SHAIDA SEHEMU YA 4



SIMULIZI: SHAIDA

MTUNZI: AISHA KHAN

SEHEMU YA NNE

ILIPOISHIA

Eddy hakusubiri Sana, aliondoka Haraka na kumuacha dada yake akimlalamikia

SONGA NAYO

Baada ya muda, Shaida na dada yake walikuwa nyumbani kwao Manzese huku wakipanga nguo ili kuhamia kwa kina Eddy. Muda wote Shai alikuwa ni mwenye kulia bila kuchoka.

"Aisee ningejuwa kuwa nipo na mtu mzaifu Kama wewe, wallah nisingekubali Kuja huku " Aisha aliongea.

"Usiseme hivo dada"

"Mtu uliekuwa unamtafuta umemuona na tayari umeuona moyo wake ulivyo, nini shida mbona sikuelewi? Au chukuwa nauli rudi kwa baba kisha ntakuwa nikikutumia pesa ndogo ndogo"

"Dada, silii kisa siwezi kufanya kazi, hapana! Nalilia muda Wangu nilioupoteza kumfikiria... Naomba niache nilie nikichoka ntakwambia"

Majira ya jioni walifika kwa boss wao, wakakaribishwa na kupewa chumba cha kulala kimoja kilichomo vitanda viwili.

"Naendelea kusisitiza, jifanye Kama vile hujawahi kumuona kabla. Chochote atakachokifanya na mkewe kipotezee kwasababu wewe siyo chaguo lake.. Sijui umenielewa? " Aisha aliongea Huku akiwa amelala.

"Nimekuelewa dada yangu. Ntajitahidi kadri ya uwezo wangu"

Alfajiri Kama kawaida ya wafanyakazi wa ndani kuamka na kuanza kufanya kazi, Shaida na dada yake walihakikisha kila kitu ndani wamekisafisha mpaka kuandaa chai na kutenga mezani.

"Sasa wewe nenda ukamuamshe boss Mimi niende kwa Eddy " Aisha alifanya hivyo ili kumkwepesha wivu mdogo wake. Baada ya muda wote walijipanga mezani kisha kina Shaida wakaenda jikoni kupata kifungua kinywa.

"Aisha aaaa " ilikuwa ni sauti kutoka kwa boss wa nyumba iliyomfikia Aisha na kusitisha kunywa chai, haraka kuelekea mezani.

"Samahani boss, umeniita? "

"Ndiyo, ninyi mpo wapi"

"Tupo jikoni"

"Mnafanya nini "

"Tunakunywa chai "

"Hapa kwangu kuna utaratibu wake, muda wa kula haijalishi ni asubuhi au usiku wote tunajumuika meza moja"

"Kweli baba nimewaambia wakakataa" aliongea dada yake Eddy na kumfanya Aisha ajibu huku akitabasamu.

"Sisi ni wafanyakazi tu. Haina shida kulia jikoni"

"Nasema Mimi njooni" Mara hii mzee aliamrisha.

Haikuchukuwa muda wote walifika mezani na kukaa huku wakijiogopa.

"Sisi ni familia, kwanini mjitenge wenyewe huko" aliuliza baba yake Eddy.

"Tusamehe boss " alijibu Aisha, kisha wakaendelea kunywa chai huku wakipiga story. Eddy Muda wote alikuwa kimya tofauti na alivyozoweleka nyumbani.

"Baby mbona huongei" Anita alimhoji mumewe na kumfanya apaliwe.

"Sorry jamani" Anita aliongea kimahaba Huku akimnywesha maji Eddy ambae alichukuwa glasi Ile na kunywa mwenyewe. Alipomaliza, alinyanyuka na kuondoka akidai ameshiba.

"Dad simuelewe Eddy kabisa " aliongea Anita kinyonge.

"Usijali ntaongea nae" mzee baada ya kujibu, alinyanyuka na kumfuata Eddy.

"Hivi huyu mtoto wako anaitwa nani" Anita alimhoji Shaida ambae alitabasamu na kumtazama Umy.

"anaitwa Umy"

"Wow come here"

"Nenda kwa shangazi" Shai alimkabidhi Anita ambae alionekana kuvutika Sana na Umy.

"OK unasoma? " Ran alimhoji Umy kiutani licha alijuwa Umy bado mdogo na haelewi chochote.

Muda huo alifika Eddy akiwa amebadiri nguo ishara anaelekea kazini.

"Hey dear unaenda wapi? " Anita alimhoji. Muda huo kwa bahati mbaya Eddy alimtazama Shai na kugonganisha nae macho.

"Naenda job" Eddy alimjibu.

"OK kiss me"

Eddy alishuka na kumkiss mkewe. Alipotaka kuondoka Anita akamwambia.

"Mkiss na mtoto jamani"

Eddy alimtazama Umy ambae kwa muda huo alikuwa anamtazama kwa hofu kutokana alikuwa hajazowea kuwaona. Eddy Kabla hajambusu, uzalendo ulimshinda Shai ikambidi kusimama na kusema kwa kigugumizi.

"A a a a" aliishia hapo huku kifua chake kikipanda na kushuka kutokana na mshtuko wa moyo.

"Usijali mpenzi mwanao nimempenda" Anita aliongea ili kumtuliza Shaida. Ndipo Eddy alimbusu Umy na kujikuta moyo wake umepokea kitu cha tofauti mno.

"OK umletee chocolate mtoto siyo unambusu busu tu" aliongea dada yake na kumfanya Anita agongelee msumali.

"Usije bila chocolate ya mtoto nakwambia"

Baada ya Eddy kuondoka, Anita alianza kumsifia Shaida kuwa anambegu nzuri ya kutoa mtoto Mzuri.

"Not yeye baba wa mtoto ndio fire" dada yake Eddy ambae ni Husna aliongea na kuwafanya wote wacheke kwa pamoja.

"Em mcheki mtoto alivyo mzuri. Yaani na Mimi ntapata mtoto Kama huyu " Anita aliongea na kuendelea kusema.

"Usijali Shaida, muda Ule niliona ulivyoshtuka ila naelewa ni kwasababu Eddy yupo kwenye Hali hii... Hata Umy ameogopa Sana, lakini mtamzowea mume wangu Hana shida, na ni mtu wakutabasamu kila muda"

Shaida na dada yake walitabasamu bila kujibu chochote.

Baada ya masaa kadhaa. Ilikuwa ni usiku ndipo Eddy alirudi nyumbani Akiwa na chocolate alizoagizwa.

Muda huo Anita alikuwa bafuni anaoga, ikambidi kutoka ili kumpokea mumewe.

"Sweet ndio utoke na povu " Eddy aliongea.

"Kwahiyo huwezi kunichumu?"

"OK hii hapa" Eddy alichomoa chocolate na kumuonesha.

"Wow umeleta " Anita aliongea Kwa furaha na kutoka chumbani haraka.

"Shaida....Shaida...." alianza kuita huku Akiwa amesimama karibu na mlango wa chumba chake.

"Abee" ilikuwa ni sauti kutoka kwa Shaida.

"Mlete Umy achukuwe chocolate zake"

Haikuchukuwa muda Shaida alifika huku akiwa amenyanyua Umy.

"Tuingie huku " Ran alimuonesha chumbani na kumfanya Shai ashtuke kwa woga.

"Mchukuwe wende nae " Shai aliongea.

"Nina povu, we njoo tu "

Ilimbidi Shaida kumfuata Anita chumbani huku moyo wake ukiwa hauna amani kabisa. Walipofika, uso kwa uso na Eddy. Hapo ndipo alikosa ujasiri na kushusha macho chini.

"Dear mpe chocolate mtoto, ngoja nitoe povu inaanza kuniwasha" Anita aliongea na kuelekea bafuni haraka, huku akiwa amewaacha watatu hao.

Eddy kuongea alishindwa, vile vile kumpatia chocolate akashindwa. Wakajikuta kila mmoja akipumua kwa kasi kutokana na kusikiliana aibu. Kama Dakika moja Anita alitoka bafuni na kuwashangaa.

"Baby hujampa tu? "

"Hapana nimekusubiri wewe uje umpe" Haraka Eddy alimkabidhi chocolate mkewe, na kutoka chumbani haraka.

"Njoo mpenzi wangu" Anita alimchukuwa Umy na kumuomba Shaida amvumilie kidogo anamleta.

"Haina shida we kaa nae, Kwanza ananisumbua huko"

Shai alimuacha Umy na kutoka chumbani. Alipofika kwenye ngazi ili kushuka chini, alishtuka mno baada ya kumuona Eddy kasimama. Moyo wa ujasiri ulimuingia ikambidi kujikaza na kuanza kushuka kwa kasi. Kabla hajampita Eddy, alishtuka kusikia kashikwa mkono. Hakutaka kugeuka ili kutazama, maana alijuwa ni Eddy. Taratibu alifumba macho na kujikaza.

"Naomba tuongee" Eddy aliongea kwa sauti ya chini na kumkumbusha mbali enzi mapenzi yao yameshamili. Shaida Taratibu alianza kuutoa mkono wake kwake bila kumjibu chochote. Ila Eddy hakutaka kumuachia.

"Tafadhali dakika mbili tu"

"naomba Uachie mkono wangu" sauti ya Shaida ilimdhihirishia Eddy kuwa anauchungu usiyo na kipimo. Ndipo Eddy alimuachia kisha Shaida akashuka haraka huku machozi yakianza kumtiririka.

"Ohh my God, nimesubiria niletewe chocolate ili na Mimi nijuwe radha yake ajabu mtu mwenyewe anarudi akilia" Aisha aliongea kiutani baada ya kumuona mdogo wake akirudi analia.

"Sizani Kama ntavumilia kuishi hapa" aliongea Shai baada ya kukaa kitandani.

"Unamaana gani au Eddy kakupiga"

"Ili anipige Mimi ni Nani kwake, najaribu kumsahau... Tatizo lililopo, kila Mara anazunguka kichwani mwangu"

"OK mchukuwe mwanao muondoke"

"Unamaana gani "

"Sina muda wa kukubembeleza Kama wewe ni kipofu utaendelea kupapasa tu" Aisha alimuachia maswali mdogo wake na kuamua kulala zake.

"Ila kweli. Mtu mwenyewe ameoa zake ila Mimi nataka kujifanya kumlilia. huu si ni upuuzi" alijisemea Shai na kulala.

"Sasa mtoto yuko wapi?" Aisha alimhoji.

"Yupo kwa Anita"

"Atalala huko? "

"Sijui"

Baada ya muda Anita alimrudisha Umy kutokana alikuwa Tayari kasinzia.

"Nimempatia chocolate amekataa kwanini jamani" aliongea Anita baada ya kumlaza kitandani.

"Ushamba unamsumbua" Aisha aliongea na kumfanya Shai aangue kicheko.

"Yaani katema "

"Eee hajazowea mambo ya kibosi" shai aliongea.

"Haina shida atazowea, ngoja niwatakie usiku mwema"

Anita aliwaaga na kuelekea chumbani kwake.

"Baby toka nimuone Umy natamani nipate mtoto wa kike " Anita aliongea Huku akiwa amelala na mumewe Eddy.

"Umempenda? "

"Tena saana, yaani kitoto kizuri sijui nisemeje"

"Usijali utapata wako"

"Halafu inaonekana mtoto amekulia kwenye mazingira magumu mno, mpaka chocolate kashindwa kula " maneno ya Anita yalimkumbusha Eddy kule alikokutania na Shaida.

"Nikweli maisha ya Kule siyo mazuri"

"Unapajuwa?" Anita alimhoji kwa mshangao.

"No! I mean huko uswahilini walikotoka"

"Aah yawezekana"

Baada ya siku kadhaa, Anita alimfuata Shaida ambae alikuwa jikoni akiandaa chakula cha mchana.

"Naona unaandaa vitu vitamu" aliongea Anita baada yakumfikia.

"Acha kunicheka. Kwanza itabidi unifundishe kupika birian yaani inanipiga chenga hatari"

"Usijali mwaya, halafu kuna Mahala nataka unisindikize Kama hautijali"

"Wapi? "

"Nyumbani kwetu please usikatae"

"Tatizo napika na mtoto amelala"

"Jamani, nimeongea na Aisha kaniambia Nije kukwambia wewe maana yeye anamkataba wa kulala. sasa sijui Nafanyaje"

Muda huo aliingia Aisha na kusema.

"Shaida nenda, kuhusu kupika ntapika, na kuhusu mtoto ntamwangalia mimi"

Anita na Shaida, walivaa kisha wakaelekea kwao na Anita ili kuwatambelea wazazi wake.

"Hey sister bado msosi? " aliuliza Husna baada ya kuingia jikoni.

"Bado kidogo " Aisha alijibu.

"OK mtoto yuko wapi "

"Amelala"

"Naenda kumuamsha"

"Usimuamshe atasumbua nyonyo"

"Hapana ntampa bomvita"

Husna moja kwa moja alielekea chumbani, akamkuta mtoto amekaa Huku akiwa ameanza kulia. Haraka alimchukuwa na kuanza kumbembeleza.

Upande wa Shaida, walifika na kukaribishwa. Anita alifurahi kuwaona wazazi wake ndipo alianza kuwapiga story za ukweni kwake. Kama dakika Mbili alifika kijana Mzuri na kuwasalimia.

"Shkamoni"

"Wow my kaka I miss you" Anita aliongea na kunyanyuka ili kumkumbatia Kaka yake.

"Staki na sijakumiss pia"

"Mamy unamsikia mwanao"

"Zawadi yangu iko wapi"

Anita alichomoa saa ya thamani na kumuonesha mdogo wake ambae aliipokea kwa furaha na kumkumbatia.

Baada ya muda wakiwa wanapata chakula cha mchana. Macho ya Sharif ambae ndo kaka yake Anita, kila Mara yalitua kwenye uso wa Shaida na kumfanya Anita atabasamu baada ya kugundua.

Muda ulienda mpaka majira ya usiku. Upande wa huku Umy alisumbua Sana kiasi Kwamba familia nzima akiwemo Eddy kuchukuwa jukumu la kumbembeleza ila haikuwezekana.

"Sasa dada tunafanyaje mbona kalia muda mrefu" Husna aliongea.

"Ndo tatizo la Shaida. Anamjuwa mwanae alivyo ila anaenda kukaa huko masaa yote" alijibu Aisha.

"Em mleteni hapa" alikuwa ni mzee wa nyumba kaongea, jambo Ambalo lilimpa hofu Aisha.

"Hapana boss atanyamanza muda huu"

Muda huo Eddy alitokea huku akiwa anajaribu kumpigia mkewe simu.

"Inaita hapokei? " aliuliza baba yake.

"Yaani hapatikani Kabisa" Eddy alijibu.

Mzee alimchukuwa Umy na kuanza kumbembeleza. Aisha aibu ilimtawala mpaka kumwangalia Eddy usoni akashindwa.

"Kwanini haupatikani?" aliuliza Eddy baada ya mkewe kupokea simu.

"Sorry dear, tuponjiani.. ntakuelezea sababu, halafu huwezi kuamini Sharif amempenda Shaida"

"What!"

ITAENDELEA.........




TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21