SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI SEHEMU YA 16-20
Simulizi: SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI
Mtunzi: NYEMO CHILONGANI
SEHEMU YA 16
alijiona kuwa mpenzi wa Patricia japokuwa bado hakuwa ameambiwa hivyo na msichana yule.
Martin akaamua kuanza kujipanga tayari kwa kumwambia Patricia ukweli wa moyo wake, kamwe hasingeweza kuvumilia na wakati moyo wake ulikuwa ukizidi kujisikia kiu ya kufanya kile ambacho alikuwa akihitaji kukifanya. Siku hiyo aliamua kukaa sana na Patricia chumbani kwake na hapo hapo ndipo alipoamua kulitoa duku duku lile ambalo lilikuwa moyoni mwake.
“Nafahamu hata kabla haujaniambia hivyo” Patricia alimwambia Martin na kuendelea.
“Sihitaji kujiingiza kwenye mapenzi Martin” Patricia alimwambia Martin maneno ambayo yalionekana kumvunja nguvu.
“Kwa nini Patricia? Kwa nini hautaki kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi pamoja nami?” Martin aliuliza kwa sauti ndogo iliyojaa huruma.
“Unafahamu kwamba ninakupenda?” Patricia alimuuliza Martin.
“Nafahamu”
“Basi fahamu kwamba sitaki uumie” Patricia alimwambia Martin ambaye alionekana kuchanganywa na maneno yale.
“Hautaki niumie? Kivipi?” Martin aliuliza kwa mshangao.
“Wewe jua hivyo tu. Sitaki kukuumiza” Patricia alimwambia.
Patricia hakutaka kukaa sana chumbani humo, akatoka na kuanza kuongea na Bi Maria, mama yake Martin. Martin alibaki chumbani huku akionekana kuchoka kupita kawaida, maneno ambayo aliyaongea Patricia yalionekana kumuondoa nguvu zote. Mawazo yake katika kipindi hicho yakajipa uhakika kamba msichana huyo tayari alikuwa katika uhusiano na mtu mwingine na ndio maana hakutaka kuwa nae kwa kuwa aliamini angemuumiza tu.
Akainuka kitandani pale na moja kwa moja kueleka nje ya chumba kile. Kila alipokuwa akimwangalia Patricia alikuwa akichka zaidi, uzuri wa Patricia ambao alikuwa akiuona wala haikufaa kabisa kuwa rafiki yake. Patricia akaamua kuaga mahali hapo na kisha kuingia ndani ya gari pamoja na Martin.
Martin alikuwa ametulia katika kiti pembeni ya Patricia, muda wote alikuwa akimwangalia huku akionekana kumchunguza kutokana na uzuri wake ambao alikuwa nao, bado moyo wake atika kipindi hicho ulikuwa na hamu kubwa ya kuendelea kumwambia Patricia umuhimu wa msichana huyo katika maisha yake.
“Nakupenda Patricia. Nakupenda sana” Martin alimwambia Patricia.
“Nafahamu. Nakupenda pia Martin ila kuingia kwenye uhusiano pamoja nae ni kitu kisichowezekana kabisa” Patricia alimwambia Martin.
“Lakini kwa nini Patricia?”
SEHEMU YA 17
“Nimekwishakwambia kwamba sitaki kukuona ukiumia Martin. Ninakupenda sana tena sana tofauti na unavyofikiria. Sitaki kukuona ukiumia Martin” Patricia alimwambia Martin.
“Hautaki kuniona nikiumia! Kivipi? Un a mvulana au? Hata kama una mvulana, niambie tu ili nijue sababu kuliko kuniweka kwenye hali kama hii” Martin alimwambia Patricia.
“Sina mvulana na wala sihitaji kuwa na mvulana. Na kama nitahitaji kuwana mvulana basi naamini wewe ndiye utakuwa mvulana wangu” Patricia alimwambia Martin.
“Lakini mbona hautaki kuniambia?”
“Muda bado. Muda ukifika nitakwambia. Tusome kwanza” Patricia alimwambia Martin.
Bado maneno yale yalionekana kumchanganya Martin, ilikuwaje msichana akatae kuwa nae kwa kuwa alihofia kumuumiza. Kwake, alikuwa amejitoa asilimia mia moja kuumia kwa ajili ya Martin hata kama kitu gani kitatokea huko mbele lakini ili mladi tu awe nae katika uhusiano wa kimapenzi.
“Labda kama una sababu nyingine”
“Wala hakuna. Sababu ni hiyo hiyo. SITAKI KUKUUMIZA” Patricia alimwambia Martin ambaye alionekana kuwa mpole.
Je nini kitaendelea?
Je Patricia ataendelea na msimamo wake?
Je ni maumivu ya aina gani ambayo yanamfanya Patricia kutotaka kuingia katika mahusiano na Martin?
ENDELEA
SEHEMU YA 18
Martin hakuonekana kuwa na furaha hata kidogo, usiku hakukulalika hata kidogo, muda wote alikuwa akionekana kuwa na mawazo tu. Kitendo cha Patricia kumkatalia kuingia katika mahusiano pamoja nae kulionekana kumuumiza kupita kawaida kwani kila siku ndoto zake zilikuwa ni kuwa katika mahusiano na msichana huyo mrembo.
Kila wakati alikuwa akiichukua simu yake na kisha kuliangalia jina la Patricia, alitamani sana kumpigia lakini kila alipokuwa akifikiria jinsi ambavyo msichana huyo alivyokuwa akikataa kuwa katika mahusiano pamoja nae alikosa nguvu za kumpigia. Hakujua ni kwa namna gani ambavyo angeumia hapo baadae kama tu Patricia angekubali kuingia katika mahusiano pamoja nae.
Kila alipokuwa akijiuliza, alikosa jibu kabisa. Alikuwa tayari kuyapata maumivu yoyote yale ambayo yangetokea hapo baadae lakini ili mladi tu akubaliwe kuingia katika mahusiano na msichana yule ambaye alikuwa ametokea kumpenda kupita kawaida. Kichwa chake bado kilikuwa kikifikiria namna ya maumivu ambayo angeyapata baadae lakini alikosa jibu ni aina gani ya maumivu ambayo angeyapata.
Akaanza kujifikiria labda Patricia alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mvulana mwingine lakini hakuweza kukubaliana na hilo. Muda mwingi alikuwa pamoja na Patricia, je kama alikuwa na mwanaume, huyo mwanaume alikuwa wapi na alikuwa akiwasiliana nae vipi? Wazo hilo likaonekana kutokuwa na nguvu kichwani mwake jambo lililomfanya kuachana nalo.
Akaanza kufikiria kwamba labda Patricia alikuwa ameathirika lakini napo wazo hilo likaonekana kutokumuingilia akilini. Kila siku Patricia alikuwa akinawili zaidi na zaidi, je huo UKIMWI alikuwa ameupata wapi na wakati kuna kipindi alimwambia ukweli kwamba alikuwa msichana bikira, msichana ambaye hakuwahi kukutana kimwili na mwanaume yeyote yule.
Kila kitu ambacho alikuwa akikifikiria mahali hapo alikosa jibu kabisa, hakuelewa ni sababu zipi ambazo zilimfanya Patricia kutotaka kuingia katika mahusiano pamoja nae. Alijiona kuwa na kila sababu za kulalamika na kumlazimisha Patricia kuingia katika mahusiano pamoja nae.
Usiku ulionekana kuwa mgumu kwake, usingizi ambao alikuwa nao ukapotea kabisa, mawazo yake yalikuwa kwa Patricia tu, alitamani akubaliane na
SEHEMU YA 19
Patricia kwamba wasiingie katika mahusiano lakini jambo hilo likaonekana kuwa gumu kwake.
Moyo wake tayari ukaanza kupatwa na wasiwasi kwamba kuna siku Patricia angekuja kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mvulana mwingine jambo ambalo lingemfanya kuumia zaidi maishani mwake. Hakutaka kuliona jambo hilo likitokea katika maisha yake, alitamani kuwa na Patricia katika maisha yake yote.
Kichwa chake kikaanza kufikiria tena muziki, nyimbo ambazo zilikuwa zikija kichwani mwake ni zile ambazo zilikuwa na majonzi ya kuachwa na kukataliwa kuwa katika mahusiano. Martin alikuwa na kila sababu za kuandika aina hizo za nyimbo kutokana na kile ambacho alikuwa akikipitia kwa wakati huo.
******
Hali ambayo ilikuwa ikitokea kwa Martin ilikuwa ni hali ile ile ambayo ilikuwa ikimtokea Patricia. Muda wote alikuwa akimfikiria Martin, ni kweli kwamba alitamani kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na Martin lakini bado moyo wake ulikuwa ukiogopa kumuumiza.
Alimpenda sana Martin hivyo hakuwa radhi kumuumiza, alipenda sana kumuona mvulana huyo akiishi katika maisha ya furaha, hakutaka yeye kuwa moja ya sababu ambayo ingemfanya Martin kutokuishi katika maisha ya furaha na amani, alikuwa akifanya kila liwezekanalo ili kumfurahisha Martin hasa katika kipindi cha baadae na si katika kipindi hicho.
*****
Mwaka ukakatika na hatimae kuingia kidato cha nne. Urafiki wao bado ulikuwa ukiendelea kama kawaida huku katika kipindi hiki ukiwa umezidi zaidi na zaidi. Bado walikuwa wakiendelea kusaidiana kwa kila kitu. Wanafunzi wote shuleni walikuwa wakiufahamu uhusiano huo kwamba watu hao walikuwa wapenzi.
Hapo ndipo mambo yalipoanza kubadilika. Martin na Patricia wakaanza kuishi maisha kama wapenzi. Wakaanza kunyonyana midomo na kuanza kutomasana hasa katika kipindi ambacho walikuwa ndani ya gari. Miili yao ilikuwa ikizidi kuwaka tamaa ya kufanya ngono katika maisha yao. Kila mmoja akawa na hamu ya kuuona mwili wa mwenzake, siku ambayo walitaka jambo hilo lifanyike ikapangwa na kila mtu kuisubiria kwa hamu.
SEHEMU YA 20
Siku ikafika. Gari aina ya Harrier nyeusi ilisimama katika eneo la hoteli ya Mtanzania. Patricia na Martin wakateremka na moja kwa moja kuelekea mapokezini na kisha kuchukua chumba. Walipoingia chumbani tu, wakaanza kukumbatiana, mabusu mfululizo yakaanza kupigwa jambo ambalo likawafanya kuanza kusaidiana kuvuana nguo.
Ni ndani ya dakika moja, wote walikuwa watupu. Martin akaanza kufanya mambo yake, japokuwa ndio kwanza ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya kile ambacho alikuwa akikifanya lakini akaonekana kuwa kama mjuzi. Patricia alikuwa akilalamika tu pale kitandani jambo ambalo lilikuwa likimpa Martin nguvu ya kuendelea kufanya kile ambacho alikuwa akikifanya.
“Sijawahiiii....” Yalikuwa maneno ambayo yalisikika kutoka kwa Patricia.
Ni kweli. Patricia hakuwa amekutana kimwili na mvulana yeyote katika maisha yake, alikuwa bikira. Martin ndiye alikuwa mwanaume wa kwanza kuyaona matiti yake, alikuwa ndiye mwanaume wa kwanza kuyaona mapaja yake mazuri na pia alikuwa mwanaume wa kwanza kumvua nguo yake ya ndani.
Harufu nzuri ya manukato ambayo alikuwa akinukia Patricia mwilini mwake ndiyo ambayo ilimfanya Martin kuchanganyikiwa zaidi na zaidi. Alifanya kila awezalo kumlainisha Patricia mpaka pale ambapo wakaanza kuvunja amri ya sita mahali pale.
Patricia alikuwa akipiga kelele za maumivu chini ya kitovu lakini Martin hakuonekana kumuacha, bado alikuwa akiendelea na shughuli yake. Damu zikaanza kuonekana, moyo wa Martin ukaanza kuogopa lakini alipokumbuka kwamba jambo hilo hutokea kwa msichana yeyote ambaye alikuwa akifanya kitendo kile kwa mara ya kwanza, hofu ikamtoka na kuendelea.
Kitendo kile kilichukua saa moja, kila mmoja alikuwa amechoka, wakabaki wakiangaliana tu. Wakainuka na kuelekea bafuni ambako wakaoga na kisha kuondoka hotelini hapo. Hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa wao kukutana kimwili. Hawakuishia hapo, kila siku walikuwa wakiendelea kufanya zaidi na zaidi. Walifanya ngono kila sehemu ambayo waliiona kustahili kufanyiwa mapenzi.
Patricia akazidi kunawili zaidi na zaidi, urembo wake ukazidi kuongezeka zaidi na zaidi, hipsi zake zikaanza kutanuka huku mwili wake ukizidi kutamanisha.
ITAENDELEA......
BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.
Maoni
Chapisha Maoni