(Episode 1) Penzi Zito La Polisi Mpelelezi Na Mwalifu
Mtunzi: EMMANUEL MRISHO
Mwandishi: EMMANUEL MRISHO
WhatsApp:+255686035594
UTANGULIZI: Mapenzi hayana komando,Hata uwe na roho mbaya ya aina gani lazima ushikwe na mapenzi tena hata kuteswa pia. Watu wengi tumekosa tafsiri sahihi ya mapenzi kwa maana mwanaume unaweza kuwa vizuri kwa kipato ukajua kwamba unaweza kumpata umpendaye kwa wakati lakini ukamkosa kabisaaa, Afu unae mpenda ukaangukia kwa masikini asiye na kitu na wewe mwenye pesa ukaachwa Solemba. Leo tunakuja na simulizi yetu ya "PENZI ZITO LA POLISI MPELELEZI NA MWALIFU" stori hii inawahusu watu wa wawili aliongukia kwenye mapenzi makali tena ya kiapo cha kutoka moyoni kwao. Ester ni polisi mpelelezi na john ni mwalifu hatari kutoka genge la kialifu linaloitwa BLOOD SHARED.
MWANZO: Ilisikika Sauti ikisema "kwenye operation hii nawachagua watu wawili Juma na Ester kuelekea mkoani Geita kwenda kupambana na uwalifu maana matukio yamekithiri maeneo yale" ilikuwa sauti ya mkuu wa Upelelezi akitoa maelekezo kwa Ester na Juma. Akaendelea kusema "Nazani mnakumbuka sheria yetu ya upelelezi sitamani kuona mkishindwa kupata taarifa kutoka maeneo yale, tumieni njia yoyote mpaka tuhakikishe tumewapata hao waalifu sawaa!!" Ester na Juma Walitoa sauti ya pamoja kama makamanda "Ndio mkuu"
Basi Ester alienda kujiaanda nyumbani kwake kwa ajili ya safari. Ester alikuwa na mpenzi wake aliitwa Joseph, mpenzi wake huyo alikuwa ni askari magereza huko mkoani mbeya. Hivyo Ester alimpigia simu mpenzi wake na kumueleza kuhusu safari yake ya kuelekea Geita. Hakika Ester na Joseph walikuwa na mapenzi ya dhati sana maana Joseph alisisitiza sana Ester kuwa awe makini sana kwani anapoelekea ni sehemu hatari. jamani mapenzi ni matamu ukipata anayejali Ester alifurahi sana kuona anavyojaliwa na mpenzi wake. Ester alikika akijisemea "ohhhh takupenda daima Joseph wangu takutuzinzia mzigo wako, hahahahaha" akajichekea mwenyewe kwa furaha,japo wao walikuwa wapenzi tu walikuwa bado hawajaoana.
Siku ya safari ikafika Ester na Juma wakawa ndani ya basi kuelekea mkoani Geita. hawakuwa kimya sana walikuwa na stori za hapa na pale, Juma alisikika akisema "Ester Najua wewe ndo operation yako ya kwanza hivyo naomba umakini uwe nao zaidi maana huko tuendapo sio sehemu nzuri" Ester ilikubali kwa kutikisa kichwa chake huku akiendelea kutafuna jojo yake mdomoni.safari ilikuwa ndefu sana kutoka Dar kwenda Geita walipiga stori mpaka wakaa kimya wenyewe Nazani mnafahamu safari zilivyo mwanzoni raha sana ila katikati mmmmmh huwa kuchungu asee uchovu wa kutosha. Eeee waaah Ester ndani ya Geita sasa, walifika Geita kwa mara ya kwanza huku wakiwa na mawazo ya kufanikisha kazi yao.
Je watafanikisha au watashindwa tayari wamefika eneo husika la kazi yao. Ester kwa mara ya kwanza kwenye operation ya kazi na Juma kama mwenyeji wa kazi.
USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA PILI!
LIKE, COMMENT & SHARE
By Emmanuel Mrisho

Maoni
Chapisha Maoni