KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 14
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO..
SEHEMU YA KUMI NA NNE.
________________
ILIPOISHIA..
________________
Hiyo siku ya Safari ilipofika ikabidi
waondoke
pamoja na Omari kama
walivyokubaliana.
Mzee Mkwiji
akawafanyia tambiko dogo kwa ajili
ya usalama wao, kisha
wakaagana nae kwa ahadi ya kurudi
tena baada ya kutoka uko waendako.
Wakaenda mpaka mjini, wakaingia
kwenye mashine ya kutolea pesa
(ATM), wakachukua
pesa ya kuwatosha wao, wakatafuta mabasi ya Shinyanga wakapanda, safari ya kuelekea shinyanga ikaanza..
____________
ENDELEA..
_____________
...Muda wote safarini Omari
aliutumia kujificha na gazeti ambalo
alikuwa analisoma, na hata
aliposinzia, alilitumia gazeti hilo
kujifunika nalo usoni.
Shinyanga
mjini waliingia saa tano usiku,
walipokelewa na mama yake Kayoza,
ila aliwashangaa kwa jinsi
walivyokuwa na majeraha,
"vipi jamani, mbona mna mavidonda hivyo
usoni" mama yake Kayoza akauliza.
"tulipata ajali mama" Kayoza akajibu
kwa kudeka.
"na hii gari, au?" mama
Kayoza akaongeza swali lingine huku kidole chake akikielekeza katika basi walilokuja nalo wakina Kayoza.
"sio hili mama, wakati tunaenda Tanga
ndio tulipata ajali" Kayoza akajibu.
"aah, haya twendeni wanangu"
mama kayoza akaridhika na majibu
ya mwanae.
Wakabeba mizigo yao,
wakaenda kwa dada yake mama
Kayoza kwa kuwa nyumbani kwa mama Kayoza kulikuwa nje ya mji, iliwabidi walale hapo mpaka siku inayofuata ndio waende kwa Mama Kayoza.
**********
Sajenti Minja alishaanza kuiogopa ile kesi, maana tayari alishaona ile kesi ina mambo kama ya kishirikina na ukingatia si polisi wala serikali inayoamini kitu hicho, na swali alilojiuliza ni kwamba, akisema ahache kaifuatilia hiyo kesi, je kwenye ripoti yake ataandika sababu gani iloyopelekea kuacha hiyo kesi?
Kipindi anawaza hayo yote, alikuwa ndani ya gari akirejea ofisini kwao ili akamshawishi tena mkuu wake ili aone kama atamuelewa katika jambo hilo la kuacha kwake kazi.
Alifika na kumkuta mkuu wake akitoka,
"Nina maongezi na wewe mkuu" Sajenti Minja aliongea kikakamavu huku amepiga saluti,
"Ingia kwenye gari twende" Mkuu wake alijibu na Sajenti Minja hakutaka kuu liza wanaenda wapi, cha muhimu alichokiona ni kuongea na mkuu wake tu.
"Nini tatizo?" Mkuu wake alimuuliza wakati akiiondoa gari,
"Kama nilivyokwambia hawali, naomba hii kesi muiamishie kwa mtu mwingine" Sajenti Minja aliongea,
"Sababu ni ipi?" Mkuu wake aliuliza,
"Sababu ni ile ile, nahisi yule sio kiumbe wa kawaida" Sajenti Minja alijibu,
"Je nikikuambia uni letee barua ya kutaka kuacha hii kesi utaandika sababu ni ipi?" Mkuu wake alimuuliza,
"Hicho ndicho kinachonitatiza" Sajenti Minja alijibu,
"Basi nenda katafute jibu, na ukilipata uje na barua yenye maombi yako" Mkuu wake alimwambia wakati akiliegesha gari nje ya mgahawa,
"Dah, mbona ni mtihani" Sajenti Minja aliongea,
"Huo sio mtihani, mtihani ni kushindwa kujielewa wewe kama askari una jukumu gani katika taifa?" Mkuu aliongea huku akiwa ndani ya gari,
"Unamaanisha nini?" Sajenti Minja aliuliza,
"Kama unashindwa kuelewa hata nilichomaanisha, basi napata wasiwasi ku husu hata uwanajeshi wako" Mkuu aliongea huku akitelemka katika gari, Sajenti Minja nae akafuata huku akihisi kudharauliwa kwa ile kauli ya mkuu wa Polisi,
"Lakini mkuu hiyo kauli inahusiana vipi na maongezi yetu?" Sajenti Minja aliuliza kwa upole,
"Nadhani haihusiani, kwa maana uwanajeshi na akili ni vitu tofauti" Mkuu alijibu kwa kejeli huku akikaa juu ya kiti, na Sajenti Minja nae akakaa,
"Tuachane na hayo mkuu, naomba tu unisaidie kunivua ile kesi" Sajenti Minja aliamua kupuuza kauli za mkuu,
"Numeshakwambia nenda kaandike barua na ulete ofisini kwangu, ila iwe na sababu tofauti na hiyo" Mkuu aliongea kisha akaagiza chakula,
"Na wewe kaka nikuletee chakula gani?" Mhudumu wa mgahawa alimuuliza Sajenti Minja aliyekuwa na mawazo,
"Naomba wali, wali nyama. Atalipa bosi hapa" Sajenti Minja aliongea huku akimaanisha kuwa atakayemlipia chakula ni mkuu wa polisi,
"Mimi na wewe biashara imekwisha, nyanyuka uondoke" Mkuu aliongea kwa amri na kwa kuwa uaskari ni utiifu, Sajenti Minja aliinuka kwa unyonge na kutoka zake nje ya mgahawa.
*************
kesho yake hasubui
wakapanda gari ambayo iliwapeleka
katika kijiji anachokaa Mama yake
kayoza, iliwachukua mwendo wa nusu saa na daladala kufika mpaka eneo ambalo alikuwa anaishi Mama Kayoza, wakatelemka na kisha wakatembea mwendo wa dakika kumi mpaka kuifikia nyumba ya mama Kayoza.
"karibuni, hapa ndio
nyumbani" Mama Kayoza aliongea huku akifungua mlango,
"asante mama" wakajibu
kwa pamoja.
Wakavua viatu, kisha
wakapita ndani,
"ehe, za chuo
mwanangu" Mama Kayoza alimuuliza mwanae baada ya kukaa,
"Za uko ni nzuri, sijui za hapa" Kayoza akajibu,
" na huyu ni nani?",
M ama kayoza akamuuliza mwanae
huku akimwangalia Omari.
"huyu ni ndugu yangu mama" Kayoza akajibu
kwa kifupi.
"ndugu yako?, mtoto wa
shangazi zako au?" Mama kayoza
akauliza tena.
"ni rafiki yangu, ila
kwa matatizo yalinitokea, alisimama kama ndugu yangu" Kayoza akamjibu
mama yake.
"Matatizo? matatizo gani
yaliyokukuta uko dodoma?" Mama
kayoza akamtupia swali jingine
mwanae.
"ni makubwa mama, na
huyu mwenzangu hadi polisi aliwekwa kwa ajili yangu" Kayoza
akamrejeshea jibu mama yake, huku
akijilaza juu ya kochi la sofa ambalo
awali alikuwa kalikalia.
"sasa si ungenitaharifu nimwambie mjomba
ako yuko pale ni polisi pia" Mama
kayoza akaongea huku sura yake
ikiwa na huzuni.
"mama bwana, sasa
we si ungenitaharifu kwanza kwamba
una ndugu dodoma" Kayoza alisema
maneno hayo kwa kudeka mbele ya mama yake.
"mimi nina mambo
mengi mwanangu" Mama kayoza akajitetea.
"ulisema ni polisi eeh?,
anaitwa nani?" kayoza akamuuliza
mama yake.
"ndio ni polisi, tena ana
cheo cheo, anaitwa Joel Minja, ila wenzake wamezoea kumuita sajenti Minja" Mama kayoza akajibu.
"mh, Sajenti Minja!!!!?" Omari akajikuta
anauliza bila kutarajia...
******ITAENDELEA******
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni
Chapisha Maoni