SHAIDA SEHEMU YA 2



SIMULIZI: SHAIDA

MTUNZI: AISHA KHAN

SEHEMU YA PILI

TULIPOISHIA: "We Aisha nakuheshimu" Ndende alimnyooshea kidole ishara anaweza kumfanyia chochote kibaya.

"Weeee!!! Subutu nikusambaze muda huu, au umesahau nilivyokua na kukunguta utotoni"

"Nini kinaendelea?" ilikuwa ni swali kutoka kwa baba yake Ndende ambae alifika muda huo.

SONGA NAYO

Wote kwa uoga waligeuka kumtazama bila kujua watamjibu nini ili kujitetea.

"Tutazidi jamani" Aisha aliwaaga baada ya kuona kizazaa kimeingilia kati, ila baba yake Ndende alimsimamisha akisema.

"Nauliza tena nini kinaendelea?" baba yake Ndende alionekana kutaka kujua kiundani ila wote wakakaa kimya kuashilia hakuna kilichotokea.

Siku zilisonga ndoa ya Eddy na Shaida ilifungwa, wakaishi kama mke na mume jambo ambalo Eddy alilitamani kwa muda murefu licha alikuwa hajui kama kweli anampenda Shaida ama anapenda tendo la ndoa, ingawa Shaida aliamini mia mia kuwa anapendwa na atadumu kwenye ndoa yake.

Maisha yalisonga, kile walichokifuata kina Eddy walikifanikisha kwa miezi mi tatu tu jambo ambalo hawakutarajia maana walihisi ingewagharimu hata mwaka.

Siku moja Shaida alikuwa amekaa na dada yake nyumbani kwao huku wakipiga story.

"Yaani dada huwezi kuamini kuishi kote na Eddy bado tu namuogopa" Shaida aliongea na kumfanya dada yake acheke.

"Kwa nini sasa"

"Eddy yupo tofauti sana, yaani nimkimya mpaka muda mwingine nahisi hanipendi, istoshe angalia alivyopaa angani na alivyomzuri yaani mpaka naona hatuendani kabisa"

"Aahh nimeona tatizo lako hujiamini ila mbona wewe ni mrembo na mmeendana tu"

"Yaani unaweza kukuta tumekaa kimya ndani, yeye zake amevaa earfone yupo bize kama nusu saa haongei. Akishaniona nimeboweka sasa, ananiangalia na yale macho yake, nikimtazama ananiuliza na ile sauti yake nzito upo sawa" maneno ya Shaida yalimfanya dada yake acheke kwa furaha huku Shaida nae akimsaidia kucheka.

"Enhe ndiyo inakuaje, nipe umbea mdogo wangu"

"Kama ulivyonifundisha nakubali kwa hofu"

Waliangua kicheko wanandugu hao maana upendo na furaha ndiyo walijaaliwa.

"Kisha inakuaje?"

"Ananiita naenda kukaa karibu yake kisha ananipa earfone ya sikio moja tunasikia wote, sema nini uoga nilionao juu yake sizani kama utaisha"

"Usijali ipo siku utamzoea, sijui mkienda zenu mjini ntaishije mimi"

"Usijali ntakuwa nakuja kuwaoneni"

Wakiwa wanazidi kupiga story zao, muda huo alifika Eddy na kusalimia.

"Shem vipi"

"Safi shemeji za mida" Aisha alijibu salamu.

"Safi, nikunyang'anye mdogo wako kwa muda" Eddy aliongea kiutani na kuwafanya wote watabasamu.

"Haina shida" Aisha alijibu na kumgeukia mdogo wake.

"Shai nenda tutaonana siku nyingine"

Shaida alinyanyuka na kumfuata Eddy, baada ya kumfikia Eddy alimshika mkono Shai kisha wakaondoka huku Aisha akiwasindikiza kwa macho, kwa mbali tabasamu ikiutawala uso wake maana alimuombea sana mdogo wake ndoa yake iwe yenye furaha muda wote.

"Maji ndani hamna" aliongea Eddy baada ya kufika nyumbani.

"Samahani sikujua" Shaida alijiona mpumbavu kwa kutokuwa makini kwenye kazi ndogo ndogo za ndani hali ya kuwa ni jukumu lake.

"Hapana nimemaliza kuyatumia mimi, si unaona nimefua" Eddy alimuonesha nguo zake alizozianika kwenye kamba na kumuondoa wasi wasi mkewe.

"Chukua dumu mbili ntakusaidia kuchota maji" Eddy kidogo alimshangaza Shaida licha Shai alihitaji kumhoji kwanini alifua na ile hali yupo ila akashindwa kumhoji kutokana na kumuonea aibu kila mara. Shai aliingia ndani na kutoka na dumu mbili kisha wakaongozana mtoni.

Walipofika mtoni, Shai alianza kuchota maji kupitia kijagi kidogo kilichowekwa mtoni kwa ajili ya kuwasaidia kuchotea maji.

"Shai nahitaji kuondoka" Eddy aliongea huku akiwa amekaa pembeni akimtazama mkewe anavyojaza dumu.

"Wapi?" Shai alimhoji bila kuelewa vizuri anachokiongea Eddy.

"Yeah nataka kurudi dar es salam"

"Vipi kuhusu mimi" mara hii Shai alijitoa muhanga na kumuuliza kijasiri.

"Njoo" Eddy alimwita kisha Shai akaacha kazi aliyokuwa anaifanya na kumfuata Eddy alipokaa, alipomfikia alikaa karibu yake kisha Eddy akaupitisha mkono wake wa kulia mgongoni kwa Shaida na kumshika mkono kisha akamlaza kifuani kwake huku uso wa Shaida ukiwa umepoteza furaha kabisa.

"Nataka nirudi mjini ila ntarudi kwa ajili yako"

Shai Uzalendo ulimshinda akaamua kujitoa kwa Eddy na kumtazama kijasiri tofauti na siku zote.

"Utaniachia nani?"

"Usijali siyo kusema nakuacha, hapana ntarudi kwa ajili yako"

"Ila mimi siyo mkeo?"

"Wewe ni mke wangu"

"Kwanini usiende na mimi"

"Niamini Shaida, naenda kuweka mambo sawa kisha ntarudi kwa ajili yako"

"Hapana Eddy unataka kunitoroka"

"Nakutorokaje na wewe ni mwanamke wangu"

"Haki ya Mungu siwezi kukuelewa"

"Ona baby ...acha nikaweke mambo vizuri nyumbani ili ufikie sehemu iliyosalama"

"Eddy hapana tutaweka salama kwa pamoja" Shaida kupinga kwake kulimpelekea Eddy kuchukia na kuanza kumfokea.

"Sasa wewe unatakaje, wewe ni mwanamke wa aina gani usieelewa... mbona upo tofauti na wanawake wengine! au nia yako niache nimekupiga ndiyo useme Eddy mtata, kukubembeleza kote wewe bado huelewi tu. aisee usinifanye nichukie" maneno ya Eddy yaliyojaa hasira na lawama yaliweza kumfanya Shaida atulie na kukubali bila kipingamiza.

"Nisamehe unaweza kwenda" shai aliongea kinyonge.

"Siyo uongee hivo, niruhusu kutoka moyoni"

"Nimekuruhusu"

Eddy alimshika mkewe na kumkumbatia huku akimbusu kichwani.

Alfajiri Shai aliamka kutoka usingizini na kupapasa anapolalaga mumewe ila hakumsikia, jambo lilolomstua sana na kutazama kitandani vile vile hakumuona, haraka macho yake aliyaelekeza ambapo begi ya nguo ya Eddy inapokuaga siku zote, vile vile hakuiona na hapo ndipo alijua tayari mumewe amemuacha.

Kikaratasi kidogo kilichokua pembeni yake ndicho kilimzihirishia licha alikuwa hajakisoma.

"Ntakupenda daima" ujumbe uliyoandikwa kwenye karatasi ile, ulimfanya Shai autafakari mara kadhaa bila kuupatia majibu.

"Ntakupenda daima? Au hatarudi! Ntakupenda ndaima?" neno dogo lenye uzito mkubwa ndani yake lilimfanya binti mrembo mwenye macho ya mvuto machozi yaanze kumtoka bila kujua nini kitafuata kwenye maisha yake, ukija kuangalia hajui wapi mumewe alikotoka wala ndugu zake, bila kujali ndipo kunapambazuka aliamka na kuangaza wanakolala mashemeji zake ila na wao pia hakuweza kuwaona. Haraka alielekea kwao ili kumpa taarifa dada yake ikiwezekana aweze kumsaidia, alipofika alimgongea dirishani kisha Aisha akaamka na kufungua mlango.

"Vipi muda huu kulikoni" Aisha alimuuliza mdogo wake huku akipiga myayo kutokana na usingizi kuwa bado machoni pake.

"Mwenzio nimeachwa" Shai aliongea huku akilia.

"Umeachika?"

"Ni sawa sawa na kuachika maana Eddy na shemeji zangu wameondoka tena bila kuniaga"

"Unasema kina nani wameondoka?" alihoji mzee Athuman baada ya kutoka mlangani na kuwafanya mabinti zake wastuke na kugeuka kumtazama.

Walianza Kujing'ata ng'ata Huku wakitazamani kwa wasi wasi.

"Siyo ninyi nauliza? " Mara hii mzee Athuman alitoka mlangoni na kusimama walipo.

"Nipeni majibu haraka iwezekanavyo"

"Ahhh.. Shai mwambie tu ukweli" Aisha alimsukumia Mpira mwenye kesi.

"Nikweli baba, Eddy ameondoka" aliongea huku akilia.

ITAENDELEA........




TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21