SHAIDA SEHEMU YA 8
SHAIDA: NO 08
"Staki kusikia chochote.... katika nyumba yangu kila mtu anata kufanya kile atakacho why Hakuna sheria"
"Kwahiyo unamsema Kaka yangu?" kidogo Anita alipandisha sauti na tayari uso wake kupokea hasira.
"Hivi wewe unahakili? Nimseme shemeji ili iweje?"
"Yeye si ndo kasema anawatoa out kwahiyo umeona anafanya vitu kinyume na nyumba yako.... OK ntamwambia hautaki kumuona na ataondika"
"Hey Anita unamatatizo gani wewe? "
"Matatizo? Mmmh Eddy umebadirika Sana, halafu toka tuingia ndani ya nyumba hii umebadirika mpaka sikuelewi"
"Tafadhali kalale"
"Siendi kulala na Kama kosa ni ya Shaida ntamfukuza na kaka ataondoka halafu uishi kwa amani"
"Staki ukiwa unaongea na Mimi unipandishie sauti.. I say kaa Kimya"
Muda huo Sharif na Shaida waliingia na kushangaa.
"Eti I say kaa kimya.. Haya huyu hapa mfukuze sasa"
Maneno ya Anita yalimchukiza Sana Eddy kiasi kwamba, akamtwanga kibao jambo ambalo lilimshtua Sharif pamoja na Shaida. Anita baada ya kupigwa, alipata mshtuko ikampelekea kukosa nguvu na kudondoka chini.
"Oh God" aliongea Sharif kwa msshangao.
Harakati za kumuinua alizifanya Eddy na hapo Hali ya Anita ilizidi kuwa mbaya ikabidi kupelekwa hospitali.
"Ilikuwaje shem" aliuliza Sharif baada ya Anita kulazwa.
"Yaani hata sijui nianzie wapi, hofu yangu ilikuwa kwenu ikanibidi kukaa sebuleni ili kuwangoja.... Ukija kuangalia Umy bado mdogo mpaka saa saba mtu hajui yupo wapi ni vigumu kukaa na kutulia so Kaja akaanza kusema..... dah! si unajuwa tena wanawake" aliongea Eddy.
"Yeah nikweli naelewa, na sisi huko tulinogewa ndo maana tumechelewa kurudi"
"Mmenogewa na nini?" aliuliza Eddy kwa mshangao uliojaa wivu ndani yake.
"Aah utaweza" Sharif aliachia tabasamu murua kuashilia Kuna jambo lilifanyika. Upande wa Eddy alinywea na kuishia kumsaidia kutabasamu. Kama Dakika ishirini, Shaida na Husna waliingia.
"Jamani wifi yangu anaendeleaje?" aliuliza Husna kwa hofu huku akiwa amemfikia mgonjwa na kuanza kumgusagusa.
"Mmekuja na Nani?" Eddy alihoji.
"Dereva wangu katuleta"
"Shaida mtoto umemuachia nani?" swali likahamia kwa Shaida.
"Nimemuachia Nyamisi, nimeona nije kuangalia Hali ya mgonjwa"
"Hali ya mgonjwa ni nzuri. Wewe hutakiwi kuwa hapa maana mtoto muda siyo mrefu atalia" aliongea Sharif.
"Nikweli..." Eddy aliongea huku akinyanyuka, kisha akamalizia kusema.
"Shaida twende nje nikakupe maelezo nini umletee mgonjwa"
Shaida hakusita na tayari kutoka wodini. Walipofika nje ya hospitali, Eddy alimshika mkono Shaida na kumsimamisha.
"Nini Eddy" alihoji Shaida kwa hofu.
"Moja, Wewe na Sharif mmefanya nini mpaka mkanogewa mkashindwa kurudi nyumbani? pili mwanangu alikuwa wapi? tatu kwanini nimekukanya usiende ukakataa? nne kwanini nilikataa usiende na mwanangu ukanionesha jeuri" maswali ya Eddy yalimchanganya Shaida, na muda huo dereva wa Husna alikuwa anawatazama kwa mshangao.
"Ona mbona.... "
"Shiii!!!" Eddy alimnyamanzisha na kuendelea kusema.
"Nenda nyumbani ntafuata majibu yangu huko" Eddy aliongea na kuingia hospitalini. Mawazo kichwani kwa Shaida yalijaa ikambidi kupotezea na kumfuata dereva.
Asubuhi saa nne, Anita aliamka na kudai apewe chakula.
"I'm sorry baby" aliongea Eddy.
"Nisamehe darling kiukweli sikutakiwa kukupandishia sauti, ila nilijikuta tu"
"Ondoa Shaka nakupenda Sana"
Kama Dakika mbili aliingia doctor, na muda huo Sharif na Husna walikuwa wamerudi nyumbani.
"Unaendeleaje? " doctor wakike alihoji.
"Naendelea salama" alijibu Anita.
"OK naomba kutoa majibu ya vipimo vyetu... Ni mshtuko wa kawaida, tena hongera wewe ni mjamzito wa Miezi miwili"
Maneno ya doctor yalimfanya Eddy ashangae kwa furaha, vile vile na mkewe Anita.
"I love you my sweet wife" Eddy aliongea huku akiwa amemkumbatia kwa furaha.
"Kwasasa unaweza kuruhusiwa maana naona afya yako siyo mbaya" aliongea doctor na kuwaacha wawili hao wazidi kufurahi.
Upande wa nyumbani Shaida kila Mara maswali ya Eddy yalizunguka kichwani pake mpaka kukosa amani.
Kama Dakika kadhaa, Eddy alifika pamoja na Anita.
"Wow wifi unaendeleaje" alihoji Husna baada ya kumkimbilia Anita .
"Nipo Vizuri" alijibu Anita kinyonge.
"Halafu kaka, usimpige tena wifi yangu" Husna alimwambia Eddy.
"Usijali, mmmmmh Kuna goodnews"
"News gani hiyo? "
"No baby usimwambie" aliongea Anita kwa madeko.
"Sisemi ng'o" aliongea Eddy kiutani na kuelekea juu. Akiwa anapanda ngazi, alikutana na Sharif akiwa anatabasamu Kama vile kuna jambo zuri katoka kuona.
"Bwana shemeji Vipi" Eddy alimsalimia na kumfanya Sharif ashtuke Kama hajamuona vile.
"Oh Shem mmerudi? "
"Yes, naona unafuraha"
"Utamuweza Shaida kwa vituko vyake" aliongea Sharif na kutoka huku akitabasamu.
Eddy alisimama Kama dakika kadhaa huku akijiuliza amfuate Shaida ama afuate kile kilichomfanye apandishe juu.
Muda huo alitokea Nyamisi ambae ni mfanyakazi mpya, huku akiwa amemnyanyuwa Umy.
"Shkamoo kaka" Nyamisi alimtolea salamu na kumtoa Eddy mbali kimawazo.
"Marhaba, mlete mtoto"
Nyamisi alimkabidhisha mtoto kwa Eddy.
"Mama yake yuko wapi? "
"Yupo chumbani kwake"
"Sawa"
Moja kwa moja Eddy alielekea chumbani kwa Shaida. Alipofika hakugonga aliingia moja kwa moja na kumkuta Shaida anapanga nguo za mtoto. kitendo cha Eddy kuingilia bila kubishahodi, kilimashtua Shaida na kugeuka kumtazama. hakuongea chochote zaidi ya kushusha macho chini.
"Swali la tano kwanini Sharif anaingia humu kila ajisikiapo" aliongea Eddy akiwa bado kasimama.
Shaida alitulia bila kujibu chochote. Upole wake na unyenyekevu wake, ulimkumbusha Eddy mbali enzi hizo wanaishi kijijini.
"Jana Hakuna tulichokijanya na Sharif, tulikuwa kuangalia senema na muda huo Umy alikuwa amesinzia. Na kuhusu Sharif kuingia humu namkataza vipi kwa mfano, anaingia Kama jinsi wengine wanavyoingia" Shaida aliongea kwa upole.
"Unataka kusema Hakuna kinachoendelea Kati yako na yeye?"
"Ndio"
"Mbona nimekutana nae anatabasamu, na nilipomuuliza kanijibu wewe ndo chanzo cha yeye kufurahi. It means kuna kitu umemfanyia"
"Eddy sijafanya chochote ukitaka muulize Nyamisi, tulikuwa wote humu ndani"
"Ila unamahusiano na Sharif?"
"Kwanini ulimpiga mkeo? Ulimpiga kisa Mimi?"
"Ulihisi siwezi kumpiga? Kwasababu yeye nani? Mimi staki dharau zenu, Kama mtafanya kile ninachokitaka ntawathamini na kuwaheshimu"
"Usitujumlishe, mkeo ni moja. Mimi na wewe tumeshaachana"
"Talaka iko wapi?"
"Kwani mpaka talaka? Si ulinitelekeza mwenyewe na huyo mtoto wako. Eddy wewe ni mtu mbaya Sana, mwaka mzima hata simu" Shaida aliongea huku akiwa ameanza kulia. Kwa bahati Mbaya Anita aliingia na kushangaa kuwakuta wawili hao. Shaida macho yalimchomoka, haraka kuanza kufuta machozi.
Eddy kwake hakulichukulia tatizo, Bali alimuomba mkewe atoke chumbani.
"Toka kwanza"
"No! baby unamfanya nini mtoto wa watu" aliongea Anita kwa mshangao, ndipo Eddy alimfuata na kumtoa chumbani kisha akabana mlango.
"Siwezi kusema tena unaniletea matatizo nimechoka kuongea neno hili" Shaida aliongea.
"Ipo siku atakujuwa wewe Nani. au ulitaka nimpigie magoti kisa kanikuta hapa?"
"Naomba mwanangu na utoke nje"
"Rudia tena"
"Sijamaanisha kwa ubaya nimeomba"
"OK acha kulia usimlize mtoto" Eddy alimuacha Umy kitandani kisha akaelekea nje.
"Mungu wangu ntamueleza nini Anita" aliongea Shaida baada ya kubaki mwenyewe.
Upande wa Eddy alimkuta mkewe kamsubiri kordo.
"Baby umemfanya nini?" Anita alimhoji baada ya kumkimbilia.
"Kamuulize mwenyewe, kwani kuna tatizo?" Eddy alijibu bila wasiwasi ndipo Anita aliamua kumfuata Shaida chumbani kwake, alipofika aliingia moja kwa moja na kumshtua Shaida ambae macho ya aibu yalimtoka.
"I'm sorry mpenzi" aliongea Anita baada ya kukaa karibu yake.
"Eddy amekufanya nini?" Anita alihoji.
"Hapana Anita usijali"
"Naomba nijibu nini kinaendelea?"
"Hakuna kinachoendelea sema.... "
"Niambie usihofu"
"Eddy ananichukia hataki kuniona nikitulia"
"I'm sorry my mambo yataenda sawa ngoja ntaongea nae"
Baada ya wiki moja kupita, Anita alimwita Shaida chumbani kwake kwa ajili ya mazungumzo.
ITAENDELEA...............
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni