MUNGU ATANILIPIA:

MUNGU ATANILIPIA: Nakumbuka nililazimishwa kuolewa ila nilikubali ili kutii amri ya wazazi. Nikabahatika kupata mtoto wa kike niliyempenda sana, kwani sikuwa na raha ya kuishi na mume wangu aliyekuwa mzee sana kwa bahati mbaya mume wangu alikufa kwa ugonjwa wa kisukari. Nikabaki mimi na binti yangu kwakweli sikutaka kuolewa tena niliamua kukaa na kulea mwanangu huyu. Kweli nilimlea na kumsomesha binti yangu, alipofika chuo ndipo mambo yalipoanza kubadilika. Binti yangu akanitaarifu kuwa amepata mchumba na akaja nae nyumbani kumtambulisha kwa ushamba wangu nikashangaa kweli ile gari ya mchumba wa mwanangu na nikaona raha kwa binti yangu kumpata mwanaume mwenye pesa kama yule, ilikuwa ni kipindi cha likizo na yule bwana alikuwa akija mara kwa mara kutusalimia huku akibeba zawadi tofauti tofauti, sikuwa na shaka naye hata akiniambia anataka kutoka na mwanangu nilimpa ruhusu wanaenda halafu anamrudisha nyumbani. Siku moja ambayo siwezi kuisahau kamwe katika maisha yangu, mwanangu akaniaga ...