NANI WA KULAUMIWA ? SEHEMU YA 18
Story: NANI WA KULAUMIWA ?
Mtunzi: HADIJA MGAZA
SEHEMU YA 18
Mi mwenzio nikajua pekeangu!
Yani mpaka nahisi , pengine anajua mahusiano yetu!
" sasa we unaogopa?
"Siogopi!
" sasa, we muache tu. Pengine amevurugwa,
"Labda ,
" sasa we mbona Leo mapema sana vipi?
"Yan salma , we acha tu,
" kunani?
"Nimerudi sina ada!
" mmmh..! Kwani mama si umemkuta?
"Ndio lakini amesema , hana pesa , na kasema hato nitolea tena!
" khaa..! Kwanini sasa?
"Sielewi kabisa hapa, nawaza kweli!
" pole , sasa unafanya je?
"Sijui!
" kwani inatakiwa sh ngapi?
"Ni nyingi!
" mmmh..! Na Mimi Nina hamsini tu!
"Usijari , kama IPO IPO , nakama nimeumbwa kwa ajili ya kusoma , Nitasoma !
" ni kweli , si kam Mimi , sijaumbiwa kusoma , nimeumbiwa ,kufanya kazi za ndani!
"Ndo hivyo tena, mi namsikilizia ,
" sawa
Maana nilikua naunguza hapa hapa!
"Ungejuta Leo, na mimi nisinge kutetea hata!
" subutu , ungeona ninacho taka kukufanyia!
"Unge Fanya nini?
" ukiniomba sikupi!
"Weee_Nani kasema
Yani uninyime Mimi!
Subutu!
" sasa unafikili mi natania ,
Nisinge kupa ng'oo!
Waliendelea kutaniana pale ,
Ilivyo fika mchana , salma alimpelekea yule mzee, chakura!
"Baba karibu chakura!
" asante , vipi mama yenu hajarudi?
"Ndio!
" aaaha..! Basi naomba uniitie shakimu mala moja !
"Sawa , lakini Leo hayupo sawa!
" amefanya nini?
"Amefukuzwa shule hana ada!
" khaa..! Kwani mama yake hakumwambia!?
"Amemwambia lakini. Mama amesema hato mtolea tena,
" huyu mwanamke ashaanza ushenzi!!
"Mmmh..! Kwanini baba!
" ha ha haakuna kitu. Nenda usije ukakutwa hapa!beba na hichi chakura "
"Sasa kwanini baba!
" we nenda tu!
Salma alikua anawaza ,
Aliondoka na kuingia ndani
"We vipi mbona umepoa;?
" hakuna kitu,
"Na chakura vipi?
" hajisikii kura!
"Huyu mzee buana , yani akiisha vurugana na mama basi,
Sijui kunanini hapa!
" kwani vipi , au wanajuana ?
"Mi najua basi!
Sielewi chochote,
Aaah..
Hembu lete hicho chakura!
Nimpelekee!
Shakimu alichukua chakura na kuondoka!
" mmmh..! Mbona sielewi,
Kwanini shakimu aumie hivi,
Au kunauhusiano, ananificha?
Mmmh ...!
Ila haya nihusu haya ,
Salma aliwaza mwenyewe!
"Mzee mbona umekataa chakura?
" nimeshiba!
"Umekura nini?
" nimeshiba mwanangu !
"Sawa kama unanidanga sawa!
" wala sikudanganyi!
"Vipi leo mbona mapema umerudi;
" ada imeisha na mama kasema hana pesa!
"Hana pesa?
" ndio. Na kasema hata toa tena!
"Kwanini wakati wewe ndo.........!
" ndo nini?
"Aaaha hakuna kitu,
Ila najiuliza ni kwanini hakulipii ada ,wakati wewe ni mwanawe!
" nashangaa sana , yani amebadilika sana , simuelewi!
"Mmmh...!
" mbona unaguna!
"Hakuna kitu;
" yani mzee we una mambo sana , hivi kuna kitu gani unanificha!?
"Shakimu. Buana , hembu achana na hayo mambo,
Ila kunakitu nataka kukuuliza!
" uliza!
"Ulienda wapi asubuhi na mama yako?
" hahahaha!.
Baba buana, sasa we unataka kujua ili iweje?
"Kwani kuna ubaya , Mimi ni kama baba yako, kwanini nisikuulize?
" najua hilo mzee wangu , wewe nakuona kama baba kwangu,
Kwasababu simjui baba!
Nitakwambia tumeenda wapi!
"Nambie!!
" mama amenipeleka sehemu moja , yani kama ni ofisini,
"Eeehe ! Ikawaje?
" mmmh..mbona unaharaka hivyo?
"Basi nambie, mwishowe ukutwe hapa!
" sawa , nimeenda huko , nikakabiziwa karatasi ambayo haina kitunikasaini!?
"nini!?
Baba alisimama na kushika kichwa!
" jamani mbona umenitisha vipi
"Mungu wangu!
Kwaiyo umesaini kabisaaaa,
Hukuuliza ya nini?
" nimeuliza lakini , niliambiwa kua kunakitu anataka kunichukulia !
"Tumekwishaaaa!!!!!
Hiviii, daah...; yani shakimu
Umefanya kosa kubwa sana ..!
ITAENDELEA.......
BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.
Maoni
Chapisha Maoni