SAA ZA MWISHO EPISODE 4
SAA ZA MWISHO
Ep4****
S.P Owino
Hatimae waliingia kijijini mama pamoja na kaka walipo fika nyumbani kwa Bibi kulikua kimya japo watu walikuwepo wengi, mama alikaribishwa vizuri kabla hajaambiwa Nini kilicho wajaza watu eneo lile ambalo lilionekana Kama kichaka kwani aliishi mamdogo tu!
Huku hospitali ilimbidi dada Helena atoke nje ili niweze kuongea na nesi, nesi aliniuliza Kama ua ninashida yoyote yakiafya Ila nilimwambia shida yakudumu sina! Alikua akinitazama usoni Kama mdadisi!
Ilikua saa11:40 jioni.
Sas ilibidi mama aambiwe kilichotokea aliambiwa kaburi tulilo mzika mama yako limeshuka chini, najua hata mama hakuelewa kwaurahisi mpaka alipo pelekwa akakuta like kilima cha kaburi hakipo! Na walikua wakimsubiri mama ili atoe ruhusa liweze kufululiwa mama akiwa katika mshangao mkubwa aliomba vijana waliokua tayari wamechaguliwa waweze kulifukua lile kaburi!!!
Ilikua saa 12:30 jioni!
Dada aliingia ndani ya kile chumba akiwa na vyakula ili niweze kula kwa jioni ile. Jioni hiyo kulikua na madaktari na wauguzi katika kikao wakijadili kutokana na kilichotokea ikionekana Kama nikitendo cha uzembe!; Kwanini Alie fariki aamke? Labda katik a vipimo vyao hawakua makini!
Kburi lilizidi kufukuliwa jua pia lilikua likizama kwamda ule lakini walifanikiwa kulifikia jeneza lililo onekana kuliwa Sana na mchwa kwani imepita miaka miwili tangu Bibi azikwe! Walishuka vijana wawili ndani ya like shimo ili kufunga kamba vizuri liweze kuvutwa juu lile jeneza! Lilipo fikishwa juu mama aliombwa alifungue chakushangaza ndani zilikuwepo nguo tu alizo zikwa nazo hazijaguswa ata kidogo na mchwa lakini mwili au mifupa haikuonekana!
Ilikua saa 1:00 usiku
Nikiwa nimelala kitandani nilihisi Kuna mtu amekaa pembeni yangu nikijua ni dada Helena, nilipo funua shuka pale kitandani hakuwepo mtu na mlango ulikua wazi pia ilikuwepo baridi Kali mdaule!!
Nilisikia sauti iliyo nong'oneza kwamba nimeanza na wewe Ila kesho anafuata maria! Hilinijina la madogo yule asiye weza kuongea!!Hatimae usiku uliingia huu ulikua usiku wa siku ya pili, ndani ya zile siku nilizo pewa za kuishi na yule nesi Alie nijilia usiku!!
Usiku huo dada Helena aliomba kukaa namimi ndani ya kile chumba cha wagonjwa!!
Ilikua saa 2 usiku.
Kule kijijini wanafamilia walizidi kuingiwa na wasiwasi juu ya kilicho tokea kwani adi mwenyekiti wa eneo lile alikuwepo pale, Wana familia walipendekeza like kaburi lisifunikwe adi mwili upatikane. Jambo ambalo kwa wengine lilionekana Kama ndoto! Ndani ya ilenyumba aliyo kua akiishi mamdogo ambayo mwazo ilikua ya Bibi Kuna chumba kilikuwepo na ilionekana Kama hua hakifanyiwi usafi hata mfumo wa umeme mle ndani haukua sawa Kaka alijikita akisukumwa kuingia mule ndani!! Aliwasha taa yake ya sim, kulikua na utando wa buibui mabegi yaliyo chakaa alianza kupekua lakin hakikuwepo chochote cha maana Ila aliziona picha, na Alie muona pale ni Bibi japo sisi hatukuwai kumuona Bibi yetu kwa sura japo tulizaliwa mpaka tukawa wakubwa adi kifo kinamkuta mama hakutaka tumuone Wala tuwe na ukaribu nae tulipo muuliza sababu hakutuambia, japo tulisha Wai kusikia akwamba Bibi yetu alikua akijishughulisha na mambo ya giza! Ila Kaka aliamua kuitunza picha moja mfukoni kwake
Ilikua saa 4
Dada Helena alipitiwa na usingizi Ila Mimi bado nilikua macho kitandani kwangu!
Mda ulizidi kwenda na ilipo fika saa 6 usiku bado sikua na usingizi kabisa nilihisi nje ya chumba alikuwepo mtu akiongea huku akikaribia kile chumba!!
Ndipo nikajaribu kumuamsha dada Helena Ila hakuonyesha ata dalili yakuamka! Mle ndani kuli jaa Moshi na harufu mbaya Sana ndipo alipo ingia yule nesi akiwa na mavazi yenye vumbi!!
Alinisogelea nikauona uso wake!! Vizuri akaniambia zimebaki siku 3!! Kisha akaondoka, Moshi ulinizidia nilikohoa adi nikipoteza fahamu!!
Ilikua saa1:30 asubuhi
Iliingia siku ya alhamis ambapo kwangu ilikua siku ya tatu ya uhai wangu katika SAA ZANGU ZA MWISHO!!
sim ya dada Helena ilikua ikiita aliamka akaipokea alikua mama!!
ITAENDELEA.........
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni