Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2022

Chelsea Kumtumia Werner Kama Chambo Kuinasa Saini ya Neymar, PSG Yataka Dau Nono

Picha
KLABU ya Chelsea ipo katika hatua nzuri ya kukamilisha dili la kuinasa saini ya Winga wa Paris Saint German Neymar Da Silva Junior kwa kitita cha Euro milioni 113 pamoja na Timo Werner kama sehemu ya dili hilo.   Kwa mujibu wa gazeti la habari za michezo la Italia Carciomercato limeripoti kuwa Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi amebariki dili hilo liendelee ingawa amesisitiza kuwa kiasi cha pesa lazima kiongezwe kutoka Euro Milioni 113 hadi 150 pamoja na Timo Werner ili kumruhusu Neymar kuondoka katika viunga vya Parc De Princes. Habari za Neymar kutakiwa kuondoka ndani ya Klabu hiyo ya PSG zimepamba moto kwenye vichwa vingi vya magazeti na vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni mipango ya Mshauri Mpya wa benchi la ufundi Luis Campos kuto ona umuhimu wa nyota huyo ndani ya kikosi hicho kwani anaamini hajitumi kuisaidia klabu hiyo. Campos aliyechukua mikoba ya Mbrazil Leonardo ni raia wa Ureno amabye amekuwa kwenye tasnia ya mpira wa miguu kwa miaka min...

SHAIDA SEHEMU YA 4

Picha
SIMULIZI: SHAIDA MTUNZI: AISHA KHAN SEHEMU YA NNE ILIPOISHIA Eddy hakusubiri Sana, aliondoka Haraka na kumuacha dada yake akimlalamikia SONGA NAYO Baada ya muda, Shaida na dada yake walikuwa nyumbani kwao Manzese huku wakipanga nguo ili kuhamia kwa kina Eddy. Muda wote Shai alikuwa ni mwenye kulia bila kuchoka. "Aisee ningejuwa kuwa nipo na mtu mzaifu Kama wewe, wallah nisingekubali Kuja huku " Aisha aliongea. "Usiseme hivo dada" "Mtu uliekuwa unamtafuta umemuona na tayari umeuona moyo wake ulivyo, nini shida mbona sikuelewi? Au chukuwa nauli rudi kwa baba kisha ntakuwa nikikutumia pesa ndogo ndogo" "Dada, silii kisa siwezi kufanya kazi, hapana! Nalilia muda Wangu nilioupoteza kumfikiria... Naomba niache nilie nikichoka ntakwambia" Majira ya jioni walifika kwa boss wao, wakakaribishwa na kupewa chumba cha kulala kimoja kilichomo vitanda viwili. "Naendelea kusisitiza, jifanye Kama vile hujawahi kumuona kabla. Chochote atakachokifanya na mkewe...