SHAIDA SEHEMU YA 7
SHAIDA: NO 07
Shaida alishindwa kujibu akaamua kuendelea na kazi zake, Eddy haraka alimshika mkono na kuanza kumvuta.
"Eddy Kuna nini mbona sikuelewi? "
Eddy bila kujibu aliendelea kumvuta mpaka sebuleni, Shaida hofu ilimtawala maana kujitoa kwa Eddy ilikuwa ngumu na istoshe alihofia Kama mtu yeyote ataona italeta gumzo ndani ya nyumba. Eddy bila kujali kuonekana ama kutokuonekana, alimtoa nje mpaka akamwingiza ndani ya gari kisha na yeye akaingia.
"Mungu wangu nini kinaendelea kwangu" Shaida aliongea huku akilia.
"Spendi unijibu utakavyo... Mimi ni mume wako" maneno ya Eddy yalimfanya Shaida kupandwa na mzuka.
"Mume? Hivi wewe wakisema wanaume wajipange pale unaweza kwenda kweli"
Eddy kwa hasira alimuwasha kibao na kumtuliza.
"Ongea ujinga wako wote ila usinidharau" aliongea Eddy.
"Eddy umenipiga?" Shaida alimhoji huku akilia.
"Na ntakupiga tena usipotulia"
"Tafadhali, naomba nifungulie mlango ntaondoka humu ndani na mwanangu"
"Lia ukimaliza utaniambia tuendelee kuongea"
"uongee na Nani? Lakini kwanini unaninyanyasa hivi? "
"Sikunyanyasi, tatizo wewe hautaki kunipa nafasi tuongee"
"Nafasi gani? Au unahisi uwepo wangu hapa ni kwa ajili yako? Mimi nilikuja hapa mjini kwa ajili ya kutafuta maisha ya mwanangu na si kukutafuta wewe, na hapa nilikuja kuomba kazi na sikujua kwamba nikwenu. Kama ni kunitelekeza ulinitelekeza, Leo ndo unataka kujifanya kunijali"
"Wewe ni mke wangu haijalishi nini na kukuleta hapa nataka tujadiri kuhusu hili lililotokea"
"Sina muda wa kujadiri chochote na wewe"
"Na vipi kuhusu mwanangu"
"Unajidanganya, Umy siyo mwanao"
"Shaida tafadhali usinichanganye"
"Nakuhakikishia na usinifuatilie"
"Nakupa onyo, nisisikie tena ukiniambia Umy siyo mwanangu"
"Mwanao? Angekuwa mwanao ungemtelekeza? "
"Sikumtelekeza"
"Bali"
"Kuna mambo flani, ndo haya nataka kukwambia"
"Staki kusikia chochote, umenipiga naomba nifungulie mlango niondoke"
"I'm sorry"
"Staki Eddy na naondoka humu ndani"
"I'm sorry"
Muda huo Anita alitoka ndani Akiwa amemnyanyua Umy, kisha akakaa kwenye kiti jambo lililomshtua mno Shaida. Kama Dakika mbili Husna nae alitoka na kukaa karibu na wifi yake.
"Eddy uliyaharibu maisha yangu awali, mpaka sasa hujarizika unataka kuniangamiza kabisa" aliongea Shaida kwa sauti ya chini mno, akihofia asisikike.
"Tulia Hakuna kitakachotokea" aliongea Eddy bila wasi wasi.
"Wakijuwa nipo humu ntaongea nini Mimi"
"Hata wakijuwa, kwani tatizo liko wapi"
Kabla Shaida hajamjibu, simu ya Eddy iliita, alipoangalia mpigaji alipokea maana alikuwa ni mkewe.
"Hi baby" Eddy aliongea na kuangalia upande wa pili aliko mkewe.
"Yes sweetie, I miss you halafu umeondoka bila kunitaarifu"
"Usijali, Nipo hapa karibu yako"
"Uko wapi?"
"Ndani ya Gari"
"Njoo basi tupige story"
"Nakuja" Eddy alikata simu na kumgeukia Shaida ambae muda wote alikuwa amebana pumzi ili asisikike.
"Twende" Eddy aliongea na kumshtua.
"Eddy jamani mbona upo hivo? Ningejuwa nisingemruhusu dada yangu akaniacha"
"OK basi we tulia ntakufuata baadae" Eddy alitoka na kumuacha Shaida ndani ya gari.
Majira ya usiku watu wote wapo ndani, Eddy alimfuata Shaida alipo ndani ya gari na kufungua mlango. Uso wa Eddy ulipokea tabasamu murua baada ya kuona uso wa Shaida ukiwa umetulia kwa kubebwa na usingizi. Taratibu alimshika shavuni, na hapo Shaida alifumbua na kumtazama.
"Mungu wangu mwanangu" Shaida aliongea na kuutoa mkono wa Eddy huku akiomba atoke akamwangalie mwanae.
"Yupo salama na hajalia" aliongea Eddy huku Shaida akiwa kashatoka ndani ya gari, Tayari kuelekea ndani. Alipofika ndani alimkuta Anita bado kamnyanyua Umy, kitendo cha kumjali mwanae kilimfanya asikitike akihisi hamtendei haki kukimbizana na Eddy.
"Dear ulikuwa wapi?" Anita alimhoji.
"Samahani Anita kwa kukuachia mzigo, kiukweli nilotoka...."
Kabla hajamalizia kuongea, alikuja Sharif akiwa amependeza na kumwambia.
"Nimekusubiri kwa muda mrefu, tafadhali naomba kajiandae tutoke out"
Muda huo Eddy alifika na kusikia kila kitu. Macho yake yalitua moja kwa moja kwa Shaida na hapo Shaida nae akamtazama bila kujuwa atafanya nini. Jicho la Eddy lilitoa tafsiri asithubutu kutoka na hapo Shaida akaelewa.
"Ntaendelea kuwa mjinga mpaka lini" Shaida akijisemea moyoni na tayari kupata majibu.
"Sawa Sharif nisubiri" aliongea hivo na kuelekea chumbani kwake kwa ajili ya kujiandaa, Kama dakika kumi alirudi na kumkuta Eddy kasimama pale pale huku akimtazama jicho mbaya.
"Wow you look so beautiful" aliongea Ran licha Shaida hakuelewa alichomaanisha, nakuishia kutabasamu.
"Tunaenda na Umy" aliongea Sharif jambo lililomfanya Eddy apinge.
"Nendeni wenyewe huyu mtoto muacheni"
"Ntaenda na mwanangu" aliongea Shaida.
"Yeah ndo itakuwa couple nzuri" Anita aligongelea msumali huku akimkabidhi mtoto Shaida. Waliondoka na kumuacha Eddy akiwasindikiza kwa macho.
Mpaka majira ya saa Saba walikuwa bado hawajarudi, kitendo kilichomfanya Eddy akose usingi na kwenda sebuleni kucheza game.
"Baby tukalale watakuja" alikuwa ni Anita baada ya kuona mumewe anahofu Sana zidi ya kina Sharif, ilibidi kumfuata sebuleni.
"Tatizo wote humu ndani wabishi, siyo wewe uliomba aletwe mfanyakazi mwingine ili Shaida apate muda wa kumlea mtoto?"
"Ndiyo baby laki..."
ITAENDELEA........
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni