FACEBOOK IMEHARIBU MAISHA YANGU SEHEMU YA 14



Simulizi: FACEBOOK IMEHARIBU MAISHA YANGU

Muandishi: GEORGE IRON MOSENYA

SEHEMU YA 14

Kwa ujasiri na tahadhari kubwa Bite akajisogeza hadi karibu kabisa na eneo ambalo aliamini hakika ndipo mlio wa risasi umetokea huku kichwani kwake akiwa ana jibu la ?nimesahau saa yangu? iwapo atakutana au kushtukiwa na mlinzi, kwa hofu alizurura katika lile eneo dakika tatu bila kuona chochoten?au wameingia nae ndani??? alijiuliza bila kupata jibu

?koh!! Koh!! Alishtuliwa na sauti ya kikohozi nyuma yake, mawazo yake alidhania ni mlinzi eneo lile lakini alipogeukz hakuwa mlinzi tena ni mwili wa binadamu ukiwa chini,hakutambua mara moja yule ni nani hadi macho yake yalipolizoea giza la pale ?Adam!!!!!?

?we ni nani??? alijibiwa kwa sauti ya chini sana iliyokuwa inaunguruma kama mnyama anayechinjwa

?Bite mimi jamani Adam?

?ondoka watakuua hao Bite ondoka niache mi nife hapa? alijibu Adam

?hapana Adam usife,usife Adam twende tukamtafute mwanetu Chrstian anatamani sana kukuona,usife Adam tafadhali? Bite alibembeleza

**********

Risasi mbili zilizopenya katika paja lake la kulia zilikuwa zimemsababishia Adam kuvuja sana damu na mbele yake alichokitarajia ni kifo hakuna kingine lakini maneno ya Bite.

Nguvu zilirejea upya kabisa tena kwa kasi?Bite ulijifungua, mtoto wangu yuko wapi? Ni wa kiume au wa kike?? alihoji maswali mfululizo Adam huku akijitutumua kusimama kwa nguvu alizokuwa amezipata

?ni stori ndefu na hapa sio mahali pake tuondoke tafadhali jitahidi kuna hatari kubwa kama unampenda mwanao jitahidi tuondoke? aliongea Bite huku akiuweka mkono wa Adam katika bega lake na kuanza kumkongoja kutoka eneo lile huku (Adam) akitumia mguu mmoja na ule uliojeruhiwa ukiwa juu juu.

Kutoka pale walipokuwa hadi barabarani haukuwa umbali mrefu sana na walifanikiwa kufika,kwa giza nene lililokuwepo hawakuweza kuonekana na mtu yeyote,nguvu zilikuwa zinamwishia Adam kutokana na kuvuja damu lakini alijikaza kijasiri sana na kuendelea mbele
********* ******* *******

Lwebe na kundi lake baada ya kumpiga risasi mbili Adam waliamini katu asingeweza kunyanyuka kutoka katika eneo lile,na hata angeweza kuinuka hakuwa na pa kwenda hakuujua mkoa huo hata kidogo. Waliingia ndani na kupiga simu kwa Bi.Gaudensia kwamba mtu wake tayari ana risasi mbili mwilini

?msimuue jamani,tafadhali sana kesho naileta pesa yenu mapema kabisa?

?nimechoshwa na ahadi zako mheshimiwa jiandae kuchukua maiti yako siku yoyote utakayotaka utaikuta nimeihifadhi na kama na kuizika nitakusaidia? alijibu kwa ghadhabu kasha akakata simu
Bi Gaudencia akapiga tena

?nakusikiliza?

?basi nielewe kwa leo na hili ni ombi la mwisho tafadhali usimuue kesho asubuhi sana nakuja huko,ninaondoka huku saa nane usiku tafadhali? alibembeleza

?na iwe hivyo atalala nje leo na hata kula hadi utakapokuja

?sawa mkurugenzi? alijibu kwa unyenyekevu Gaudensia

Akini ya Bi.Gaudensia ilifanya kazi haraka haraka akapekua kila kona katika chumba anacholala na mumewe na kwa bahati nzuri kwa akakutana na kadi ya benki ya mume wake ambayo alikuwa akifahamu vizuri kabisa namba zake za siri.

Bila kupoteza muda akampigia dereva wake wa siri ambaye huwa anampeleka Iringa naye haraka haraka bila kuhoji akatii amri aliyopewa.bila Reshmail kujua Bi.Gaudensia akaondoka majira saa saba usiku,nafsi ilikuwa ikimuhukumu juu ya baya lolote litakalomkuta Adam

?damu ya Adam ipo juu yangu?

?naenda kwa rafiki yangu ameugua ghafla ? mama Reshmail alimuaga mlinzi wa getini

?sawa bosi? alijibu mzee yule wa makamo huku akifunga geti baada ya mama kuwa ametoka nje
Kwa kasi ya ajabu gari iliondoka jijini Dar-es-salaam kwa kuwa ilikuwa usiku sana vizingiti vya watu wa usalama pamoja na foleni havikuwepo sana hivyo dereva alikimbiza gari kwa kadri ya uwezo wake.

Breki ya kwanza ilikuwa ni katika benki ya C.R.D.B maeneo ya Ubungo ambapo mama Reshmail alishuka na kuvuta pesa kutoka katika akaunti ya akiba ya mzee Manyama
Badala ya masaa matano kwa gari binafsi kufika Iringa walitumia masaa matatu pekee

?mh!! Huku napo kijijini kweli huyo nae sijui ni mgonjwa sasa usiku huu atapata wapi lifti ya gari?

Mama Reshmail alimwambia dereva wake alipoona watu wawili wakisimamisha gari

?ah!! Ndo maisha ya Tanzania yalivyo? alijibu dereva huku akiongeza zaidi mwendo wa gari hadi wakaifikia ngome ya vigogo waliyokuwa wakiifuata

**** **** *****

Magari makubwa ya mizigo yatokayo Morogoro kwenda Zambia na Malawi ndiyo yaliyotoa msaada kwa Bite na Adam ambapo Bite alijitambulisha kama mke wa Adam na kwamba wamevamiwa na majambazi na mumewe (Adam) amepigwa risasi.

Laiti kama madereva wangekuwa watanzania kwa jinsi walivyo waoga katu wasingewapandisha wawili hawa lakini wakongomani wale ambao vita kwao ni jambo la kawaida waliwachukua Adam na Bite hadi Iringa mjini walipowaacha jirani kabisa na hospitali ya rufaa.

?bila RB hatupokei mgonjwa wa aina hii? alisema muuguzi wa kike wa hospitali ile wakati Bite anajieleza.

Ni kweli yule muuguzi(nesi) alikuwa na haki zote za kupingana na ujio ule kwani hali aliyokuwa nayo Adam ilihitaji taarifa za polisi kwanza

?haa!!! Mama Christian, ni wewe hata siamini au nakufananisha??

wakati Bite akijiegemeza kwenye ukuta huku akiwa amekata tama alishangaa kutambulika kwake na nesi yule

?Mungu wangu mama wawili jamani!!!?

Baada ya kumkazia macho naye Bite akamtambua yule nesi kuwa waliwahi kufanya nae biashara katika soko la Uyole Mbeya na pia alikuwa jirani yake pale alipokuwa anaishi,ulikuwa mshangao mkubwa sana

?ehe!! Kulikoni tena ndugu yangu yamekukuta yapi tena mwenzangu?? alihoji nesi huku akiwa amechangamka sana safari hii

?ni makubwa sana,lakini ningeupata msaada wako kwanza kwa mume wangu ndio tungeongea vizuri shoga? alijibu Bite akiwa na matumaini tele

?ondoa shaka shoga huduma mnaipata sasa hivi tena huduma bora,daktari tunaheshimiana naye sana na pia ni shemeji yangu? nesi aliongea hayo huku wakisaidiana kumwingiza Adam ndani ya chumba cha wagonjwa,hapakuwa na maswali mengi,undugu ulitawala pale.

Adam akafanyiwa upasuaji mdogo wa kuondoa risasi katika ambao haukuchukua hata hata nusu saa damu na maji pia vikaongezwa katika mwili wake uliokuwa dhaifu sana.kufikia majira ya saa kumi na moja alfajiri Adam alikuwa amepata nafuu kubwa na aliweza kutembea japo kwa kuchechemea

?shoga nikueleze wazi tu kwamba sisi pa kufikia hapa Iringa mimi na mume wangu hatuna! Tangu niondoke ghafla niliacha sijalipa kodi nina uhakika chumba sio changu tena kwa hiyo pa kwenda hatujui? Bite alimweleza hayo mama wawili baada ya kuwa amemsogeza pembeni ili mtu mwingine asiweze kusikia

?Ondoa shaka Bite mimi kwangu pana nyumba kubwa tu!! Nimejengewa na mnyakyusa mmoja,nimemweka kwenye kiganja kwangu mimi hasikii,haoni wala hasemi,ni kaka yake na huyu daktari we mwenyewe si umeona alivyowashughulikia haraka? kwa sauti ya chini kabisa nesi alijibu

Wote watatu katika teksi wakaongozana hadi nyumbani kwa nesi ni kweli nesi hakuwa na chembe ya utani hata kidogo nyumba ile ilikuwa kubwa sana na haikuwa haki kukaliwa na watu wawili pekee vilikuwa ni vyumba sita pamoja na sebule

?karibuni! Karibuni sana! Nesi aliwakaribisha walipofika nyumbani kwake.

?asante sana ndugu yangu ama kweli ishi na watu uvae viatu? alisema Bite kwa upole sana

?usijali Bite tumeishi vizuri,hatukuwahi kugombana hata siku moja,tumetwishana matenga ya nyanya kwa nini sasa nishindwe kukutendea wema!!!? nesi alimtoa hofu Bite

Chumba walichopewa kilikuwa kikubwa cha kuwatosha kabisa,kitanda cha tano kwa sita kilikuwa saizi yao kabisa.

Adam alishangazwa sana na wema huo wa nesi lakini mshango wake uliongezeka maradufu baada ya kukutana na mume wa nesi siku ambayo walikuwa wakitambulishwa kwake kama shemeji zake yaani ndugu zake Bite.mzee huyu wa kinyakyusa aliyeitwa Gwakisa ni kama heshima ilipitiliza na kuwa kama anawanyenyekea wawili hawa.

Adam alihudumiwa na yule daktari kana kwamba alikuwa ni mgonjwa wa kisukari au alikuwa ni mtoto wa mfalme,Adam alipata farijiko kubwa sana kuishi pale

Bite kama kawaida alikuwa mwanamke wa kujituma sana,ndani ya wiki moja tayari alikuwa amepata kazi ya ndani katika nyumba nzuri waliyoishi wanafamilia watatu, mwanaume na mke pamoja na mtoto wa kama miaka mitatu wa kike aliyekuwa anasoma shule ya awali

***** ****** ****** ******

?bite mama!!?

?bee mama?

?mpeleke mtoto shule halafu baadaye mpeleke pale zahanati akapimwe jana usiku amekohoa sana?

ilikuwa sauti ya Eveline akimpa maelekezo Bite ambaye alikuwa mfanyakazi wake mpya na wa kwanza wa ndani ya nyumba yake na mchumba wake.

Ratiba ya Bite ilikuwa ni kazi kuanzia asubuhi ya saa mbili ambapo alikuwa akimpeleka Loyce {mtoto wa kaka yake Benny} shuleni na kisha akirejea a naandaa chakula cha mchana kwa siku ambayo Benny hurudi nyumbani mchana na baada ya hapo humfuata Loyce shuleni,kisha maandalizi ya chakula cha jioni na majira ya saa kumi na mbili huaga na kuondoka,ilikuwa kazi ambayo haikumtoa jasho Bite na malipo ya shilingi laki moja kila mwezi yalimtosheleza kabisa kupanga chumba kidogo walicholipia shilingi 15000 kwa mwezi

?tunashukuru sana kwa ukarimu wenu bwana na bibi Gwakisa Mungu awazidishie baraka katika kazi zenu? alitoa shukrani za dhati Adam kwa niaba ya mke wake wa bandia (Bite).

uchangamfu wake na wingi wa vituko ulifanya nyumba ya Gwakisa iwe iwe yenye shangwe na tabasamu kila siku,kitendo chake cha kuaga pale kilimsononesha Gwakisa na mkewe lakini hawakuwa na jinsi, kutoka mfukoni mwake aliwakabidhi shilingi laki mbili za kuanzia maisha yao huko waendako
Tayari Adam alianza kumpenda kwa dhati Bite uchapakazi wake na jinsi alivyomwokoa kutoka katika kifo ulichangia sana lakini kiunganishi cha mtoto Christian ndio ilikuwa chachu kubwa ya mapenzi yao.

walivyohama katika nyumba yao ya kupanga walianza rasmi kuishi maisha ya mke na mume Adam hakuwa na amani hata kidogo na familia ya Reshmail hasa baada ya kukuta katika nyumba hiyo ndogo waliyohamia magazeti yaliyobandikwa kama mapambo likisema;

?imani za kishirikina zamwondoa mheshimiwa Manyama bungeni? alitamani sana kuisoma habari hiyo kiundani iliyotoka takribani miaka mitano iliyopita lakini ilikuwa imeandikwa inaendelea ukurasa wa pili anbao haukuwepo pale ukutani

?Au walikuwa wanataka kunitoa kafara? Mungu wangu!! Niliwakosea nini mimi? alijiuliza Adam wakati wakiingiza yao ya Rambo ndani ya chumba hicho kimoja kilichotenganishwa na pazia kufanya sebule na chumba

Hisi hizo mbaya zikamfanya Adam aamue kuanzisha rasmi uhusiano na mwanamke ambaye amezaa naye mtoto pia aliyeokoa maisha yake bila kutarajia mwanamke ambaye hajawahi kumkwaza,mwanamke mpiganaji anayempa furaha tele kila siku

?Bite nataka uwe mke wangu?

?Mh!! Niwe mkeo mara ngapi mimi mkeo tayari jamani? alijibu Bite huku akichezea ndevu za Adam ikiwa ni siku ya pili tu tangia wahamie katika makazi hayo mapya

?una utani wewe mbona ulikuwa hujaniambia wala sijawahi kusikia ukiniita mume wako?

?sio lazima nikwambie tayari nina mtoto wako halafu humu ndani kuna kitanda kimoja tena kidogo tu,ulidhani chako mwenyewe!!!? aliuliza Bite kisha wote wakacheka huku wakikumbatiana na kuangukia kitandani

**** *******?

Maisha ya Reshmail jijini Dar-es-salaam yalikuwa yamebadilika sana akiwa anasubiri wakati baba yake akimtafutia kazi itakayompendeza alifurahia mara zote na Christian huku akiwa amewabadili watu wote wanaomfahamu kwa ukaribu kutokea kumwita Reshmail na sasa walimwita mama Christian na alikuwa amejivika pete ya ndoa katika kidole chake cha shahada ikwa na jina Adam na nyingine ndogo akiwa amemvisha Christian ikiwa imeandikwa Reshmail.

Hakuwa mtu wa kulialia tena wala msongo wa mawazo haukumsumbua tena aliamini nafasi ya Adam ilikuwa imezibwa vyema na Christian ambaye alikuwa Adam mpya kwake. Walilala wote, walicheza wote na kusimuliana mambo mbalimbali.alipoenda kusalimia rafiki zake walienda wote Christian mkono wa kulia.

Harakaharaka Christian alijikuta akimpenda mno Reshmail kuliko hata ilivyokuwa kwa mama yake mzazi,maisha ya kifahari ya kwao Reshmail yalimfanya Christian anawiri sana ungewakuta wakicheza bustanini kama vile wanalingana umri walibembea pamoja na kupigana kiuongouongo,kwa ufupi waliishi maisha ya kusisimua kwa kila aliyewaona.

Akiugua Reshmail ni Christian atamuuguza kwa kukaa pembeni yake bila kutoka nje hadi apone hivyo hivyo kwa Reshmail abaye alimwogesha na kumlisha.

Wakati huo Reshmail ndio alikuwa mwalimu wa Christian akimfundisha kusoma na kuandika jambo ambalo hata baba yake alilipenda na Christian alikuwa mtu anayeelewa haraka akifundishwa ,reshmail alifurahia sana.

Baada ya kukaa na Christian mwezi sita reshmail kwa mara nyingine Iringa kwa rafiki yake jambo kubwa lililompeleka huko ni harusi ya rafiki yahe huyo ambapo alitarajiwa kuwa matron wa kipenzi chake hicho.

?shoga shughuli kesho kutwa hata haujaonekana jamani au ndio mambo yetu yale haja ya kufanyiwa make up?.? Aliuliza kiutani.

Eve katika simu alipokuwa anaongea na Reshmail.

?Kesho asubuhi na mapema nakujua ,mume wangu alikuwa na mafua ndio tatizo si unajua tena.?alijibu Reshmail.

Haya mume huyo anavyoringiwa shauriro ?alijibu Eve .Christian alikuwa amependekezwa kuwa bwana harusi mdogo pamoja na Loyce (mtoto wa kaka yake Benny).

?He unatoka mume wangu asiuze sura,na jinsi alivyoandaliwa huku Dar es salaam ,utachoka mwenyewe na simtoi mpaka siku ya shughuli,atakayeruhusiwa kumuona ni bibi harusi mdogo(Loyce) peke yake wakati wa kujifunza,sitaki mwingine amuone mpaka siku yenyewe?alijibu Reshmail kwa furaha.

?Haya umeshindwa ambao hatuna waume tunalo,alijibu Eve kisha wakaagana.

Asubuhi ya siku iliyofuata majira ya saa nne asubuhi tayari Reshmail,Christian,mpambaji pamoja na dereva walikuwa ndani ya gari la baba yake (Resh)taratibu safari ya Iringa ikaanza.

?Usitupeleke kwa kasi sawa eeh,alitoa malekezo Reshmail na kukubaliwa na dereva kwa sababu hawakuwa na haraka yeyote ila mbele yao yalikuwa bado masaa mengi sana kabla ya harusi kufanyika.

Kwa mwendo wa kinyonga kabisa gar lilifika mbele ya nyumba ya Eve majira ya saa nne usiku na hakuna aliyekuwa ameschoka sana.Shamrashamra zilikuwa kubwa sana maeneo ya pale kwa Eve kelele zilizidi alipofika Reshmail, na kama alivyoaahidi kweli alishuka yeye peke yake kutoka katika gari akifuatiwa na dereva,urembo wake utadhani alikuwa amepembwa tayari kuingia ukumbini.

?Shoga tabia gain hiyo kupendeza kuliko bibi harusi??aliuliza eve kiutani baada ya Reshmail kuingia katika chumba ambacho Eve alikuwa amehifadhiwa akiwa na wapambaji wake.

?Hebu acha utani wako,kila mara unadhani tuko shuleni?mwone,?alijibu Reshmail,Eve akajiziba mdomo kwa aibu huku akiwatazama wapambaji wake waliokuwa wamejizuia kucheka lakini uvumulivu ukawashinda wakacheka kwa nguvu.

Chumba kile kikageuka kijiwa cha story kati ya Reshmail na Eve ,stori zingine zilikuwa juu ya mume wa Reshmail (Christian),shoga hadi pete?

?Sina utani mie mbona??alijibu Resh huku wapambaji wakiwa hawajui hata kinachoongelewa.

?Mama kuna mtu anataka kukuona,ilikuwa ni sauti ya kike ikimueleza Eve.
?Heh!!ushazaa na wewe??aliuliza kiutani Reshmail.Mh!!niringe huyu ni msaidizi wangu tu wa kazi anaitwa Bite,nampenda naye ananipenda pia.

?Sio kama mimi na Christian ?alidakia Reshmail ambaye tangu aingie chumba kilitawaliwa na vicheko.

?Bite humuwezi huyu anaitwa mam Christian ni rafiki yangu tangu utotoni.

?Nafurahi kukufahamu mama Christian hata mimi.

Alitaka kuondelea kuongea Bite akakatishwa na Eve.

?Anayetaka kuniona nani huyo tena?,mwambie nina mgeni" Bite akajiondokea bila kumalizia kauli yake.

Sherehe ilifana kuanzi kanisani lakini mambo yote yalikuwa saa mbili usiku maharusi wadogo walipokuwa wametangulia mbele wakifuatiwa na wana ndoa wenyewe(Eveline na Benjamin)huku nyuma yao Reshmail na Fredrick wakifunika kila kitu kwa pale mbele Christian aliteka macho ya watu huku kamera zimemulika yeye.

Tabasamu lake pana la wakati wote lililoonyesha vishimo katika mashavu yake yote lilisababisha watu wengine wahisi huenda sio kutoka Tanzania , suti yake iliyoendana kabisa na mwili wake na viatu vyake pia jinsi mkono wake ulivyokuwa umemshika kiustadi Loyce (bi harusi mdogo) ulimfanya MC ashindwe kukaa kimya ?nani mwenyewe harusi,wa mbele,nyuma au kati? aliuliza kwa mbwembwe

?mbeleeeeeeeee!!!.......nyumaaaaa!!!!? ndio majibu yaliyosikika kutoka kwa wengi

?hayaa wageni waalikwa wanasema maharusi wa katikati wamefunika sana? alidanganya MC aliyefahamu wazi Christian na Reshmail wameteka macho ya watu wengi pengine kuliko maharusi wenyewe.

Picha zilipigwa kwa wingi lakini Christian hakuonyesha wasiwasi wowote ?mh!! Katoto kazuri halafu kajanja hako? wanawake walikuwa wakinon?gonezana huku wakimtazama Christian anavyozidi kusonga mbele

?wamekatoa nje,baba yake ni mreno? alidakia mama aliyesifika kwa umbea pale mtaani aliyejulikana zaidi kwa jina la mama mwingi.hata hawakuhangaika kujibishana nae kwani walishamzoea

Taratibu kabisa kwa mwendo wa kunyata jozi hizi tatu za kuvutia ziligawanyika huku jozi mbili za wakubwa zikienda katika meza kubwa kabisa na watoto wakienda katika meza yao ndogo iliyokuwa akimeremeta soda na vinywaji vingine baridi,

?kusema ukweli sherehe imependeza,siongei kama MC bali kama ndugu Kidagaa Peter Kubalunga wengi wananiita MC K.P? alichombeza Msema Chochote (MC) na kushangiliwa sana na umati mkubwa uliohudhuria sherehe hiyo

********** ************ ********

?Dah!! Umependeza kweli sitaibiwa huko na wajanja,hebu ona ona mgongo wako utadhani huna mamba ulivyopendeza,ona kifua chako mpenzi wangu hapana nitaibiwa mke mie? Adam alikuwa akimtania Bite huku akim funga zipu yake ya mgongoni

?Acha wivu mwanaume wewe,kaa ndani usubirie ya kwako aniibe nani wataishia kutamani tu!!? alijibu Bite huku akimun?gunya midomo yake ili lipstick aliyopakaa ikae vizuri zaidi na kioo kikiwa mbele yake

?Nakupenda sana mke wangu,tambua hilo niliamua toka moyoni mwangu na wala sijutii hata kidogo najionamwenye bahati sana? Adam kwa sauti ya chini iliyomaanisha anachokisema alimwambia Bite ambaye alitulia tuli akamtazama Adam kisha akamkumbatia na kumbusu.

?nakupenda pia nakupenda sana? Bite akamwambia Adam halafu akatoka nje na kupanda teksi iliyokuwa inamsubiri kwa nje na kuondoka,Adam hakuthubutu kutoa hata pua yake nje kwani bado alikuwa na uoga wa kurejea mikononi mwa watu wabaya

Majira ya saa tatu na nusu Bite tayari alikuwa mlangoni akionyesha kadi yake ya mwaliko kwa watu wa ulinzi kisha mwanadada kutoka kamati ya maandalizi akamwongoza Bite kuelekea katika upande ambao ndugu zake na mwanamke walikuwa wamekaa,eneo la chini ya meza ya bwana na bibi harusi mdogo.Bite alikuwa tayari kama ndugu wa damu kwa Eveline walitokea kuheshimiana sana na hawakuwahi kuingia katika malumbano makubwa sana.

Amani ilitoweka katika meza ya bwana na bibi harusi wadogo,Christian alikuwa amekosa utulivu mara kwa mara alikuwa ananyanyua shingo yake aweze kuona kitu Fulani ambacho hakuna aliyefahamu ni nini kimemsibu

?Au kanaumwa tumbo?? alijiuliza matron huku akienda kwenye ile meza kumsikiliza Chriss ana shida gani.

?Chriss ni nini baba umekuwaje?? alimuuliza baada ya kumfikia

?nataka kwenda kwa mama? alijibu kwa sauti iliyojaa manun?guniko sana

?subiri kidogo mtoto mzuri nitakupeleka sawa? matron alimdanganya Chriss huku akiamini shida yake ilikuwa kwenda kwa Reshmail,kidogo Chriss alitulia japo bado hakuwa na katika hali ya uchangamfu kama awali

Muda wa kutoa zawadi ulipofika m aharusi wote katika jozi tatu walitakiwa kuwa mbele ya umati kwa ajili ya kupokea zawadi zao.Christian na Loyce waliwekewa viti wakakaa wakati Eve,Benny,Reshmail na Fredrick walisimama wima kupokea heshima hizo

?heee! We mtoto vipi? Jamani huyu mtoto kulikoni? yule mwanamke aliuliza baada ya kushikwa gauni lake na Christian alipotaka kuondoka baaba ya kutoa zawadi.

Bahati mbaya muziki ulikuwa umezimwa hivyo ukumbi mzima ulishuhudia tukio hili la kushangaza

?mamaaaa!! Mamaaaa!!? Chriss alimpigia kelele alipotaka kuondoka

ITAENDELEA.....

BAKI HAPA HAPA KWENYE APP YETU, MUITE NA MWINGINE.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21