MTOTO NISIE NA HAKI!!!!

 


MTOTO NISIE NA HAKI!!!!


Hadithi fupi ya kusisimua na kufundisha.


MTUNZI..... EMMANUEL MRISHO


MWANDISHI ...... EMMANUEL MRISHO


SIMU....0768753999


          Kwa majina naitwa mtoto maana mpaka sasa sina jina lasimi!!!


           Maisha yangu ni ya tabu sana toka nilipo wajuwa wazazi wangu kama miungu wangu japo hawakunithamini kwani sikuziliwa kabisaa!!! Baba alinipenda saaana wakati sikujitokeza na mama alitamani kuniona japo hakunitaka !!!!!


         Nakumbuka baba na mama walikuwa hawajuani kabla ila nilikuwa kwa baba kwa miaka mingi sana japo hakuniona 😓 na mimi nilitamani kumuona. fikla za baba zilikuwa kumpata mama atakae pendana naye sana kwani baba alitamani nihishi nae kwa upendo.miaka ilizidi kwenda baba akampata mama!!!


   Duuuuh!!!!! Nilifurahi sana na mimi kumpata mama kwa siku ya kwanza.nilikaa kwa mama kwa wiki mbili japo yeye hakujua kama mimi nipo karibu yake......sitosahau nilipo ona kwa siku ya kwanza mama hampendi baba namaanisha hana mapenzi ya dhati kabisaaaaaaa nilichukia sana ila mama hakujali nilishuhudia akiwa na mtu tofauti na baba yangu. Hiyo siku nililia sana kwa uchungu   oooooooohh haaaa hhiiiii


    Hali ilizidi kubadilika baada ya mama kujua nipo karibu yake jamaniiiiii mimi nilihisi kunganyikiwa kumbe mama alikuwa hampendi baba yeye alihishi na baba sababu ya pesa onaaaaa hiii baba yupo wapiiiiii ulisema utanipenda!!!!!!! Nililia saaaana siku hiyo. Nakumbuka hiyo siku mama alikunywa pombe nyingi sana tena kali ili nitoke nilitamani kumuita baba ila alikuwa mbali hakuweza kunisikiliza...  Nilimuomba mama msamaha lakini hakujali.


     Baada ya siku tatu kupita toka mama alipofahamu mimi nipo karibu yake nilisikia mama akiongea na rafiki zake kuwa anitoe kuwa ana mimba!!!!! Oooooooohh ndo siku ya kwanza kujua mimi bado ni mimba japo najielewa !!!!!!

     Nililia saaana saaaana saaaana oooooooohh Mungu wangu huyu ndo mzazi wangu na ulisema wazizi ndo Mungu wa kwanza kumbe wao ndo mashetani angalia sasa naenda kuuwawa kikatili hiviiii kwanini mimi Mungu weeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!! 

     Kiukweli nililia sana maana nilitamani kuchezea udongo,kukimbia,kuchezea maji na kunywa kama watoto wengine.

      Nikasubili sana mama abadili maamuzi ila alikuwa katili oooooooohh jamani niliwekewa vitu nisivyovifahamu viliniumiza saaana hasa upande wa moyo nilitoa sauti kubwaaa ooooooooooohhhhhhhhhhhhh mama mama nakufaaaaaaaaaaaaaaa ilinitesa sana ndoto zangu za kuchezea udongo zikayeyuka mwisho wake nipo chini ya udongo.

      Kwa atakae muona mama yangu amuulize kosa langu nini?  Siwezi mlaumu ila yeye ni Mungu gani kwangu mbona hakuwa na huruma??

      Mjue sisi watoto tuliokufa kwa sababu tunaumia saaana na sisi tuna nafsi kama nyinyi tulindeni ila mimi sitamani tena kurudi kwa mama mbaya.


       MWISHO BY EMMANUEL MRISHO

                      0768753999

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: BINAMU 🔞 SEHEMU YA 11

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 1-5

CHOMBEZO: MASSAGE ROOM🔞 SEHEMU YA 21