MCHUNGAJI MCHAWI, EPISODE:08



Story: MCHUNGAJI MCHAWI.
Mtunzi: Nellove
Episode: 08


Ilipoishia...

"Msiwe na shaka, naamini hili kubwa ndilo litammaliza kwelikweli kisha itakuwa rahisi kumpoteza kabisa kwa uchawi wetu sasa"

Endelea...

Mkuu wa wachawi mzee Lunde aliposema hayo, alitulia kidogo na kutazama huku na huku, akiwaacha wenzake katika shauku kubwa ya kufahamu ni wazo gani jipya,,, ni mbinu ipi mpya,,, ni mpango upi huo utakaommaliza kabisa adui yao. Mzee Lunde alitazama kushoto kisha kulia na baada ya hapo aliliweka wazi wazo lake hilo,, aliwaambia kwa ufasaha bila kuficha ficha. Basi baada ya kuambiwa na kulichambua kila mmoja akilini mwake, wazo hilo lilikubalika kwa asilimia mia moja bila kupingwa. Hakika waliamua kumwendea adui yao kibinadamu zaidi,, yaani ni vita vita waliamini Plan A ikifeli basi Plan B ipo kufaulisha.

                   
Ilikuwa siku moja ya Jumamosi, hii haikuwa siku ya huduma lakini mchungaji Joshua alikuwa anatoa huduma mahali fulani baada ya kualikwa kwenda kumponya Mama mmoja aliyekuwa anasumbuliwa na pepo wabaya,,, mchungaji hakutaka kukata tamaa ndio maana alikubali kuitikia wito.  Mahali alipoalikwa hapakuwa karibu sana na Tungi. Kwa kuchunguza muda basi mtu aweza kutumia hata lisaa kutembea hadi kule. 
Njia ya kwenda huko ilikuwa na mapori mengi tu bila kusahau vichaka vilivyojifanyia makazi pembezoni mwa njia.

Alipata kumuhudumia vizuri yule Mama na kufanikiwa kumponya. 
Yapata majira ya saa kumi na moja na dakika zisizopungua kumi hivi jioni, ndipo alipoamua kutoka kule kurudi nyumbani Tungi. Alitembea njiani huku akijisindikiza na nyimbo za kumsifu Mungu kwa makuu anayoendelea kuyatenda na jinsi anavyompigania hata katika aibu mbalimbali ambazo anakumbana nazo. Hakuwa na hofu yoyote, aliendelea kutembea.

Baada ya kutumia dakika kama 20 alifika mahali palipokuwa na vichaka vingi na mapori makubwa. Ilikuwa rahisi kuogopa hasa ukizingatia alikuwa peke yake na muda haukuwa mzuri sana, hata hivyo hakuona sababu ya kufanya hivyo, aliendelea kutembea kwa ujasiri huku anaimba.
Sasa bwana,,, mchungaji alipiga hatua kama tano hivi baada ya hapo alishtuka na kusimama haraka baada ya kuisikia sauti fulani. Alisimama kwa umakini na kuangaza macho huku na huku ndipo alipofanikiwa kutambua mahali sauti inatokea,, Ilikuwa inatokea kichakani.

Hii ilikuwa sauti ya mtu anayelia na mlio wa sauti hii ulidhihirisha kwamba hakuwa mtu mkubwa sana, ni mdogo tu tena wa kike.
"Naomba unisaidie" ilisikika kwa uzuri sauti hii baada ya mchungaji Joshua kusogea karibu zaidi.
Alijikaza na kutupa jicho kwenye kichaka kile,, alishituka sana kumuona binti mdogo akiwa uchi huku mapaja yake yakiwa yamelowa damu.
"Oooh my God!" Alisema kwa mshituko mchungaji. Alimkimbilia na kumfunika kwa sketi yake iliyokuwa pembeni imechanwa.
"Binti nini kimekupata?"
"Kun,,a mtu ameniba..." Aliona aibu kusema lakini mchungaji alishaelewa.

"Pole sana binti, unaitwa nani?"
"Glory,,, Glory Martin"
Basi Mchungaji hakutaka kuuliza maswali mengi baada ya kuona hali ya binti yule inaendelea kuwa mbaya. Alimfunga vizuri kwa sketi ile na kumbeba ili amuwahishe hospitalini.
Alitembea naye haraka haraka lakini hakufika mbali sana alichoka hivyo alihitaji kupumzika kidogo. Alimuweka chini na kupumzika huku akitamani  uwepo wa mtu mwingine kusaidiana naye. Muda nao ulizidi kusonga mbele,, ilikuwa saa kumi na mbili kasoro,, giza lilijiandaa kuchukua nafasi yake.

Akiwa ameinuka ili kuendelea na safari, muda si mrefu alisikia kelele za watu ambao bila shaka hawakuwa wawili wala watatu.
"Oooh! Ahsante Mungu,, hao watanisaidia kumbeba"
Alisema na kushukuru tena. 
Alikaa chini na kuwasubiri maana walikuwa kule alikotokea.
Sio muda wale watu walifika pale
"Jamani ndio huyu" alisema kijana mmoja aliyekuwa ameshika gongo refu,, uso wake ulidhihirisha hasira zilizojaa ndani yake.
"Wewe ndiye unayetembea na wake zetu si ndio!? Tena umeona haitoshi umeamua kumbaka mtoto wangu" aliongea kwa hasira mzee aitwaye Martin. Mchungaji alishituka sana.

"Oooh! hapana mzee wang..." Hata hakumaliza kusema, alipigwa ngumi nzito na hakukaa sawa alipigwa teke na kuanguka chini.
"Unambaka mwanangu wewe!?" Alifoka mzee na kuongeza kipigo.
"Huyu apelekwe mahakamani,, haiwezekani kuendelea kufanya uovu wake. Anatuchukuliaje sisi??? Tumechoka sasa." Watu walipamba moto,, walimbeba msobe msobe kwa lengo la kumpeleka mahakamani. 
Alipelekwa lakini kwa kuwa muda uliisha sana basi aliwekwa chini ya ulinzi wa wananchi wenye hasira kali.

Kesho yake asubuhi na mapema alipelekwa mahakamani wakati yule binti alikuwa hospitalini hajiwezi. 
Kesi iliendeshwa na ushahidi ulionekana sasa atafanya nini mchungaji Joshua,, alijitetea sana lakini wapi.
"Mnatumia kivuli cha uchungaji kufanya maovu ndani ya jamii zetu" yalikuwa maneno ya wapambe wakiongozwa na wazee wachache waliokuwepo eneo hilo.
"Jamani binafsi naomba tusubiri neno kutoka kwa yeye mwenyewe aliyefanyiwa kitendo hicho. Siwezi amini kama mchungaji anaweza kufanya vitu kama hivi" yalikuwa maneno ya Fabiana. Watu wachache waliokuwa upande wa mchungaji Joshua waliunga mkono.

Kesi iliahirishwa akisubiriwa binti Glory apone kwa ajili ya ushahidi wa uhakika zaidi. Zilihitajika siku tatu za matibabu kwa binti huyu ili kupona kabisa. 
Baada ya hapa, kesi ilirudishwa mahakamani na mchungaji alipandishwa kizimbani tena.
Ni tamko la Glory tu ndilo lililokuwa linasubiriwa pengine kumuweka huru ama kumfunga mchungaji. Lakini atafungwaje ikiwa yeye hajahusika?? Ngoja tusonge mbele...
"Binti! tunahitaji ushahidi wa hili suala kutoka kwako mwenyewe kwa maana si mwingine yeyote anayefahamu ukweli wa hili jambo. Ni wewe peke yako ndio unafahamu kila kitu. Sasa je Huyu umuonaye mbele yako unamfahamu?"
"Ndio namfahamu" alijibu japo kwa wasiwasi
"Unamfahamuje na ulimuona wapi?"

Binti aliguna kidogo na kumtazama tena mchungaji. Watu mioyo ilikuwa inawadunda, hawaelewi ni jibu lipi litatoka. Mchungaji hakuwa na wasiwasi wowote ule,,, yeye alikuwa kimya akisubiri jibu la binti lililobeba uhalisia wa jambo.
"Binti tunaomba Jibu lako tafadhali. Ulimuona wapi huyu?" Lilikuwa swali lililoulizwa kwa mara nyingine.

"Huyu nimemuona juzi huko njiani na ndo huyu aliyenibaka" alijibu binti Glory,,, Mzee Martin ambaye ni Baba mzazi wa Glory na wazee wengine wengi waliokuwepo pale walishangilia mno.
Walishangilia hadi watu wengine walipata mshangao mkubwa.

KUNA WAZEE WANASHANGILIA SANA,, WHY?????
        

        ITAENDELEA.....

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWENZAKO

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5