ZOMBI WA DAR EPISODE 5
ZOMBI WA DAR
ABELUKA FILM
EPISODE YA 05
TULIISHIA....
"Kijana sisi ni police usije ukaingilia kazi yetu mbwa we. unatufugia viumbe vya ajabu kwenye mjini wetu.." Aliongea Afande daudy sauti nzito, Moja kwa Moja akaenda na wenzako kufungua kile chumba alikuwa zombi.
Afande Anavuta mlango kwa hasira na kutazama ndani, lakini alichokiona mbele yake duuh!!!
ENDELEA....
"Huyu ndo zombi ety ?.." aliuliza Afande daudyTena kwa kutabasam baada ya kumuona kijana mmoja mzuri mbele yake akiwa smart Hana doa hata moja usoni Yani alikuwa mzuri na ngozi yake haikuonekana kuwa Kama ya zombi.Afande daudy alisogea jirani na yule mtu aliyemuona ndani ya kile chumba. Akacheka kidogo alipo mkaribia
"Vipi afande mbona mnaingia chumbani kwangu kwa fujo hivi shida Nini?..." Aliuliza yule mtu aliyeonekana ndani ya kile chumba.
"Hapa police tunachezewa kijinga ngoja.
We mamaaaa...." Afande alimwita mama tony ambaye alipiga Simu police. Mama tony alifika pale haraka.
"Ndiyo afande..."
"Huyu ndo zombi uliye tuambia?.." Afande alimuuliza mama tony kwa ukali kidogo
"Ndio Afande Ni kama huyu lakini hakuwa hivi mwanzo! Kama hutojali Naombeni akaguliwe vizuri.." Aliomba mama tony kwa heshima Sana.Afande akamtazama mama tony kwa jicho kali, mwishoni akafyonya alafu akamshika kifuani yule mtu anayedaiwa kuwa zombi.
Baada ya kumgusa alisikilizia mapigo yake ya Moyo Kama yanadunda maana alijua fika kuwa hakuna mtu zombi ambaye moyo wake unaishi
"We mama siku nyingine uwe unatoa taarifa za maana sio kukurupuka tu jeshi la police sio genge la nyanya sawa.huyu mtu ni binadamu kabisa.."
"Samahani afande..."
"Aya toka hapa mshirikina wewe.." mama tony alitoka haraka haraka na kwenda nje.
"Tunaomba radhi kwa usumbufu olio jitokeza, tulionyeshwa video za zombi tukaamini kweli huyu jamaa atakuwa ni mtu mbaya ila tume jihakikishia wenyewe, muwe na siku njema..."
"Ila mnatakiwa kunilipa kwa usumbufu ulioleta nyumbani kwangu!.." aliongea same lakini afande daudy na wenzake hawakujibu chochote, hao wakatoka nje na kuondoka.
Same akamfuata yule mtu haraka
"Oya Rama umeingia saa ngapi ndani?.."aliuliza same kwa furaha kidogo. Kumbe yule mtu aliye onekana na police ndani ya chumba alikuwa ni rafiki wa same mwanzo alikuwa chuoni saizi amerudi likizo fupi anaitwa Rama. Rama anakaa mbeya ila kuepusha gharama huwa anabaku likizo kwa rafiki yake same.
"Aaah mwanangu nimefika hapa nimekuta haupo mlango wenyewe upo wazi nikaona nipumzike magetoni sasa bwana sindoikaingia mtu imechafuka kishenzi Kama zombi alafu nikasikia police wamekinukisha hapo nje aah nikajikaza kiume huyo mchawi wako nikamuingiza chini ya kitandani..."
"Duuh mwanangu umenisaidia pakubwa mnoo maana leo nilikuwa naisha..."
"Inamaana mwanangu kweli unaishi na huyu mchawi?.."aliuliza Rama alafu akatulia kwa makini kusikilizia jibu la same.
"Yeah ni Kama ndugu yangu sioni ubaya wowote kwa sababu sio mbaya kiivyo sema tu Ni zombi..." Same alimjibu Rama alafu akainama kidogo kuchungulia chini ya kitandani.
"Oy zombi toka huko chini police wamesha ondoka.." baada ya same kuongea zombi aliaanza kujivuta taratibu kutoka chini ya uvungu.
"Same ee ngoja mi niende.." aliongea Rama akiwa anachukua begi lake dogo la nguo.
"Sasa unaenda wapi mwanangu likizo hii situna kaaga pamoja?.."
"Bora niende tandika kwa mamdogo hapa baki mwenyewe bro .."aliongea Rama akiwa anafungua mlango wa kile chumba mkononi akiwa na bagi lake.
"Fresh tu man nenda ila naomba usije ukatoa Siri hii kwa mtu yoyote au vipi?.."
"Powapowa mshikakaji hatojua mtu.."
"Nakuaminia..."same alimjibu Rama kwa sauti ya juu kidogo alafu akageuka nyuma alipo zombi.
"Zombi vipi mbona unajitazama kwenye kioo.."
Aliongea same mda huo zombi akiwa anataza sura yake katika kioo. Zombi akiwa anaendelea kujitazama pale mala Kuna kumbukumbu zinamuingia kwa mfumo wa kelele kwenye ubongo wake
"Kakaaaa, kakaaa, nisaidie nakufa mimi.." hiyo ilikuwa ni sauti ya kike iliyomjia zombi kichwani na kumfanya ajisikie kizunguzungu na kuanza kuunguruma akionesha kupatwa na maumivu ya kichwa.
"Zombi unashida gani?.." same haraka alienda kumdaka zombi maana ilibaki kidogo aanguke.zombi alizimia mikononi kwa same.
NYUMBANI KWA KINA ENJOY
Enjoy ambaye ni mpenzi wake na same alikuwa anaishi katika jumba Moja kubwa sana yeye na baba yake Mr hance. Mama yake enjoy alifariki miezi mitano iliyopita.
Mr hance ni mfanya biashara mkubwa East Africa pia ni muajiri wa same Yani same anafanya kazi kwenye kampuni ya Mr hance.
Majira haya Hapo sebuleni kwa Mr hance ugomvi unaendelea Kati ya baba na mtoto
"Kwani baba Kuna shida gani Mimi kuwa na mwanaume ninaye mtaka wewe inakuuma nini haswa?.."aliuliza enjoy akionekana kuwa na hasira.
"Mimi nimeshasema nisikuone tena unatoka na yule kijana lasivyo nitamtimua kazini sawa.." aliongea Mr hance kwa kufoka.
"Lakini baba na Mimi na haki zangu mama angekuwa hai asingenifanyia hivi, mi nampenda same..."
" nimekupa nafasi ya juu kwenye kampuni yule kijana atabaki kuwa mfanyakazi wa kawaida kwako nikija kuwaona mnaleta mapenzi yenu ya kijinga namuuwa si unanijua vizuri we mtoto?.."
"Sawa nitamuacha..." Alijibu enjoy machozi yakiwa yanashuka kwenye macho yake huyo akaenda zake chumbani.
KESHO YAKE ASUBUHI
jana zombi tulimuona akiwa kwenye Hali ya maumivu baada ya kujiangalia kwenye kioo. Tena Kuna kelele za mwanamke alikuwa anasikia zikimwita
"kaka, kaka, kaka.. nisaidieeeeee..."
Baada ya pale alipoteza fahamu.
Leo majira ya asubuhi tunamuona kitandani,
"Zombi amka.."same alimuamsha zombi akiwa anaendelea kufunga vigungo vya shati lake la suti akijiandaa kwenda kazini.
"Zombi amka Basi nikupemaelekezo..."
aliongea tena same akamfuata zombi na kumgeuza, zombi anafumbua macho na kumtazama same kwa jicho la usingizini.
"Jana kabla sijapoteza fahamu nilisikia kelele za mwanamke zikiniita kaka! inamaana kabla sijafa nilikuwa na mdogo wangu?. "
Zombi alijiuliza kimoyo moyo baada ya kufumbua macho majira hayo ya asubuhi
"Mshikaji mi naenda kazini,make sure unaoga alafu kitu kingine usije ukatoka nje tena kusababisha balaa, ukisikia njaa uende kwenye jokofu nimeweka nyama mbichi unazo pendaga.." aliongea same akiwa anamalizia kuvaa viatu mda huo zombi anasilizia akiwa amelala.
"Okay zombi fanya Kama nilivyo kwambiya mi naenda..." Aliongea same akiwa anatoka nje ya chumba cha zombi alafu akanyoosha mikono kuonyesha kuaga.
"Jamaa ananidhami Sana..."
NDANI YA KAMPUNI
ni katika kampuni kubwa inayo milikiwa na Mr hance, majira hayo ya asubuhi Kila mfanya kazi alikuwa anawasili kazini akiwa na gari lake, miongoni mwa watu wanaofika mida hii ya saa mbili alikuwa same.
Aliweka packing gari yake na kushuka.
"Woow same mambo?.." aliuliza dada mmoja mrembo aitwaye ( Linah ) aliyekuwa miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni ya Mr hance na yeye alikuwa anatoka ndani ya gari lake.
"Aah Linah fresh tu za siku?.." same alijibu salamu akiwa anafunga mlango wa gari.
"Tukikumic siku mbili tatu hizi..tuliambiwa ulienda kijijini kwenu..." Aliongea Linah akiwa ame siamama anamsubiri same waongozane kuingia ofisini.
" Yeah nilienda kumcheki mother kidogo ila Kama kawa nisharudi.." same na Linah walinza kuekea ndani ya kampuni pamoja.
Linah alikuwa cheo kikubwa kwenye kampuni zaidi ya same licha ya kwamba same alikuwa anaelimu ya juu zaidi kushinda linah.
Kabla hawajaingia ndani ya kampuni kuna sauti ya gari lilisikika nyuma yao Kama likisimama.
Same aligeuka nyuma kutazama na kuona gari la enjoy
"Poa Linah we tangulia ngoja niongee na enjoy hapa..." Aliongea same Linah akaingia ndani same akabaki mlangoni kumsubiri enjoy.
Enjoy alishuka ndani ya gari na kuanza kuelekea mlangoni aliposimama same. Kitu Cha ajabu alimpita same bila hata ya salamu.
"Enjoy umekuwaje mbona sikuelewi?.." aliuliza same kwa jazba akiwa ana fuata enjoy kwa nyuma lakini enjoy hakujibu chochote alielekea mpaka ofisini kwake.
Same hakuwa na namna alikausha na akiwa amesimama nje ya ofisi ya enjoy
" We same nenda kaendelee na kazi zako usije ukajaribu kuingia ufisini kwa enjoy siunamjua bosi..." Aliongea secretary akiwa anaendelea kufanya shughulikia zake.
Ok nimekuelewa..."
Same aliondoka pale na kwenda kukaa kwenye meza yake ndani ya sehemu hiyo kubwa ambayo ilikuwa inawafanyakazi wengi haswahaswa mabinti wa kike.
"Handsome wetu amsrudi kazini.." walikuwa wanaongea baadhi ya mabinti wakitabasam kumuona same tena.
"Acheni ujinga nyie fanyeni kazi mnaongelea wanaume kazini pumbavu nyie jiangalieni lasivyo..."aliingilia jamaa mmoja wa kiume aliyeitwa sadiki. mda huo same alikuwa anaendelea na kazi zake japo kwa mawazo.
"We Sadiki unataka tukuongelee wewe na sura läko hilo mbaya hahahah.." aliongea linah wadada wote mle wakacheka.
Mala mlango ukafunguliwa wote wakaa kimya baada kumuona Mr hance anaingia akiwa na wageni wawili wakubwa Sana kutoka serikalini
"Nilisikia kelele humu?.." aliuliza Mr hance akiwa amesimama na wageni wake mbele
"Hapana bosi?.." alijibu Linah kwa woga kidogo.
"Okay endeleeni na kazi..."
Mr hance aliingia kwenye lift akiwa na wageni wake na kuelekea ofisi ya juu ambayo ni ofisi yake kwa ajiri ya kikao binafsi.
MCHANA
NI majira ya mchana ndani ya jiji jua ni kali sana mda huo wafanyakazi walikuwa wanapata chakula ndani ya kampuni Tena juu ya meza zao za kazi wakiendelea kupiga story za mahusiano ya kimapenzi, Kama kawaida linah ndio muongoza mada.
"Mimi siwezi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume ambaye Hawana hela.."
"Hahahahah .."
aliongea linah akiwa Kisha akanywa grass ya maji wanaume wote mle walicheka kasoro same maana alikuwa kwenye strees kidogo sababu enjoy alimkaushia ile asubuhi.
Wakiwa wanaendelea na story mlango wa ofisi ya enjoy ukafunguka. Akatoka enjoy alafu akasimama mbele.
"Aaah dada enjoy huyu jamaa yetu hapa sijui anatatizo gani Leo haongei kabisa.." aliongea sadiki akielekeza kidole kwa same alipomuona enjoy
Enjoy hakuongea chochote alianza kutembea kuelekea mlangoni ili atoke nje.
Kabla hajafika mlangoni mala mlango ukafunguka. Enjoy akasimama haraka na kubaki kinywa wazi.
"Nyie angalie kule mlangoni alipo enjoy.." aliongea binti mmoja wafanyakazi wote wakageuka
Linah tabasam lake lilikata ghafla akiwa anaendelea kutazama mlangoni.yani Kila mtu alibaki kustaajabu.
"Ayaaa huyu jamaa sijui amepajuaje hapa nilimwambia atulie ndani ona Sasa alichofanya!!" Aliongea same bila kusikika.
ITAENDELEA.........
Siri kubwa kuhusu huyo mfanyakazi linah inafichuka sehemu ijayo....Siri gani hiyo? Tukutane sehemu ya 06
🔥
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni