AKWELINA SEHEMU YA 20-21
AKWELINA
SEHEMU YA 20
Mvua hiyo ilinyesha kwa muda mrefu sana, Yalipofika majira ya asubuhi kakinga alikuwa anatetemeka kutokana baridi kakinga alipomkagua akwelina alimuona anapumua kwa tabu hali iliyompatia Kakinga wasiwasi mkubwa sana kakinga alihisi huenda akwelina anasikia baridi akaenda katika mgahawa akanunua chai ya moto akaweka ndani ya mfuko akamuwekea katika nguo za akwelina ili apate joto, Hali ilizidi kuwa mbaya kwa akwelina ikampelekea akwelina akawa anatetemeka sana , kakinga alipoona hali imezidi kuwa mbaya aliondoka hadi hospital alipofika daktari ampima akagundua mtoto amepata ugonjwa unaotokana na baridi kali :
“”” kijana mtoto wako amepatwa na baridi Kali ambayo linaweza kumsababishia kifo kwahiyo inatakiwa ukalipie shilingi laki moja ( Tsh 100000 ) kwa ajili ya matibabu ya mtoto wako sawa kwa sasa nampatia huduma ya kwanza na dawa hizo zitadumu ndani ya siku tatu baada ya hapo anaweza kupoteza maisha hakikisha umelipia.
Daktari alipomaliza kumueleza Kakinga alimchukua akwelina akaenda kumpatia huduma ya kwanza .
?? Mungu wangu naitoa wapi hiyo pesa Mimi daah mungu nisaidie nipate kazi yeyote ili niokoe maisha ya akwelina ??
Yalikuwa ni maneno ya kakinga akijiuliza wapi anaweza kupata pesa kwa ajili ya kumtibu akwelina. Kakinga akaingia mtaani kutafuta kazi, kakinga alitafuta kazi ndani ya siku mbili akapata pesa kidogo akanunua mayai akayachemsha akaanza kuuza ili apate pesa kwa haraka. Safari ya Kakinga ilikuwa ngumu kutembeza mayai bila kupumzika wakati kakinga anavuka barabara lilitokea gari likamgonga kidogo kakinga akadondosha mayai yake yote ambayo alikuwa anayategemea kwa kusaidia maisha ya akwelina , Kakinga kwa hasira alisimama akafuata lile gari akafungua mlango akamkuta mwanamke akamshika mkono yule mwanamke alipomtazama kakinga , Kakinga hakuamini macho yake kwamba aliye mbele yake ni monna ..
Monna kakinga aliuachia mkono was Monna kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme kakinga akarudi nyuma hatua chache cha ajabu Monna alipiga magoti mbele ya kakinga Monna alikuwa anashindwa kumtazama kakinga usoni kwa matendo aliyomtendea, Monna akiwa chini amepiga magoti alishindwa kuyamiliki macho yake akayaruhusu machozi yamtawale, Mvua ya machozi ilinyesha kwa muda mrefu sana katika macho ya Monna , kakinga hata hakujali hilo alisogelea mayai yake akayaokota yote akarudi alipokuwa monna kakinga akamrushia Monna yale mayai alafu akamwambia :-
KAKINGA ?? Samahani dada umesababisha niharibu biashara yangu hii naomba pesa yangu ni shilingi elfu kumi na mbili tu ( 12000/= ) naomba hiyo pesa nina mambo mengi ya kufanya .
MONNA ?? Kakinga mume wangu leo hii unaniita mimi dada kweli daaah nimejisikia vibaya sana niangalie vizuri ni Mimi Monna mke wako au umenisahau jamani ?
KAKINGA ?? Dada eee samahani buana naomba pesa yangu unanipotezea muda hapa nani Monna mbele yangu naomba pesa yangu kabla sijakuitia watu kwamba unataka kuniibia mayai yangu .
Monna alitamani kufa akasimama akaingia kwenye gari akachukua pesa nyingi sana akamrushia kakinga, baada ya kuzirusha Monna alisema kwa sauti ya juu akiwa analia kwa uchungu mno :-
?? Chukua kakinga chukua pesa zote hizo kama unapenda pesa chukua hizo na ukitaka zaidi nitakupatia chukuaaaaaaa .
Pesa zile zilikuwa nyingi mno lakini kakinga alichukua elfu ishirini ( 20000/= ) kwakua zilikuwa ni noti za elfu kumi kumi kakinga akachukua chenchi akamrudishia Monna alafu akasema :-
“” Chenchi yako hii hapa Dada na kingine nakushauri pesa zinahitajika kutunzwa sio kutupwa ovyo kama hivi kwa sababu pesa huwa inakimbia na siku ikikukimbia hutaipata tena jaribu kutunza pesa zako sawa kwaheri .
Kakinga alipomaliza kuzungumza maneno hayo aliondoka , Monna hakuchoka alimfuata kakinga nyuma nyuma na gari lake popote alipokwenda siku hiyo kakinga aliunguka sana katika mji huo yalipofika majira ya jioni kakinga alirudi hospital kwa daktari alipofika daktari alimwambia imebaki siku moja kwahiyo kesho anatakiwa akachukue maiti ya mtoto wake kama hatopata hizo pesa , Monna alisubiri kwa muda mrefu alipoona kakinga hatoki nje Monna alishuka kwenye gari akaingia ndani ya hospital hiyo kwa mbali akamuona kakinga anazungumza na daktari mmoja, Kakinga aliposikia maneno hayo alijaribu kumuomba sana daktari huyo lakini haikusaidia kitu .
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
SEHEMU YA 21
Kakinga akatoka nje ya hospital hiyo akiwa amechanganyikiwa sana , baada ya kakinga kutoka Monna alimfuata yule daktari akazungumza nae yule daktari alimueleza Monna mambo yote yanayomsumbua kakinga , Monna akalipa gharama zote za matibabu ya akwelina alafu akamuomba daktari huyo ampeleke sehemu ambayo akwelina yupo. Yule daktari alimpeleka chumba alichokuwepo akwelina Monna alishikwa na huruma sana alipomuona akwelina anaishi kwa kutumia gesi Monna alilia kupita kiasi akamsogelea akwelina akambusu sana akasema :-
“”” Nisamehe mwanangu nakupenda sana leo upo katika hali hii daah nisamehe sana binti yangu “”
Muda ulizidi kwenda Monna alikuwa bado yupo hospital anamsubiri kakinga arudi, Monna alisubiri sana lakini kakinga hakurudi yalipofika majira ya saa mbili usiku Monna aliamua kurudi nyumbani. Safari ilikuwa ndefu sana hatimae Monna alifika nyumbani alipofungua malango alimkuta Patrick kasimama mlangoni Monna alipotaka kumkumbatia Patrick , Patrick alimpiga kibao Monna ……
Safari ilikuwa ndefu sana hatimae Monna alifika nyumbani alipofungua mlango alimkuta Patrick kasimama mlangoni Monna alipotaka kumkumbatia Patrick , Patrick alimpiga kibao Monna alafu Akamshika nywele akazikunja kisha akamuuliza : Ulikuwa wapi mbuzi wewe ?
Patrick akampiga Monna kibao kingine alafu akamsukuma mbali, Kibao alichopigwa Monna kilimpatia maumivu makali sana, Monna hakuamini kama Patrick angeweza kumpiga kibao na kumfanyia unyama huo wakati Monna akiwa katika mshangao mkali damu zilimtoka katika pua yake, Monna akagusa puani akahisi kuna vitu kama maji yanatoka akayatazama vizuri maji hayo akagundua zilikuwa ni damu zinamtoka puani na sio maji .
Patrick hakutosheka akamvuta Monna akamsukuma hadi kwenye kiti akamfuata akampiga sana , Monna alipigwa sana usiku huo kipigo kilivyozidi Monna alipoteza fahamu, Patrick hakujali hilo alimuacha Monna kwenye kiti akaingia chumbani kwake bila kujali wala kumpatia msaada wowote .
Muda ulikwenda, Masaa yakasonga mbele yalizidi Monna bado hali ya Monna ilizidi kuwa mbaya, Patrick alitoka ndani akamkuta Monna bado amelala Patrick akachukua kinywaji chenye kilevi kikali ndani yake ( Pombe ) akanywa chupa tatu akili ilianza kutoka taratibu Patrick akazidisha chupa nyingine , Kinywaji hicho kiliibadirisha akili ya Patrick akaanza kusema hovyo hovyo Patrick akasogea kwenye kiti alipokuwa amelala Monna akamwangalia sana kuanzia kichwa hadi miguu, akarudia tena kumtazama Monna alipofika kwenye mapaja aliona yapo wazi kutokana na kumpiga sana Monna nguo zilipanda juu mapaja yakabaki wazi kutokana na uzuri wa Monna , Patrick alimtamani sana Akaweka chupa la kinywaji pembeni akamvua nguo zote, Patrick akamuingilia Monna bila kujali Monna kapoteza fahamu, Patrick alifanya mapenzi na Monna kwa muda mrefu hadi alipojirishisha akanyanyuka akarudi chumbani kwake akalala .
Yalipofika majira ya saa kumi na moja asubuhi kulikuwa na upepo mkali wenye baridi ndani yake kwakua mlango ulikuwa upo wazi baridi iliingia ndani kwa wingi , baridi ile ilisaidia kurudish a fahamu za Monna , Monna alipopata fahamu alikaa kwenye kiti alihisi kizunguzungu , kichwa kilikuwa kinamuuma sana , Monna alitulia kwa muda kiasi kichwa kilipotulia Monna alist uka baada ya kujiona hanavaa nguo yeyeote ( Utupu ) hali hiyo ilimpatia mashaka sana .
Monna alijisikia tofauti katika sehemu zake za siri alipojichunguza aligundua ameingiliwa kimwili, Monna alilia sana akasimama akaenda ndani akamkuta Patrick amelala akiwa uchi Monna akajua Patrick ndio aliyemfanyia kitendo kile Monna alishikwa na hasira mno akaenda jikoni akachukua kisu akarudi chumbani akamchoma Patrick kisu cha shingo alafu akavaa nguo zake akatoka nje akakimbia.
Yalipofika majira ya asubuhi na mapema Kakinga alienda hospital akiwa amechoka sana alipofika hospital Kakinga alienda katika chumba cha Daktari akamkuta Daktari anajaza karatasi , Daktari alipomuona Kakinga alimkaribisha ndani Kakinga akapiga magoti mbele ya daktari kisha akamwambia :
KAKINGA : Tafadhali Daktari naomba saidia maisha ya mtoto wangu nampenda sana nipo tayari kukutumikia maisha yangu yote nimekosa pesa nisaidie kaka yangu nimetafuta sana pesa lakini nimekosa msaidie mtoto wangu nipo tayari kufanya kazi kwako kwa muda utakao hitaji lakini mwanangu apone nisaidie ndugu yangu tafadhali .
ITAENDELEA........
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni
Chapisha Maoni