitokeza lakini nitakabiliana nayo” akasema Happy kwa kujiamini “Nitakutana na Mike baadae na nitaitumia nafasi hiyo kumweleza ukweli na nina imani atanielewa na kuniacha huru ili niweze kuwa na mtu ninayempenda kuliko wote katika maisha yangu” Happy akasema na Margreth akamtazama dada yake kwa huruma. ENDELEA…………….. Saa sita za mchana gari ndogo nyeupe yenye namna za ubalozi wa Marekani ilisimama mbele ya nyumba ya akina Happy na kijana mmoja mtanashati aliyevalia suti nzuri nyeusi iliyomkaa vyema akashuka.Alikuwa ni kijana mwenye sura nzuri sana na ambaye ni wazi alikuwa akiwasisimua mabinti kila apitapo.Huyu alikuwa ni Mike mchumba wa Happy.kwa uzuri aliokuwa nao happy alistahili kuwa na kijana kama huyu Margreth ambaye alikuwa amekaa sebuleni akatoka kwa kasi na kwenda kumpokea shemeji yake na kumkaribisha ndani.Mike akasalimiana na familia yote kisha akaletewa kinywaji na kuanza kunywa tara...

Kisinda Akubali Kurudi Yanga

Picha
MZEE wa spidi 120, Tuisila Kisinda ambaye kwa sasa yupo ndani ya RS Berkane amesema kuwa anaweza kuja kucheza Tanzania tena ikiwa Yanga watahitaji huduma yake.   Kisinda alikuwa anacheza Yanga alijiunga na RS Berkane mwanzoni mwa msimu huu wa 2021/22 na jana alikuwa katika kikosi cha kwanza kilichoshinda mabao 2-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya makundi ambapo Simba ipo kundi D.   Kisinda amesema:”Naongea tu Yanga ni nyumbani kama bosi ananitaka ninarudi kucheza fresh, tutaongea tu fresh. “Kwenye mpira hapa tunacheza na Tanzania tunaweza kucheza kwenye mpira fresh tu kila kitu kinawezekana,”.

Wimbo wa Taifa Urusi hautapigwa

Picha
Shirikisho la Soka Duniani ( FIFA ) jana lilijibu shinikizo la kimataifa linaloongezeka kuhusiana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine likisema Urusi itacheza mechi zake za nyumbani katika viwanja visivyoegemea upande wowote na vilevile haitoruhusiwa kuimba wimbo wa Taifa au kupeperusha bendera za Urusi kwenye mechi. FIFA imesema kwenye taarifa yake kwamba itaendeleza majadiliano na kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC, shirikisho la soka barani Ulaya UEFA na Mashirika mengine ya michezo ili kuangazia hatua yoyote zaidi ama vikwazo ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kutengwa kwenye michuano hiyo iwapo hali haitaimarika haraka. Tangazo hilo linatolewa wakati mataifa hayo mawili yakiwa yamefuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia mwakani huku Ufaransa na Uingereza, Sweden Jamhuri ya Watu wa Czech zikisema hazitocheza na Urusi.

PENZI LISILO NA MWISHO SEHEMU YA 1

Picha
Simulizi: PENZI LISILO NA MWISHO Mtunzi: NYEMO CHILONGANI SEHEMU YA 1 “Nahitaji kubadilisha tairi, unaweza kunisaidia kaka?” ilisikika sauti ya mwanaume mmoja akimuuliza kijana aliyekuwa amekaa pembeni kwenye tofali. “Hakuna tatizo, kuna hela?” “Kunisaidia tu mpaka hela?” “Ndiyo! Hakuna msaada bila hela, hasa kwa nyie mnaomiliki magari ya kifahari! Yaani Range Rover SUV, thamani zaidi ya shilingi milioni mia moja, ushindwe hata kunitoa buku teni! Acha masihara.” “Basi sawa! Nitakupa! Nisaidie kwanza.” Ukimya ulikuwa umetawala sehemu kubwa ya Posta Feri, watu wachache walikuwa wamesimama pembeni kwa ajili ya kusubiri pantoni waweze kuvuka na kuelekea Kigamboni. Muda ulikuwa umekwenda sana, ilikuwa ni saa sita usiku muda ambao si watu wengi waliokuwa wakivuka eneo hilo kwenda Kigamboni. Gari zuri la thamani, Range Rover SUV nyeusi ilikuwa imesimama pembezoni mwa barabara ya kuingia katika kivuko cha pantoni karibu kabisa na Kituo cha Polisi cha Magogoni. Halikuwa limeegeshwa kwa makusudi...