JINI WA DARAJA LA SALENDA SEHEMU YA 2
SIMULIZI: JINI WA DARAJA LA SALENDA
MTUNZI: ALLY MBETU
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA; Kingine, hali waliyomkutanayo kama mtu aliyekuwa amefariki dunia na kushangazwa na jinsi alivyoamka na kukutwa hana ugonjwa wowote zaidi ya uchovu wa usingizi. Alijiuliza hali ile imemtokea kwa sababu gani. Akiwa katika dimbwi la mawazo shoga yake kipenzi, Sharifa aliingia. “Vipi shoga mbona leo sikusomi?” “Mmh, shoga wee acha tu kuna mambo yamenitokea yananichanganya.” “Yapi? Hebu kaa chini nikueleze yaliyonisibu najuta kwenda klabu usiku.” “Yapi tena hayo shoga?” Suzana alimueleza yote aliyokutana nayo usiku na hali iliyomkuta baada ya kumaliza kuoga ili aende kanisani na alipoamka na kukukuta watu wamemzunguka na kumueleza walimkuta akiwa kama amekufa. “Haa! Shoga unayosema ni kweli?” “Kweli kabisa.” “Huyo mtu unasema umemuona wapi?” “Daraja la Salenda” “Mmh!” Sharifa aliguna. “Mbona unaguna?” “Mbona tukio linafanana na kama langu.” SASA ENDELEA... “Lako?” “Eeeh.” “Tukio gani?” “Unajua kuna mtu nilimueleza akasema eti ni uongo na uzushi, si unakumbuka kuna tukio moja lilitamba katika vyombo vya habari?” “Tukio gani?” “Lile la msichana kuota manyoya baada ya kumpa msaada ombaomba kwenye Daraja la Salenda?” “Ndiyo.” “Mimi nilikuwa mmoja ya watu walio kataa katakata kuwa ni uzushi, Suzana mimi ni mbishi sana kukubaliana na jambo linaloonekana ni la kusadikika.” “Mh.” “Basi wiki iliyopita katika majira ya saa kumi na mbili jioni nikiwa narudi nyumbani, si unajua foleni za Dar. Toka pale Palm Beach magari yalikuwa yakienda taratibu sana, tulipofika katika Daraja la Salenda magari yalisimama. Niliendelea kusubiri huku nikisikiliza nyimbo za Injili. “Nje ya magari kulikuwa na ombaomba wachache, sikushughulika nao, niliendelea kusikiliza muziki nikisubiri foleni isogee. Nilishtushwa na dirisha kugongwa kwa nje, niliponyanyua macho nilimuona ombaomba wa kike akitaka msaada kwangu. “Huruma iliniigia, nilifungua dirisha kidogo na kumpa noti ya elfu moja, halafu nilifunga dirisha na kuendelea kusikiliza muziki. Nilishtushwa tena dirisha kugongwa, nilipoangalia nilimuona yule yule ombaomba wa kike. Nilijiuliza ana shida gani ya kugonga tena, safari hii nilijikuta nimefungua kioo mpaka chini na kumuuliza: “Una shida gani tena?” Yule ombaomba aliyekuwa ameinama na uso wake kuzibwa na nywele nyingi alinyanyua uso wake na kunitazama, alionesha kama kunishangaa. Nilijiuliza mbona amenishangaa huenda kanifananisha na mimi nilikaza macho kumwangalia. Kilichonishangaza zaidi ilikuwa sura yake iliyofanana sana na yangu kama pacha. Moyo ulinilipuka ajabu, kuna kitu nilikiona kikitoka kwenye macho yake na kupiga kwenye macho yangu na ghafla alitoweka.” “Weee!” Suzana alishtuka. “Ndiyo maana nikasema tukio kama langu japo tofauti yake ni ndogo sana. Baada ya foleni kuanza kutembea, niliondoa gari na kwenda moja kwa moja nyumbani. Amini Suzana tukio lile wala sikulitilia maanani kwa vile sikulielewa na pia sikuwa muumini wa mambo ya kishirikina.” “Mh!” “Basi shoga, siku ile nyumbani nilikutana kimwili na mume wangu. Kama kawaida mzunguko wa kwanza ulikwenda vizuri, ajabu wa pili hakuwa na nguvu. Kila alivyojitahidi nguvu zake za kiume ziligoma.” “Mmh!” Suzana aliguna na kujitengeneza vizuri kwenye kiti chake. “Tokea siku ile mpaka leo mume wangu hana nguvu za kiume.” “Usiniambie!” “Kweli kabisa.” “Sharifa unataka kuniambia ombaomba yule ndiye aliyesababisha yote hayo?” “Sasa napata picha kuwa sehemu ile kweli kuna kitu kinafanyika.” “Kwa hiyo unataka kusema ni kweli pale kuna jini kama watu wanavyoamini?” “Sina uhakika kama ni jini lakini kuna kitu kibaya.” “Kwa hiyo hata ya mwanamke kuota manyonya ni kweli?” “Inawezekana.” “Mmh! Kama ni kweli basi tuna hatari, kwani yule mwanamke alipatikana?” “Nilisikia alionekana ufukweni akiwa uchi na akili zake kama chizi.” “Unataka kuniambia ndiye aliyetutokea?” “Huenda.” “Basi kuna umuhimu wa kulifanyia kazi jambo hili.” “Ngoja tutafute ushauri wa watu wazima.” “Kwani mumeo ulimueleza uliyokutana nayo?” “Sikumueleza kwa kuamini hali ile imetokana na yeye kutoka nje ya ndoa.” “Una uhakika gani?” “Suzana, sasa naingiwa na imani hiyo kutokana na tukio lililokutokea wewe.” “Sharifa kabla ya kutafuta ufumbuzi mbadala kwa nini usikae chini na mumeo kutafuta sababu ya yeye kuwa vile?” “Suzana mume wangu namfahamu vizuri, hata kama anatembea nje haijawahi kutokea, ninaye mwaka wa kumi sasa.” “Mmh! Bado haijawa sababu, kwani yeye anasemaje?” “Kwa kweli nyumba yetu imeingia matatizo ya kulaumiana huku nikimlaumu mume wangu na yeye kusema haelewi sababu ile inatokana na nini.” “Mmekwenda hospitali?” “Suzana wazo hilo sikuwa nalo, akili yangu yote niliielekeza kwenye lawama.” “Sharifa hasira siku zote haijengi ulitakiwa kumsikiliza mwenzako.” Wakiwa tukiwa katikati ya mazungumzo Brighton mpenzi wa Suzana aliingia. Baada ya kusalimiana Sharifa aliwaaga na kuwaacha wapendanao wazungumze. Baada ya kuondoka Sharifa alimuangalia Brighton kwa jicho la hasira. “Vipi sweet, mbona unaniangalia hivyo?” “Brighton wewe wa kunifanya hivyo, nimepungukiwa nini mwilini mwangu kufikia hatua ya kunidhalilisha kiasi hicho,” Suzana alimlalamikia mpenzi wake.
“Sikumueleza kwa kuamini hali imetokana na yeye kutoka nje ya ndoa.” “Una uhakika gani sababu ya mumeo kuwa hivyo ni kutokana tukio lile?” “Suzana sasa naingiwa na imani hiyo kutokana na tukio lililokutokea.” “Sharifa kabla ya kutafuta ufumbuzi mbadala kwa nini usikae chini na mumeo kutafuta sababu ya yeye kuwa vile?” “Suzana mume wangu namfahamu vizuri, hata kama anatembea nje haijawahi kutokea ninaye mwaka wa kumi sasa.” “Mmh! Bado haijawa sababu, kwani yeye anasemaje?” “Kwa kweli nyumba yetu imeingia matatizo ya kulaumiana huku nikimlaumu mume wangu na yeye kusema haelewi sababu ile inatokana na nini.” “Mmekwenda hospitali?” “Suzana wazo hilo sikuwa nalo, akili yangu yote niliielekeza kwenye lawama.” “Sharifa hasira siku zote haijengi ulitakiwa kumsikiliza mwenzako.” Wakiwa katikati ya mazungumzo Brighton mpenzi wa Suzana aliingia, baada ya kusalimiana Sharifa aliwaaga na kuwaacha wapendanao hao wazungumze. Baada ya kuondoka Sharifa alimuangalia Brighton kwa jicho la hasira. “Vipi Sweet mbona unaniangalia hivyo?” “Brighton wewe wa kunifanya hivyo, nimepungukiwa nini mwilini mwangu kufikia hatua ya kunidhalilisha kiasi hicho?” Suzana alimlalamikia mpenzi wake. ... “Suzana nimekufanya nini tena mpenzi wangu?” “Hujui...hujui eeh, juzi umenifanya nini Bilicanas?” “Sasa Suzana nani wa kulaumiwa kati yangu na wewe?” “Brighton unachukua mwanamke unaniacha club peke yangu, nilikulazimisha kuwa na wewe siku hiyo, si ni wewe ndiye uliyenipigia simu nije tujumuike wote kisha nikalale kwako. Kama ulijua una miadi na mwanamke mwingine kwa nini uliniita?” Suzana alijisahau kama yupo ofisini na kujikuta akitokwa na machozi ya uchungu. “Mimi?” “Kwani nazungumza na ukuta?” “Suzana juzi si nilikuacha unakunywa mimi nikapanda juu kuzungumza na Shakoor, nilipoteremka nilishangaa kukuta meza nyeupe na vinywaji vipo kama nilivyoviacha. Nilijua umekwenda msalani lakini muda ulipokwenda sana ilibidi nitoke nje kukutafuta. Kilichonishangaza sikukuta gari lako ilibidi nikodi teksi hadi nyumbani kwa kuamini umekwenda huko. “Kila nilipopiga simu yako iliita bila kupokelewa, nilipofika nyumbani kwangu sikukuta, nilisubiri kwa saa moja mpaka saa tisa na nusu. Baada ya kutokukuona niliamua kukufuata kwako, nilikuta mlango umefungwa. Nilipomuuliza mlinzi aliniambia hujarudi. “Hapo nilichanganyikiwa, nilijiuliza utakuwa wapi? Huwezi kuamini mpaka kunakucha nilikuwa sijapata jibu. Simu yako kila nilipopiga iliita bila kupokelewa, nilirudi nyumbani na kuamua kujilaza kidogo niende kanisani misa ya pili kutokana na uchovu wa kutopumzika. “Amini usiamini nimeamka saa tatu usiku toka saa moja asubuhi nilipoweka ubavu, toka nizaliwe na kuwa na akili zangu timamu sijawahi kutokewa na usingizi wa ajabu kama ule. Hata nilipoamka nilikuwa kamsa mlevi niliyekunywa pombe nyingi, sikunyanyuka kitandani niliendelea kulala, huwezi kuamini nililala bila kula kwa saa 24 na nilipoamka leo asubuhi nilikuwa na nguvu kama sijatokewa na kitu chochote. “Nilipitia kwako mlinzi alinieleza kama ulirudi, lakini kuna kitu kilitokea kilichoonesha kuna jambo limekupata na kuchukuliwa na familia yako. Mimi kiguu na njia mpaka kwenu, nilipofika niliambiwa umekuja kazini na afya yako ni salama. Kwani ulitokewa na nini?” “Yangenitokea bila wewe?” “Bila mimi kivipi Suzana?” “Eeh, kama ningekwenda kwako unafikiri ningekutana na mauzauza, Brighton uliondoka na mwanamke unajitetea tu,” Suzana alizidi kulakamika. “Suzana mpenzi wangu tuna muda gani juzi nifanye hivyo?” “Si umenichoka.” “Suzana naapa kwa jina la Yesu Kiristo uliniacha juu sikutoka na mwanamke muulize hata Shakoor kama nilitoka na mwanamke au muulize mlinzi wako nimefika kwako saa ngapi?” “Itanibidi nikubali kwa vile nakupenda.” “Suzana mpenzi wangu niamini siwezi kwenda kunyume na ahadi yetu, nakupenda na sitakusaliti hata siku moja.” “Basi yamekwisha lakini uliniumiza sana.” “Mh, eti ulipatwa na nini?” “Samahani Brighton toka niingie ofisini sijafanya kazi yoyote, naomba unipe muda baada ya kazi nikitoka hapa nikakuja kwako moja kwa moja tuzungumze, ni mazungungumzo marefu.” “Nigusie hata kidogo” “Ni kuhusu nilipotoka Bilicanas na mambo niliyokutata nayo njiani.” “Mambo gani?” “Nimekueleza nitakueleza au unataka nifukuzwe kazi?” “Basi mpenzi wangu nimekuelewa.” Waliagana Brighton na mpenzi wake Suzana na kumuacha akifanya kazi. Baada ya kuondoka Brighton, Suzana alijikuta akihamia kwenye maelezo ya Brighton juu ya hali iliyomtokea ya kulala zaidi ya saa kumi na nne. Alijiuliza kama yeye alikutana na maajabu yale, Brighton alikutana na kitu gani. Kazi kwake ilikuwa nzito siku ile, aliomba ruhusa na kurudi nyumbani kupumzika, kabla ya kutoka alimjulisha mpenzi wake kuwa anatangulia nyumbani kwake. Baada ya kutoka kazini alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa mpenzi wake, kwa vile alikuwa na funguo za nyumba alifungua na kuingia ndani. Alipoingia alishangaa kukuta chumbani kumesafishwa tofauti na siku zote, mara nyingi usafi wa nyumba ile alikuwa akifanya yeye. Ile haikumsumbua akili yake aliamini kutokana na msongo wa mawazo hali ya usafi ya nyumba ingemfanya asisumbue mwili wake zaidi ya kwenda moja kwa moja chumbani kujilaza. Hali ya hewa ndani ilikuwa nzuri tofauti na siku zote huku harufu ya manukato aliyowahi kuyasikia alipokutana na maajabu ya dalaja la Salenda. Upepo mwanana uliompuliza ulimfanya apitiwe na usingizi bila kujijua, katikati ya usingizi alishtushwa na Brighton akimpapasa. “Aah, mpenzi umerudi zamani?” “Kama robo saa.” Kwa vile Brighton alikuwa amekwishaoga Suzana naye alikwenda kuoga na kujumuika wote kitandani. Kama kawaida walisafiri katika meli ya wapendanao, safari ya kwanza ilianza vizuri kila mmoja aliifurahia. Baada ya safari ya kwanza kwisha Suzana hamu ilikuwa bado haijamuisha alitaka asafiri safari moja zaidi ndipo wapumzike. Ajabu kila alipomgusa mwenzake jogoo alikataa kuwika kitu kilichomshtua Suzana. “Vipi mpenzi mbona hivi?” “Hata mimi nashangaa.” Nini kimempata Brighton? Au ndiyo yaliyompata mume wa Sharifa?
Kwa vile Brighton alikuwa amekwishaoga, Suzana naye alikwenda kuoga na kujumuika wote kitandani. Kama kawaida walisafiri katika meli ya wapendanao, safari ya kwanza ilianza vizuri kila mmoja alifurahia safari ile. Baada ya safari ya kwanza kwisha, Suzana hamu ilikuwa bado haijamuisha, alitaka asafiri safari moja zaidi ndipo wapumzike. Ajabu kila alipomgusa mwenzake, jogoo alikataa kuwika kitu kilichomshtua Suzana. “Vipi mpenzi mbona hivi?” “Hata mimi nashangaa.” .. “Au umeanzia kwa mwingine?” “Lakini kwa nini kila linapotokea tatizo unanifikiria vibaya kuwa nilikuwa na wanawake? Siku hizi sina kazi, kazi yangu kutembea na wanawake,” Brighton alilalamika. “Mbona leo imekuwa hivi?” “Hata mimi nashangaa.” Suzana alijitahidi kumkanda mpenzi wake kumrudisha kwenye hali ya kawaida lakini hakukuwa na mabadiliko, jogoo alikataa kuwika. Aliamua kumwacha ajipumzishe waendelee baadaye. Alijilaza pembeni ya Brighton aliyeonekana mwingi wa mawazo. Suzana akiwa amejilaza alikuwa na yake aliyokuwa akiwaza, ghafla mazungumzo yake na Sharifa yalijaa kichwani na kuyakumbuka maneno aliyoelezwa juu ya tatizo la mume wake. “Basi shoga, siku ile niliporudi nyumbani nilikutana kimwili na mume wangu kama kawaida mzunguko wa kwanza ulikwenda vizuri, ajabu wa pili hakuwa na nguvu kila alivyojitahidi, nguvu za kiume ziligoma.” Sauti ile ilijirudia kichwani mwake na kumfanya atishike na kuamini huenda tatizo la Sharifa limempata na yeye. Bila kujielewa, alijikuta akikaa kitako na kumshtua Brighton aliyekuwa katika dimbwi la mawazo. “Brighton,” alimwita kwa sauti ya juu japo alikuwa pembeni yake. “Unasemaje?” “Hali hii imekutokea mara ngapi?” “Suzana swali gani hilo, toka niwe na wewe hali hii imeshanitokea?” “Hapana, basi utakuwa na tatizo la muda mrefu.” “Lakini siamini huenda ni uchovu ngoja nipumzike kidogo tutaendelea,” Brighton alimtoa hofu Suzana. “Mmh! Sawa,” Suzana aliguna akiwa na wasiwasi na maneno aliyoelezwa na Sharifa ya mpenziwe kuwa amekufa nguvu za kiume. Kila mmoja alilala upande wake, mchana waliamka na kwenda kupata chakula cha mchana. Wakiwa wamekaa wanakula, Brighton akamsifia Suzana kwa usafi aliofanya na kuifanya nyumba ipendeze. “Mpenzi umetumia muda gani kufanya usafi ule?” “Usafi gani?” “Wa nyumba,” kauli ile ilimshtua Suzana na kuamini kabisa tayari nyumba yao imeingia kwenye tatizo lakini hakutaka kulikubali mara moja ili kuficha kila anachokiwaza, alijikuta akikubali pongezi zisizo zake. Baada ya kupata chakula walirudi nyumbani kupumzika, kwa vile kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzake baada ya kuoga walipanda kitandani kujiachia kwa raha zao. Lakini hali ilikuwa mbaya zaidi Brighton hakuwa na nguvu za kiume. Hali ile ilizidi kumweka Suzana kwenye hali mbaya, hakukubaliana nayo, aliendelea kumsaidia mpenzi wake lakini hali ilikuwa ile ile. Suzana alijikuta akiangua kilio kitu kilichomshtua Brighton na kuhoji: “Suzana mbona unalia?” “Brighton unajiona upo sawa?” “Sijajua nikujibu nini?” “Hujioni haupo sawa?” “Hali ya leo inanishangaza hata mimi si kawaida yangu.” “Inawezekana kuwa ndiyo yenyewe,” Suzana aliropoka. “Yenyewe nini?” “We acha tu, kesho nitakwenda kumweleza Sharifa.” “Kumweleza nini?” Brighton alizidi kuyashangaa maneno ya mpenzi wake. “Naomba leo tuachane na hilo.” “Kwani umegundua nini kuhusu tatizo langu?” “Brighton sijagundua lolote.” “Mbona unasema utanijibu kesho?” “Sijajua nini tatizo, linafanana na la Sharifa.” “Sharifa ana tatizo gani?” “Brighton tutazungumza kesho, naomba niondoke.” “Si ulisema utalala?” “Kwa hali hii siwezi kulala niache tu niwahi nyumbani.” Brighton hakuwa na la kusema zaidi ya kumruhusu Suzana akalale kwao. Suzana akionekana amechanganyikiwa, aliwasha gari na kurejea kwake. Alijikuta akilia njia nzima juu ya hali ya mpenzi wake huku akijiuliza kama itakuwa hivyo mpenzi wake amekufa nguvu za kiume atafanya nini? Alipoingia ndani kwake alijitupa kitandani hata usingizi ulivyomchukua hakujua. Suzana alishtuka siku ya pili, alijiandaa kwenda kazini huku akiwa na shauku ya kuonana na Sharifa kumwelezea yaliyomsibu kama yake. Alipofika kazini kiti alikiona cha moto, hakukaa, alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Sharifa. Sharifa alipomuona alishtuka na kumkaribisha: “Mmh! Dada mbona asubuhi asubuhi?” “Wee acha tu, ukiona hivyo ujue kuna jambo.” “Karibu, mi ndo naingia sasa hivi hata vumbi sijafuta kwenye kompyuta.” “Yaani wee acha tu,” Suzana alisema huku akiketi kwenye kiti. “Mh, kuna kipi kipya?” “Kuna mapya! Yale yaliyokutokea yamefika na kwangu.” “Yapi hayo tena?” “Si yaliyomtokea mume wako.” “Unamaanisha jogoo kushindwa kuwika?” “Ndiyo.” “Ehe!” Suzana alimwelezea Sharifa yaliyomkuta, baada ya kumsikiliza alishusha pumzi na kusema: “Unajua unaweza kuona nakutania .” “Kwa kipi?” “Jana usiku nilipokutana na mume wangu huwezi kuamini, nimefurahia tendo kama kawaida.” “Wewee! Mara zote?” “Tena ajabu lilikuwa penzi tamu ajabu hata asubuhi nimeamka nilihisi kama siku ya kwanza kuonana na mume wangu.”
ITAENDELEA........
TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.
Maoni
Chapisha Maoni