ADUI WA MAISHA SEHEMU YA 5



SIMULIZI: ADUI WA MAISHA

MTUNZI: LISSA WA MARIAM

SEHEMU YA TANO

Baada ya kutoka hospital Isabella alifanya taratibu za kwenda mwanza, baadhi ya wanafunzi na walimu walimchangia rambirambi, Lameck nae hakumuacha pekee yake, kama alivyoahidi alitoa kiasi cha pesa kwenye akaunti yake wakasafiri wote pamoja na baadhi ya wanafunzi, baada ya kufika mwanza Lameck alimtaarifu mama yake kuwa yupo mwanza

"Umeenda kufanya nini mbona gafla" Mama Lameck aliuliza

"Kuna rafiki yangu kafiwa na wazazi wake wote wawil"

"Jamani dah!! Mpe pole sasa wakimaliza mazishi si unarudi"

"Ndio mama"

"Haya kuwa makini" waliagana na kukata cmu, msiba ukaisha na baadhi ya wanafunzi wakarudi Dar, ni Lameck pekee ndie Alibaki alisubiri mpaka 40 iishe ndipo arudi, mapenzi aliyokuwa nayo kwa Isabella yalizidi Mara mbili, siku zikapita hatimae wiki ya pili ikawa inakaribia, mama yake alikasirika na kumpigia simu

"Hivi wewe upo kwa nani huko mwanza na huku chuo umemuachia nani akusomee? Hivi unajitambua wewe"

"Mama Sina muda mrefu Sana nitarudi"

"Usiniambie habari za nitarudi, umeniudhi Sana nakupa siku mbili tu uwe ushafika Dar, tofauti na hapo hatutoelewana"

Baada ya maneno hayo kutoka kwa mama yake, ilibidi Lameck amuage Isabella na kuanza taratibu za safari, siku ya pili asubuhi alikuwa tayari kwenye gari yake anarudi kwao

*******

"Ulikuwa wapi" mama yake aliuliza

"Kwank si nilikuaga mama mbona unaniuliza tena ina maana hujui nilipokuwa"

"Habari zako nishapata, kumbe una mwanamke umekaa wiki mbili, hujui kama kuna masomo"

"Basi nisamehe kesho nitaenda" Lameck alijbu na kuingia chumbani kwake akaoga na kulala

*********

Asubuhi Lameck alienda chuo, alipoingia darasan alikuta msichana mgeni kwenye macho yake amekaa kwenye kiti chake

"Habari yako hii ni sehemu yangu" Lameck alimwambia ili yule msichana aweze kupisha

"Oh kumbe ni nafasi yako basi sorry sikujua, mimi ni mgeni hapa, niliona nafasi haina mtu nikapenda nikae hapa" alisema yule msichana mrefu, mwenye hips za kufa mtu na ngozi nyeusi inayong'aa hakika alipendeza

"Ah basi wewe kaa hakuna shida"

Lameck alitoka na kukaa sehem nyingine, mara yule msichana akamfata

"Hi naitwa Jenny, nimetokea Kenya nilikuwa nasoma huko, kwasasa naishi masaki sijui unaitwa nani"

"Naitwa Lameck"

"Wow! nice to meet u Lameck tunaweza kuwa friend? Maana nimependa ukarimu wako"

"Wow!! nice to meet you Lameck, tunaweza kuwa friends? Maana nimependa ukarimu wako, it's just a friend" alisema Jenny huku akimuangalia Lameck

"Why? Lameck alijikuta akiuliza

"Kwasababu wewe ni mkarim unaonyesha ni mcheshi pia tutasaidiana mambo mengi kwenye masomo, hivyo naomba kampani usinikatalie ni urafiki tu" jeni alijibu

"Ok poa" walipeana mikono Jenni akarudi na kukaa, urafiki ukaanzia hapo zilipita siku nne wakawa wameshazoeana, Waliingia darasani pamoja, baada ya kumaliza kipindi, Lameck alitoka na Denis na kwenda kiwanja Cha basketball wakawa wanacheza, Jenny nae alifika akiwa na vinywaji mkononi, akaviweka kwenye bench lililokuwa pembeni na kusimama baada ya kuona Lameck amefunga goli, akawa anapimgia makofi, Lameck alitoka uwanjani na kwenda alipo Jenny

"Nilijua tu Kama utakuwa mchezaji mzuri ndio maana sikutaka kukuuliza" aliongea huku akitabasamu

"Kwanini ulifikiri hivyo ikiwa hujawahi kuniona nikicheza"

"The way ulivyo, mwili wako unazungumza, umekaa kimazoezi" Jenny alijibu na kuchukuwa kinywaji akampa Lameck

"Thanks" waliongea mengi Denis nae akaungana nao kupiga story wakacheka

"Jamani me naondoka zangu, Lameck unaweza kunipatia namba yako"

"Hakuna shida" alkmpa kisha akaondoka

"Mwanangu upo juu, watoto wazuri wanavyokupenda" Denis alitania "Aah wewe kausha me nina mke wangu"

"Kwani ukiwa na mke ndio Nini, mtoto akijilengesha mwenyewe unapiga tu alafu unasepa"

"Hahaha, mi Mambo hayo nishaacha muda, nataka kutulia kwenye mahusiano sasa hivi, nisije kupoteza mke bure, Bella ndo furaha yangu" Lameck aliongea akimaanisha kweli anampenda Bella kuliko msichana yoyote

"Ujue huyu Jenny anamzigo wa maana kule nyuma, Mimi ndio umenichanganya haswa alafu kachongeka lakini bella ndo mzuri bana ana kishep flan hivi amazing, alafu ile rangi yake Kama mnyarwanda flani hivi, dah Lameck shukuru mungu kakuumba handsome, bila hivyo Bella usingempata"

"Ningetumia hata pesa zangu kumpata"

"Umesahau Kama hata Bella wazazi wake walikuwa matajiri huko mwanza, yaaani siku ya msiba wanafunzi wote tulishangaa huo wadhifa unavyosomwa, alafu tulipoenda kuangalia hiyo nyumba ya baba yake iliyoungua hatari kabisa" Denis alitoa sifa kuonyesha Isabella hakuwa msichana wa mchezo mchezo kabisa, waliendelea kuwapambanisha Isabella na Jenny, Lakini baadae wote wakakiri kuwa Isabella ni zaidi ya Jenny na sio Jenny tu hata chuoni kote hakuna anayefikia uzuri wa Isabella, Kama wangegombania uzuri Basi Bella angechukuwa namba moja na ingekuwa Shep Basi jenny ndo angeshinda kwa Isabella na sio kwa wasichana wengine Maana wapo waliojazia kuliko jenny.

"Kwanza umenikumbusha kitu ngoja nimpigie simu mke wangu" alisema Lameck na kutoa simu akapiga

"Vipi mamy uko poa...sasa huku ratiba ya mtihani imetoka fanya uje tupate kusoma sawa.... usijali nitakuja kukupokea fanya uje kesho nikitoka hapa nitakutumia pesa.,.,ok bye take care honey" alimaliza na kukata simu

"Oya me naenda home" alimuaga Denis na kuachana

********

Lameck alikuwa nyumbani, siku hiyo ilikuwa ni jumamosi, Jenni akampigia simu alipokea wakasalimiana

"Nilikuwa naomba twende beach leo"

"Duh Jenny leo sina muda wangu, maana nataka nitoke kidogo"

"Una mishe gani tena Lameck tuonane bana kuna kitu nataka nikwambie"

"Si uniambie hata hapa Jenni"

"Basi ukipata muda utaniambia, maana nataka tukae sehemu ndo tuongee"

"Tufanye kesho nikija chuo au vipi"

"Basi poa" wakakubaliana,

Baada ya kukata simu Lameck aliamua kumpigia Isabella ili kujua amefikia wapi kwenye safari yake, Isabella alimwambia kuwa muda Si mrefu atakuwa amefika hivyo ajiandae kumpokea, Lameck alichukua gari na kwenda Ubungo, walikutana wakakumbatiana na kupigana mabusu mfululizo

"I miss you honey"

"Even me my love miss you more" alijibu Lameck, Waliingia kwenye gari na kuondoka, walitafuta sehemu yenye mgahawa mzuri walikaa wakala mpaka wakasaza

"Mh saa 5 kumbe itabidi tukalale nyumbani sawa" alisema na kuwasha gari wakaondoka walifika hadi Kawe wakaingia ndani walioga wakajitupa kitandan, hakika ulikuwa usiku mzuri kwao kwa mara ya pili Lameck alishiriki mapenzi na Isabella, huyu binti hakuwa na hiyana tena kwa Lameck alijikuta akimkumbatia na kumuita majina mazuri yote kwa sauti laini hatmae usingizi ukawapitia

*********

CHUONI

Lameck alifika chuo akiwa na Isabella

"Baby naenda staff mara moja nikaripoti"

"Ok utanikuta hapa" Isabella alimuacha Lameck na kuondoka, Jenny alifika na kumziba macho Lameck alafu akatoa

"Mambo ndo umefika sasa hivi" aliuliza

"Ndio"

"Ok, twende class basi alafu usije kusahau ahadi yetu, tukienda kupata lunch tuzungumze maana ni Jambo muhimu" kabla Lameck hajajibu kitu Isabella alifika akamsalimia Jenny, hapo ikabidi Lameck awatambulishe alianza kumtambulisha Jenni kama rafiki akamaliza kwa Isabella

"Jenny huyu wifi yako anaitwa Isabella au ukipenda utamuita Bella"

Jenny aliposikia hivyo alionyesha kunyong'onyea Lakini akajikaza

"Ooh nice to meet you Bella, kwani anasoma hapa" aliuliza

"Ndio ila alipata matatizo kidogo akaenda mwanza, wazazi wake wamefariki mwezi ulioisha" Lameck alijibu

"Oh sorry my dear" alijibu Jenny na kumpa mkono Isabella kisha wakawa wanaongozana wakaingia darasan, baada ya masomo kuisha, Isabella alienda hostel wakakuta na shoga yake Eliza walipiga story nyingi sana wakajikuta wakimuongelea Jenny

"Mwenzangu yule demu ana mwezi sasa hivi lakini mtu ambae yuko karibu nae ni boy wako, sasa sijui kuna nini" alisema Eliza

"Lameck kaniambia ni marafik tu"

"Mmh haya kama marafiki lakini mimi siamini" Eliza aliongea na kumfanya Bella abaki na maswali lakini hakufatilia kwani alimuamini Lameck kupita maelezo,

******

Baada ya kuwa nyumbani Lameck alimpigia simu Jenny

"hallo, sorry Jenny Leo sikuweza kupata nafasi ya kuzungumza na Wewe"

ITAENDELEA........


TUPATIE NYOTA 5 KWENYE APP YETU KULE PLAY STORE NA KU COMMENT ILI TUPATE SUPPORT YAKO.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21