KIDAWA NO.1
Stori: KIDAWA
Mtunzi: GAOOH MUSSAH
NO: 1
Nawakaribisha wote kwa pamoja kusoma simulizi hii ya kuvutia.
Katika makuzi yangu sikuwahi kumuona baba wala mama, sura pekee niliyowahi kuiona pindi tu napata fahamu za kitoto alikuwa ni bibi, tangu niweze kuongea na kujielewa sikuona ndugu yoyote nyumbani kwetu zaidi ya majirani tu ambao nao walitutenga hakuna alieshirikiana nasi, japo nilifanya juhudi kadhaa ikiwemo kukataa kula na hata kutishia kutoroka ili tu bibi anieleze walipo wazazi wangu lakini haikuwa rahisi wala haikuwezekana kama nilivyotaka, naweza sema bibi ndio alikuwa baba, mama, na hata familia nzima, Kidawa ndio jina langu nina umri wa miaka kumi na tisa sasa(19) nimeishi nikimtumikia bibi yangu katika kazi zake, nilijua fika bibi yangu ni mchawi kweli ni mchawi mara kadhaa alikuwa akiondoka usiku na kuniacha peke yangu kitandani,na hata sikunyengine kuondoka na mimi, nilishakula nyama nyingi sana usiku alikuwa akileta nyama na kunilazimisha nile zilikuwa mbichi alinilisha kwa lazima kisha nikila ndio inakuwa furaha yake, vitendo vile vilinifanya nizoee kiasi kwamba bibi akitoka na asiporudi na nyama mbichi huwa namlilia,mazoea yalijenga tabia.
Usiku mmoja nikiwa nyumbani,niliandaa chakula ulikuwa ni ugali na nyama sikujua ni nyama ya nini bibi alireta na kunitaka niipike huku akisema kuna wageni wake watakuja usiku huo, nilitii na kuanza kupika saa kadhaa bibi aliingia, alikuwa peke yake tofauti na nilivyodhania nitegemea angekuja na wageni.
“Bibi, umerudi!” niliuliza.
“Ndio vip, chakula tayari?” nae aliuliza, hakuitika.
“ndio tayari bibi wageni wako, wako wapi?”
“Mbona wako hapa, we andaa chakula uweke mezani ugeni wa leo ni mkubwa si kila binadamu anaruhuskuwaona we bado mdogo kidawa ukikuwa utawaona!”
“Hmmmm!” niliguna mana yalikuwa mapya sikutaka kuingilia mambo ya watu niliandaa chakula kama bibi alyoagiza na kuweka mezani sambamba na maji ya kunawa, kisha nikaingia chumbani kujipumzisha.
Mbali na kuwa na miaka zaidi ya kumi na tano ila sikuwahi kwenda shule bibi hakutaka niende shule jibpekee alilonipa ni kuwa “shule nitaenda kufundishwa ujinga tu” hali ile ilinisumbua kipindi cha utoto wangu nikiwaona wenzangu wakienda shule huku wamevalia sale zao, walipendeza kuwaangalia nilikuwa nikitamani ningekuwa mimi sikuwa na bahati hiyo ila kwa sasa nishakuwa mdada sitamani tena shule, nikiwa nimejilaza juu ya kitanda cha kamba nilisiiki sauti ambayo nilitambua fika ni ya bibi.
“Kidawa…kidawa..” niliamka kutoka kitandani na kwenda nilipoitwa.
“Abee, Bibi”
“Ulikuwa umelala… kwani umeshakula!”
“Hapana, Bado ila sihisi njaa!”
“Kipi kimefanya usihisi njaa,”
“Hakuna chochote Bibi!”nilijibu huku nikijinyoosha.
“Leo kuna kazi tunatakiwa tukafanye pamoja ,”
“kazi?””Ndio mbona unashangaa kwani we ni mgeni na kazi zangu!”
“hapana bibi,”
“sawa tunatakiwa tutoke sasa,” bibi alisema, hapo yeye alikuwa kashavalia kaniki yake nyeusi, alinivalisha na mimi kaniki nyengine, kisha alisema tutoke nje tulitoka hapo nilishangaa kuona nyoka mkubwa akiwa pale nje tena akiwa na mabawa, japo tulishawahi kusafiri mara kadhaa kwa kutumia usafiri wa aina mbali mbali ikiwemo ungo hata farasi leo nilishangaa nilipandishwa kwenye nyoka mwenye mabawa, sikulijali sana jambo hilo tulikwea kisha safari ilianza, ilituchukua muda mchache nyoka yule alitua kwenye moja ya jengo kubwa ambalo tulitizamana nalo japo sikwenda shule ila kusema maneno ya kiswahili niliweza, nilisema jengo lile na kugundua palikuwa ni muhimbili, sikuwahi waza ipo siku nitafika hapo, leo imekuwa kama maajabu, bibi alinielekeza cha kufanya aliniambia niking’ate kidole changu cha mwisho cha mkono wa kushoto nami nilitii hapo nilishangaa kuona umbo langu limebadilika sikuwa binadamu tena nilikuwa paka bibi nae alibadilika na kuwa pake mweusi mwenye madoa meupe shingo aliniambia nimfate nami nilitii tukaingia wodini, mlizi hakuwa macho wakati huo alikuwa amelala, hivyo ikawa rahisi kupita muda wote nilikuwa nikitetemeka juu ya muonekano wangu ule,tuliongozana mpaka wodi ya wazazi tukaingia.
“Chagua wakike wawili!” bibi aliagiza, na mimi nilikubali, nilikuwa nikifata maagizo ya bibi bila kupinga nahisi haikuwa akili yangu kila alichosema nilifanya nakumbuka siku ile tulibeba vichanga vitano mimi nilibeba wawili yeye akachukua watatu ambao wote tuliwachanganya ndani ya ungo kisha kupakia kwenye nyoka tuliekuja nae na kuondoka eneo lile, safari yetu ilitufikisha kwenye uwanja mkubwa ambao ulikuwa kati kati ya msitu, uwanja huo ulimea viginga vya moto sambamba na kelele za hapa za hapa na pale wasichana waliimba na kucheza huku wengine wakipiga ngoma wote walikuwa wanazunguka.
“BIBi kuna nini hapa,”niliuliza.
“Tupo kwenye ibada ya kuchagua kiongozi mpya, kiongozi wet wa zamani muda wake umeisha, leo ndio analiwa nyama kisha nafasi yake anachukua mtu mwengine,” bibi alinifafanulia tukio lile, vichanga vile bibi alivipereka pale mbele kati kati ya mduara ule aliniambia kuwa ni sadaka hivyo ni amri wanapewa kila mmoja kuleta, wakati bibi amepereka sadaka yake nilibaki mwenyewe nimesimama hakuna mtu niliye mjua eneo lile walikuwa wamama na vijana wengine walitisha jinsi wanavyoonekana kila mmoja alikuwa yuko makini na shughuli yake, bibi hakuwahi kurudi alicherewa jambo hilo lilifanya usingizi uanze kunichukua nilisinzia pale nilipokuwa nimekaa baada ya kusimama kwa muda mrefu nilikaa mwishoni nikaanza kusinzia, sikujua kilichoendelea eneo lile mwishoe nilistuka nikajikuta nipo nyumbani tena juu ya kitanda, “Bibi biibiii<” baada ya kuamka niliita jina la bibi lakini sikuitikiwa nikahisi labda ameenda kwenye kuni, lakini nilikumbuka kuni tayari nilikuwa nimeleta za kutosha. “ Atakuwa ameenda wapi mbona hakuniaga na hapa nyumbani je nimefikaje?” nilijiuliza sikupata jibu, nilionelea ni bora niamke kitandani nilipokuwa nimelala, niliamka na kutoka nje kulikuwa tulivu eneo lote ni miti tu na sauti za ndege ndio nilizisikia, nyumba yetu haikuwa karibu na makazi wanayoishi watu wengine tulikuwa tukikaa mbali kidogo, bibi aliwahi kunieleza kuwa wanakijiji walimtimua baada ya kutaka kuchoma nyumba yake ndio akaondoka na kukaa mbali nao,sikuwa nikijua alipobibi japo nilipata fikra za kuwa ni mtu mzima kama katoka atarudi nyumbani mwenyewe, nilisubiri nikasubiri lakini hakurudi siku hiyo.
Siku zilipita sikumuona bibi tena nikabaki kama yatima sikuwa na ndugu wala rafiki upweke uliniandama kuishi mwenyewe porini, niliamua kuhama kule nilipokuwa naishi na bibi kisha nikarudi sehemu ambayo wanaishi watu wengine, sikuwa na mwenyeji pia hakuna aliekuwa akinijua, baada ya mwendo wa hatua kadhaa nilifika kwenye moja ya shamba ambalo lipo kando kando ya mto nilifika pale kwa ajili ya kunywa maji, sikuwa nikijua niendako nitafikia kwa na nani, baada ya kunywa maji njaa nayo haikuacha kuonesha uwepo wake nikajikalia chini ya mparachichi ambao haukuwa na dalili ya kutoa matunda, nikiwa pale mawazo yakiniandama kuwa wapi nitapata chakula kuistili njaa nilikuwa nayo wakati huo ndipo alitokea mwanamke akiwa amebeba jembe kichwani, alionekana akitokea shamba, nilimsalimu baada ya yeye kusimama akinisikiliza alikuwa ni mama wa makamo nilimweleza kuwa nimepotea sijui nitokapo wala niendapo, mama wawatu hakuwa na makuu aliniambia kuwa niongozane nae nami nikatii hapo nikampokea jembe alilobeba, tulifa mpaka nyumbani aishimo, hakuwa na mume zaidi ya kuwa na mtoto mmoja wa miaka tisa anaesoma darasa la tatu.
“Naishi na mwanangu hapa anaitwa subira anasoma darasa la tatu!”
nikiwa pale mawazo yakiniandama kuwa wapi nitapata chakula kuistili njaa nilikuwa nayo wakati huo ndipo alitokea mwanamke akiwa amebeba jembe kichwani, alionekana akitokea shamba, nilimsalimu baada ya yeye kusimama akinisikiliza alikuwa ni mama wa makamo nilimweleza kuwa nimepotea sijui nitokapo wala niendapo, mama wawatu hakuwa na makuu aliniambia kuwa niongozane nae nami nikatii hapo nikampokea jembe alilobeba, tulifa mpaka nyumbani aishimo, hakuwa na mume zaidi ya kuwa na mtoto mmoja wa miaka tisa anaesoma darasa la tatu.
“Naishi na mwanangu hapa anaitwa subira anasoma darasa la tatu!”
Tuendelee.
“baba yake yuko wapi?” nilihoji.
“Ni story ndefu ila baba yake subira alishafariki miaka kadhaa iliyopita,”
“Pole sana, mama!”
“Asante mimi nimekwishapoa na maisha yanaendelea, ila? Hujanitajia jina lako sijui waitwa nani?” aliniuliza.
“Naitwa kidawa Mama!”
“Karibu mwanangu kama utakuwa tayari utaishi hapa kwngu mpaka pale utakapo kumbuka kwenu, usijali tutaishi tu hapa,”
ITAENDELEA......
BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.
Maoni
Chapisha Maoni